Longolongo kwisha: Slaa amaliza misunderstanding hapa jf

MS naona kiswahili kinakupiga chenga maana Neno kutambua na kutomtambua hujui maana yake, kuna kumkubali, kumtambua, kumjua, kumfahamu, neno kutomtambua ni sahihi kabisa kwani hamkubali yeye kama yeye lakinianalazimishwa na katiba mbovu kumkubali kufuatana na vipengele vya ujanja ujanja vilivyoweka tangu enzi za chama kimoja, ikiwa chini ya chama kimoja, hata ukikataa kumtambua na kumkubali utaenda wapi, sasa imefikia WaTz tuache uoga tukemee mabovu tusije kuwa kama Ivory Coast, lakini inakaribiana na Ivory Cost maana hali halisi inafanana, kiufupi TZ hakuna Democrasia kwa katiba hii, ni uhuni tu
 
Huwezi kukataa process halafu kukubali zao, simple as that. Either unakataa process na zao, au unakubali process na zao.
Kuna marais wameingia madarakani kwa njia za mistuni na mitutu walipotangazwa tu hadi leo ni marais, kaingia kwa process ya mtutu wa bunduki utalazimika kumkubali kama rais upende usipende ila hutakubaliana na process.

Kwa hiyo kwa mawazo yako Mseveni kwa vile alitokea mstuni utamkataa si rais, hebu tuweke sawa hapo.

Kuna sheria zingine za kidkteta kama hizo bado ziko tanzania tunazotaka kuziondoa, NEC ikishamtangaza hata jambazi unalazimika kulitii likuongoze, ndiyo maana CDM wanasema hawazitambui process lakini wanalazimishwa na sheria elewa- 'Rais wa kulazimishwa' inabidi wakubali kwa shingo upande ni kama mapinduzi ya kijeshi utake usitake utatii. Need I say more?
 
WanaJF naomba tusiwe tunapotosha kauli za watu! Tutakuwa hatuwatendei haki waliotoa kauli hizo, Nitaendelea kuamini kuwa Dr Slaa ni mtu makini asiye kurupuka kwenye kauli na utendaji wa mambo yake. Tusiongozwe na hisia na dhana halafu tukatoa hukumu, Tunahitaji kuonyesha ukomavu fikra vya kutosha. Sio kwa sababu hapa tunaweza kuandika kila kitu basi tuwe waandika na shudu. Kinachoandikwa hapa kinaonyesha unachofikiria na ulichokuwa unafikiria kwa wakati huo.
 
Huwezi kukataa process halafu kukubali zao, simple as that. Either unakataa process na zao, au unakubali process na zao.


Wakati mwingine hii kanuni inaweza kufa.

Binti kapata mtoto wa matokeo ya kubakwa, afanyaje??? Amtupe mtoto au???
 
Mimi naona hakuna ukweli uliopindishwa na Dr. Slaa hata kidogo. Tukumbuke kwamba katika mkutano wake na waandishi wa habari wakati matokeo ndio yameanza kutangazwa na NEC alisema kabisa kuwa ameamua kusema mapema kabla ya rais kutangazwa kwa kuwa akishatangazwa rasmi huwezi kuhoji tena. Ndio kauli ileile anayoeleza hata sasa, kwamba SHERIA AU KATIBA INATAMKA KUWA RAIS AKISHATANGAZWA HUWEZI KUBADILISHA CHOCHOTE. Ila matukio yaliyofanyika bungeni na hata yanayoendelea kufanyika sasa ni kuufahamisha umma juu ya mwenendo na mfumo wa uchagguzi ulivyokuwa mbovu ili kuweza kuchukua hatua.

Watanzania inatupasa kutambua kuwa sote tunaathirika na mfumo mbovu na kwa hivyo tuna wajibu wa pamoja kubadilisha mfumo ili kuleta ahueni kwetu sote.

Matonange, mimi sielewi kwa nini watu hawaelewi somo zima na ukomavu na busara ilionyeshwa na Dr. Slaa na CHADEMA kwa ujumla. Kwanza wameonyesha ni viongozi makini ambao wanafuata sheria hata kama sheria hizo ni mbaya kiasi gani, lakini pia wameliepusha Taifa letu kuingia kwenye janga kubwa kama wangewahamasisha wanachama, wafuasi na umma kwa ujumla kupinga matokeo, tungechinjana ile mbaya maana hapo kusingekuwa tena CHADEMA au CCM bali Mtanzania anamchinja Mtanzania mwenzake, sasa ingelikuwa ndio hati miliki kwa CCM kutawala daima kwa kutumia sera ya Amani na Usalama, yaani CHADEMA kingelikuwa ndio chanzo cha vurugu wtz wengi wangeona heri CCM indelee kuwa madarakani.

MY TAKE: Kauli ya CHADEMA haijabalika, iko pale pale. Wanaona vinginevyo basi hawatutakii mema
 
Wakati mwingine hii kanuni inaweza kufa.

Binti kapata mtoto wa matokeo ya kubakwa, afanyaje??? Amtupe mtoto au???
Kwa maana yako urais wa Kikwete ni sawa na mtoto wa kubakwa inabidi tuukubali tu au? hivi mtoto anayetokana na kubakwa huitwa mtoto wa nini vile...............???
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom