Loliondo, OBC, Dowans: The disturbing connection and secrets


  • Ni katika mbuga ya 'Loliondo ya Mwarabu'

Ndimara Tegambwage


WAMEPOTEZA tabasamu. Nyuso zimekunjamana. Macho yanabubujika machozi. Hawana hamu na mgeni. Wewe waweza kuwa "haramia" anayerudi kumalizia uhai wao.

Ni wanaume, wanawake na watoto ambao nyumba zao zimechomwa moto. Hawana pa kulala. Baadhi ya watoto hawajapatikana tangu walipokimbia milio ya mpasuko wa risasi na moto mkubwa uliotafuna nyumba zao kwa kasi isiyomithilika.

Hiyo ni sura unayokumbana nayo eneo la Loliondo, mkoani Arusha, lililoko zaidi ya kilometa 400 Kaskazini Magharibi mwa mji wa Arusha. Hapa wafugaji wanalazimishwa kuhama ili kupisha "utalii wa uwindaji."

Njia ambayo wahamishaji wameamua kutumia ni ile ya kuchoma moto nyumba, maghala ya vyakula na maboma ya mifugo – ng'ombe, mbuzi na kondoo.

Mkazi wa kitongoji cha Kirtalo-Karkarmoru katika kijiji cha Soitsambu anasema askari "waliovaa sare ya FFU" wakiwa na magari matatu ya aina ya Land Rover, moja likiwa na bendera nyekundu, ndio waliteketeza makazi kitongojini hapo.

Anasema walifika na kufyatua risasi angani huku wakiamuru wafugaji waondoke na ng'ombe wao. "Kufumba na kufumbua, askari wakaanza kuchoma moto nyumba zetu (pote hapa, anaonyesha) na maboma ya ng'ombe."

Unaonyeshwa lundo la majivu: Hapa ilikuwa nyumba ya baba. Hapa ya sisi watoto wake. Hapa lilikuwa ghala la chakula…Ndivyo ilivyo kote ambako moto umetumika kushinikiza wafugaji kuhama makazi yao. Ni msiba mkubwa.

Mzee Orkoskos Yiele anasema ana umri wa miaka 100. "Kaburi la baba yangu liko hapa. Kaburi la mama yangu liko hapa. Niondoke niende wapi?" Anauliza huku machozi yakimdondoka.

Ana familia ya zaidi ya watu 60. Wote hawana mahali pa kulala. Wanakoka moto. Wanapika kilichopatikana. Wanakula. Wanalala hapohapo nje wamezunguka meko – watoto kwa wakubwa.
Wiki mbili kabla ya kuchomewa nyumba, Mzee Orkoskos alikuwa na ugeni. Mmoja wa wageni alikuwa mwandishi Mussa Juma wa gazeti la Mwananchi aliyeko Arusha.

Mussa anakumbuka, "Hapa (akionyesha lundo la majivu), kulikuwa na nyumba nzuri tu kwa viwango vya huku. Tulikaribishwa na mzee Orkoskos, akatupa maziwa tukanywa na kuongea kwa muda mrefu."

Leo hakuna nyumba. Hakuna maziwa. Hakuna maboma ya ng'ombe, mbuzi wala kondoo. Hakuna furaha na vicheko. Ni kiza kisichobanduka nyusoni na ndani ya mitima ya wanakaya.

Orkoskos aliyeonekana kusononeka sana anasema, "Sijapotelewa fahamu; nimejawa hasira. Sina hamu ya kula. Wazazi wa watoto waliochoma mali zangu ni kama wajukuu zangu ambao hawana mahali pa kulala, mh…" (anashusha pumzi).

Anaeleza kuwa mtoto wake wa kike alikuwa mjamzito wa miezi minane au tisa. Wakati anakimbia moto na risasi, mimba ilitoka na kichanga ambacho kilikuwa cha kiume kimefariki. "Nani anajua kingekuwa nani katika jamii yetu au nchi nzima?" anauliza.

Kati ya ng'ombe 1,000 wa mzee Orkoskos, 100 wamepotea (hadi Jumatano iliyopita). Alikuwa anaendelea kuthibitisha mifugo iliyopotea kati ya mbuzi 800 na kondoo 700 aliokuwa nao awali.

