FairPlayer
JF-Expert Member
- Feb 27, 2006
- 4,145
- 716
Ngorongoro Constituency Session No Principal Question No To the Ministry of Sector Date Asked 10 137 NATURAL RESOURCES AND TOURISM Forestry/Fishery 15 February 2008 Kwa kuwa hivi karibuni Serikali iliongeza na kutangaza viwango vipya vya ada ya leseni ya uwindaji kwa kampuni zenye vitalu vya uwindaji wa kitalii; na kwa kuwa viwango hivyo vipya viliendelea kulalamikiwa na mengi ya kampuni husika kuwa bei hizo ziko juu mno:-
(a)Je, ni kampuni ngapi za uwindaji zinahusika na zoezi nchini?
(b) Je, tangu viwango vipya vya ada vitangazwe ni kampuni zipi zililipa na ni fedha kiasi gani?
(c) Kwa zile kampuni zitakazoghairi kulipa. Je, ni hatua zipi zitachukuliwa dhidi hayo hasa ikizingatiwa kuwa kwa ujeuri wao huo utaathiri Bajeti ya Serikali ya 2007/2008 pamoja na miradi ya wananchi ambayo ingetekelezwa kwa fedha za uwindaji wa kitalii katika maeneo ya vijiji inayozunguka vitalu hivyo?
ANSWERS TO PRINCIPAL QUESTION #137 SESSION # 10
NATURAL RESOURCES AND TOURISM WAZIRI alijibu:-
Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Kaika Telele, Mbunge wa Ngorongoro, lenye sehemu (a), (b) na (c) kama ifuatavyo:-
(a) Uwindaji wa kitalii unaendeshwa na kampuni 54 katika vitalu 158 vilivyopo katika mapori ya akiba, mapori tengefu na maeneo ya wazi. Hivyo, ongezeko la ada za uwindaji wa kitalii (vitalu na wanyamapori) kama ilivyo katika tangazo la Serikali Na. 159 la tarehe 29/06/2007 linahusu kampuni zote 54 zenye kibali cha kuendesha uwindaji wa kitalii nchini. Tangazo la Serikali Na. 159 la terehe 29/06/2007 liliwafikia wadau rasmi tarehe 11/07/2007. Wakati huo baadhi ya kampuni zilikuwa zimeshalipia vitalu kwa kiwango cha ada za zamani zilizotumika msimu wa mwaka 2006 cha USD 10,000.00 kwa kila kitalu.
(b) Pamoja na hayo kampuni 11 zimelipa nyongeza ya ada (ada za wanyamapori na vitalu) kikamilifu au sehemu yake ambapo USD 622,540.00 zimekusanywa. Kampuni 42 mpaka sasa hazijajitokeza kufanya malipo. Kampuni zilizolipa nyongeza ya ada au sehemu yake ni kama ifuatavyo:-
(i) Ortello Business Corporation (T) Ltd. imelipa ada zote za wanyamapori na vitalu.
(ii) Morogoro Hunting Safaris (t) Ltd. na Grumeti Reserves zimelipa ada kamili za vitalu.
(iii) Kampuni ambazo zimelipia sehemu ya ada za wanyamapori waliowindwa ni; Rana Tours Ltd, Northern Hunting Enterprises, Game Frontiers, Royal Frontiers, Eco Safaris, Intercon Adventure Safaris na Mwanautu & Co Ltd. Kampuni za Mwanauta & Co. Ltd na Bushman Hunting Safari Ltd zimelipia kitalu kimoja kila mmoja kati ya vitalu viwili vinavyomilikiwa na na kila kampuni hizo.
(c) Kanuni ya 11 (2) (a) (iii) ya Kanuni za uwindaji wa kitalii za mwaka 2000 na marekebisho yake, inatoa Mamlaka kwa Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori kuchukua hatua za kisheria dhidi ya Kampuni inayoshindwa kulipa ada stahili za Serikali. Hatua hizo ni pamoja na kuzifikisha kampuni husika mahakamani na kuzinyang�anya vitalu.
Mheshimiwa Spika, katika hatua za awali, Wizara yangu imewaandikia wenye kampuni za uwindaji wa kitalii wote barua ya kuwataka walipe madeni yao. Aidha Wizara imefanya majadiliano na wawakilishi wa chama cha wenye kampuni za uwindaji wa kitalii (Tanzania Hunting Operators Association (TAHOA) kuhusu suala la ulipaji wa madeni ambapo makubaliano yamefikiwa kwamba utekelezaji wa malipo ufanyike kabla ya kumalizika kwa mwaka wa fedha wa 2007/2008.
Source: http://www.parliament.go.tz/bunge/parl_question.php?pageNum_quest=2&totalRows_quest=13&memberid=1344