LOLIONDO: Wasaliti Wenu hawa hapa

LOLIONDO: Wasaliti Wenu hawa hapa

acacia

Member
Joined
Mar 23, 2013
Posts
45
Reaction score
6
Wananchi wa Loliondo wamesalitiwa tena. Kwa kipindi hiki ni mbunge wao Saning'o Ole Telele na Mbunge wa Simanjiro Ole Sendeka. Kuna tetesi kuwa Sendeka alisafirishwa kutoka Arusha kwa gari ya Mwarabu hadi Loliondo na kulala huko akionana na Meja. Inasadikiwa kuwa alishinikiza kuwa ni lazima naye Telele aje ili kelele ziishe na aunge mkono hoja.

Telele yeye aliletwa na gari ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro. Alisiskika akisema kuwa "baada ya kuwatetea wananchi muda mrefu, sasa ni wakti wa kutetea kampuni" yaani ya OBC
 
Nimemsikia kupitia ITV kwenye taarifa ya habari ya saa mbili usiku huu akidai,baada ya kubanwa na wananchi,kuwa kama ni kujiuzulu kwa kashifa ya kutaka kugawa ardhi hiyo kwa wawekezaji basi wajiuzulu viongozi wote wa kuchaguliwa!
 
Telele anatakiwa kuonyesha kuwajibika kwake kwa kujiuzulu bila shinikizo lolote. Siku zote anatembea na Kagasheki, alienda na kagasheki Loliondo na hakutaka hata kuwaona wananchi wake waliojikusanya, alienda Loliondo akitokea Mwanza. Yeye ni wakala wa Serikali na OBC kwa sasa. Ameshindwa hata kuongea na waziri ili awashirikishe wananchi wake kabla uamuzi haujatolewa???
 
Loliondo mpoooo?
Loliondo safiiiiii?
Mbunge saafiiii?
Madiwani jee?

Haya asanteni sana na kidumu chama chetu.

Hahahahaaaaaa hii ndo tanzania na sijui kama na huko kwa wenzetu wa ulaya na mashariki ya mbali kama wana maajabu kama ya kwetu! Najaribu kuwaza kwa sauti ila naomba mtu yeyote asinisikie, sawa jamani ee?
 
Tatizo kubwa la Tanzania ni uongozi. Viongozi ndio wanaowaangusha Watanzania.
 
Tatizo kubwa la Tanzania ni uongozi. Viongozi ndio wanaowaangusha Watanzania.

Kila kiongozi arudie ahadi zake wakati wa kampeni, sasa baada ya kuchaguliwa: Tuanze na JK, Kagasheki na Telele. Kisha wengine wafuatie.... Wengine watashangaa kwamba walisema hivyo
 
uongozi wote kunzia mbunge kuihama ccm.huku kagasheki kishagawa eneo. cha kusikitisha kagawa mbele ya waandishi wa habari badala ya wananchi loliondo
 
Haya sasa Yule Msaidizi Makini wa Ole Sendeka ndugu Ole Mandalo njoo basi umtetee boss wako tena , duh! Yaani tangu CCM ifahamu kwamba 2015 wanaondoka madarakani basi wanataka kuuza kila kitu , taarifa zinaonyesha kwamba watauza hata Calculator za ofisi za umma ! Naona Aibu sana .
 
Kule Loliondo kulikuwa na ufisadi mwingi sana enzi za mzee Ruksa. Kumbe bado mambo yanaendelea. Naililia nchi yangu Tanzania.
 
Hawa wananchi wa Ngorongoro na Loliondo huwa wananichefua kweli kweli...sijui CCM imewaloga! wao huwa wanakumbwa na njaa mpaka wanaishia kula mizizi na matunda pori pamoja na kuzungukwa na utajiri mkubwa ambao unawanufaisha wawekezaji!! CCM wote wezi, hakuna msafi ...
 
Wananchi wa Loliondo wamesalitiwa tena. Kwa kipindi hiki ni mbunge wao Saning’o Ole Telele na Mbunge wa Simanjiro Ole Sendeka. Kuna tetesi kuwa Sendeka alisafirishwa kutoka Arusha kwa gari ya Mwarabu hadi Loliondo na kulala huko akionana na Meja. Inasadikiwa kuwa alishinikiza kuwa ni lazima naye Telele aje ili kelele ziishe na aunge mkono hoja. Telele yeye aliletwa na gari ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro. Alisiskika akisema kuwa "baada ya kuwatetea wananchi muda mrefu, sasa ni wakti wa kutetea kampuni" yaani ya OBC

sasa sendeka ameingiaje hapa? maji taka.
 
Alafu bado waseme tena Kidumu chama tawala mwaka 2015,itakula kwao
 
We unauliza ole sendeka kaingiaje?kupitia keybord.
ccm wanaangalia pa kuingilia kama kuna mnuso?we utashangaa m2 ndani.
 
Nimemsikia kupitia ITV kwenye taarifa ya habari ya saa mbili usiku huu akidai,baada ya kubanwa na wananchi,kuwa kama ni kujiuzulu kwa kashifa ya kutaka kugawa ardhi hiyo kwa wawekezaji basi wajiuzulu viongozi wote wa kuchaguliwa!

Yeye awe wa kwanza kujiuzulu.
 
Haya sasa Yule Msaidizi Makini wa Ole Sendeka ndugu Ole Mandalo njoo basi umtetee boss wako tena , duh! Yaani tangu CCM ifahamu kwamba 2015 wanaondoka madarakani basi wanataka kuuza kila kitu , taarifa zinaonyesha kwamba watauza hata Calculator za ofisi za umma ! Naona Aibu sana .

kama Masha aliiba hadi vitasa na mapazia hilo sishangai mkuu!
 
Lakini mpaka mwekezaji ajenge kiwanja cha ndege tena mpakani na Kenya kwani usalama wa Taifa ulukuwa wapi? Kwa mantiki hii nao ni wasaliti wa Watanzania!!! Hivi kweli kiwanja cha ndege kujengwa kinachukua siku moja?

Na watendaji walioruhusu huo mpango bado wanapumulia wapi? Niseme ni maelekezo toka juu!!! Haiwezekani hata mbunge kuruhusu hali kama ile kama hakuna mkono mrefu toka mahali fulani!!!! Na bado mikataba mipya hii tutaona kila rangi!!!! Sijui ni ya miaka 99!!!

Tutaendelea kuuzwa na kufanywa watumwa na manamba ndani ya nchi yetu!!! Another style of Colonialism!! My God my gracious!! My sons and daughters, my grandchildren!! This country is dedicated to foreigners!! You only own your blood and water in your body!!! Poor me, poor Tanzanians!!!
 
Back
Top Bottom