Moto haukuchoma nyumba na mazizi peke yake. Ulichoma pia imani na utamaduni wa Wamasai. Mahali pa kufanyia tambiko, ambako ni moja ya sehemu muhimu kwa imani za jamii hii, napo palibakizwa majivu matupu.

Katika kitongoji cha Karkarmoru, Masambe Nguya anasema askari mmoja alipoona anatetemeka kwa woga, akammwagia mafuta ya petroli na "kunisukuma kwenye moto. Nilianguka chini kabla ya kuingia motoni; kutoka hapo nilikimbia bila kutazama nyuma."

Anasema pamoja na mali nyingine, mbuzi wake wawili na mbwa wachanga wanne waliungulia kwenye nyumba yake.

Hadi mwishoni mwa wiki, taarifa zilisema zaidi ya maboma 160 yalikuwa yameteketezwa katika eneo lote la Loliondo linaloitwa "Loliondo Game Controlled Area."

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Isidory Shirima anasema wafugaji wanatakiwa kuondoka kwenye maeneo hayo na "kurudi walikotoka." Anasema walipewa miezi mitano ya kuondoka lakini wamekaidi.

Anawaonya waandishi kutoandika habari zinazolenga kuwachochea wafugaji na kwamba yeye ana jukumu la "kulinda na kutekeleza sheria iliyopo hadi itakapofutwa."

Laiti Shirima angekutana na mzee Orkoskos aliyekuwa analea makaburi ya wazazi wake ambao inaaminika walikufa wakiwa na umri mkubwa; angejua kuwa kaya hiyo ina karibu karne mbili pale wanapoifukuza.

Ukoo huu na koo zingine, umekuwa katika eneo hili hata kabla wakoloni wa Kiingereza hawajalitangaza kuwa mbuga ya wanyama.
Kawaida Wamasai hawali nyama ya pori. Hivyo wamekuwa walinzi wa wanyama ambao dunia inakuja kuona, kupiga picha na kuwinda.

"Loliondo Game Controlled Area" ni eneo la ukubwa wa kilometa za mraba zipatazo 4,660. Hivi sasa eneo liko chini ya kampuni ya Ortelo Business Corporation (OBC) Limited ya Umoja wa Falme za Nchi za Kiarabu (UAE) ambayo mmiliki wake ametajwa kuwa Brigedia Mohamed Abdulrahim Al-Ali.

Kama mkoloni wa Kiingereza, kama mwekezaji Ortelo Business Corporation Limited. Walichotaka na wanachoendelea kuhitaji ni wanyama tu. Siyo binadamu.

Eneo la hifadhi, ambalo lina baadhi ya makazi yaliyoandikishwa kisheria kama vijiji, ni kubwa mno. Hata makao makuu ya wilaya, polisi, magereza, halmashauri, mji mdogo wa Wasso, vyote vimo katika eneo hili.

Kwa mujibu wa "miliki" hii, mtawala wa Ortelo anaweza kuchukua kijiko na kung'oa makao makuu ya wilaya au polisi, au hata kuyachoma moto kama askari walivyochoma makazi ya wafugaji.

Jeuri hiyo inajidhihirisha kwa tangazo linaloingia moja kwa moja katika simu yako ya mkononi ya kampuni ya Zain, pale unapoingia eneo hili.

Ghafla unasikia ujumbe wa simu unaingia na ukifungua unakuta yafuatayo kwa lugha ya Kiingereza: "Karibu Umoja wa Falme za Nchi za Kiarabu (UAE). Furahia kuwa kwako hapa kwa kutumia mtandao wa zain…" Hakika ni UAE ndani ya Tanzania.

Ni kuwepo kwa kampuni hii ya Arabuni ambako kunafanya wafugaji wawe na maoni makali dhidi ya Ortelo na serikali. Kila kitongoji unakokwenda, wahanga wanalaumu "Mwarabu" kuwa ndiye anashinikiza wahame.

Leina Koipa wa kitongoji cha Olorien katika kijiji cha Ololosokwan anasema mtoto wake wa miaka sita, Meirish Koipa, alimaliza siku mbili vichakani akiwa amekimbia moto baada ya kuona makazi yao yanachomwa na askari.

"Huyu Mwarabu ndiye chanzo cha matatizo yetu. Hii ni mara ya pili ninachomewa nyumba. Wanachoma hapa nasogea pale. Sasa angalia nimeishaanza kujenga hapa. Itakuwa hivi mpaka watuue sote..." anaeleza Koipa kwa sauti ya uchungu.

