Loose ends Kifo cha Martha Towo

Marehemu awezi kusemwa vibaya.ila aliachishwa kazi kwa sababu ( ).
Cheo chake ni afisa mikopo?.
Mdada mzuri aliyesumbua wanaume mpaka kumiliki gari aina toyota ratics new model.
Baba yake anasema mwanae kamlea vizuri na alikuwa anatarajia kuolewa siku za karibuni. Inaweza kuwa kisasi cha mapenzi au kazi
 
Aliwek hisia

Alisema anaamini mwanae alipakizwa kwa gari na bodaboda maana kwa jinsi alivyo lazma wangeangushana tu
 
Aiseee pori la mitamba /ranchi ni hatari halafu ni tengefu ni bora serikali walikate viwanja vya makazi,niliwahi kupita hapo nikitokea kibaha kwenda Baobab ,ni hatarishi endapo ukipata breakdown.

Hivi Macho yanarecord taswira za watu? Wazee wa forensic tupeni maujuzi hapa ,kama ndiyo kuretriev data za kwenye macho wanatumia technoljia gani?

Mzee wake alisema hao ni proffesional killers means watakuwa wanafanya kila kitu kutoacha alama na ndiyo maana hata kanisani hawakuonekana japo kulikuwa na CCTV ,aliyeeonekana ni Martha tu ,kwahiyo walijua kabisa kanisani kuna CCTV hivyo walikaa nje.

Kwenye traces za Finger Prints ,Macho,Simu sitaki kwenda sana maana ni issue za kipelelezi na sitaki kuweka wazi mbinu maana tutawapa kazi nzito polisi katika kufatilia issue za kipelelezi.
 
Wewe ndiyo unatufuruga kabisa. Ukisikia watu wanaoingilia uchunguzi na kuufuruga kwa interest zao, basi ndiyo wewe sasa.
 
Intelligence yangu inaniambia pasi na shaka kuwa hili tukio ni UGOMVI WA MAPENZI..

Mzee wake alisema kwamba Martha aliacha kazi kama siku chache zilizopita na kuanza kufanya shughuli zake ,waanzie pia kazini kwake huenda alipiga mshindo akawarusha wenzake na inaoenekana alikuwa mtu wa madili mengi maana mzee wake anasema alikuwa na mali.

Kama alivyosema mshana ,case hii ni very simple kwa wapelelezi maana ina alama nyingi sana za kufatilia wahusika wa mauaji.
 
hoax
 
Chonde conde hawa waliofanya kitendo hiki kama watapatikana basi wasifunguliwe mashtaka yeyote Bali watajane wote mwanzo Hadi mwisho alafu na wao wapigwe kibiriti mbele ya camera .

Tusilee ujinga kama huu kwa kuwafunga kifungo Cha maisha.

Wanatakiwa kufa kama wao walivyo ua
 
 
Kama ndivyo, basi kesi hii ni nyepesi.
 
Chanzo cha yeye kuacha kazi ni nini? Je walimpima kugundua kama alipewa sumu?

Kwanini arudi kwao ndio tukio litokee?
Ukijaribu kuunganisha dots utaona fika plan ya tukio zima limeanzia huko shinyanga na kuja kuhitimishwa huko kibaha.

Na watekelezaji inawezekana wametokea pia huko huko shinyanga ndio maana walikuwa na uwezo wa kumteka na kumpeleka kumuua.

Haki itendeke juu ya kifo cha marehemu.
 
Ishu ya sumu imekuja baada ya figo kufeli na wataalam wa tiba za moto walithibitisha kwamba ule moto majeraha yake yasingeweza kumuua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…