Julius Yiele (28) anasema, "Yote haya ni Mwarabu. Amehonga serikali na serikali sasa inatufukuza." Nilipomwambia kuwa kauli hiyo ni kali na yenye madai makubwa, alijibu haraka, "Ndivyo ilivyo. Sisi ni wakazi wa hapa."

Naye Ormeron Narikai wa kitongoji cha Olorien anakumbuka kuwa alikuwa na Sh. 1,150,500 nyumbani. "Ziliungulia humo pamoja na sanduku langu jipya. Acha Waarabu watuue tubaki historia, lakini hatuhami," anasema. Hapa unagundua uchungu uliokithiri.

Bali kivumbi cha kauli kilikuwa katika kijiji cha Ololosokwan, kwenye mkutano wa hadhara ambako wanakijiji walijadili uchomaji moto nyumba zao.

Mzee Yohana Sinyiu (60), baada ya kuambiwa kuwa kuna waandishi wa habari, alianza kwa kuuliza iwapo wana uwezo wa kuandika ukweli ili taarifa zifike kwa watawala na nje ya nchi. Nilitakiwa kujibu swali hilo. Nilisema, "Uwezo tunao."

Mzee Sinyiu alisema, "Tanzania ni mwanachama wa Umoja wa Mataifa. Imeridhia mikataba ya kimataifa ya haki za binadamu. Ina Katiba. CCM ina ilani yake ya uchaguzi. Vipi serikali itutendee unyama jinsi hii?"

Kwa sauti ya ukali alisema, "Andikeni. Ishawishini serikali itutendee haki; itupe usalama kama ilivyokuwa. Sisi hapa ni CCM tangu wakati wa Nyerere, Mwinyi, Mkapa na sasa Kikwete," akitaja jina mojamoja la marais.
Kama anayekaribia kudondokwa machozi, mzee Sinyiu anasema, "Hatujawahi kukaribisha upinzani hapa… Tunashangaa CCM kututendea hivi…"

Mkasa katika eneo hili unaelezwa vema katika ripoti ya kijiji yenye kichwa kisemacho, "Uharibifu uliofanywa na Operesheni ya OBC na FFU dhidi ya wanakijiji cha Ololosokwan, tarehe 4 Julai 2009 saa 1 asubuhi hadi saa 4 asubuhi."

Ripoti inataja majina ya wahanga wa operesheni: mkuu wa kaya na wote katika kaya husika. Jumla ya kaya 44 zilikumbwa na kimbunga hicho na watu 137 ama wamepoteza vifaa, vyakula, fedha, dawa za mifugo au mifugo. Ni hasara ya mamilioni ya shilingi.

Mjadala wa ripoti hii ulikuwa mzito kutokana na kauli za wanakijiji. Babu Olonyo alisema, "Tunashangaa kuona mtu anatoka Arabuni anapewa ardhi, sisi hatuna mahali pa kuchimba choo, kupumzikia na hata kuzikana."

"Sasa andika haya: Tumechoka kuishi… Mwambie mkuu wa wilaya na rais watupige bomu tufe tuishe," alisema Olonyo akichuruzika chozi kutoka jicho la kushoto.

Kanyo Ndoinyo (74) alisema, "Walikuja watawala wa Kiarabu, Kijerumani na Kiingereza. Wakatoka. Tukapata uhuru. Sasa ukoloni umerudi. Uhuru wetu umekwenda wapi?"

Ephraim Kaula (54) anauliza, "Kumetokea nini katika awamu ya nne ya utawala," na kuongeza "Tumekosa nini? Tumekaidi nini? Tuitwe wahanga wa nani… Sasa tutaendelea kulima. Tutajenga bila kujali kama tutakufa au tutapona."

Msembi Ndoinye alisema, "Wanyama ambao Wazungu na Waarabu wanakuja kuona, kuwinda na hata kubeba na kupeleka kwao, tumewatunza sisi, lakini sasa shukrani ni kufukuzwa."

Nasha Leitura aliwakomalia waandishi wa vituo vya televisheni vya Channel Ten na Star TV watangaze kuwa kitendo cha kuwachomea nyumba na mali kimewafadhaisha; ni ukatili mkubwa na uvunjaji wa haki za binadamu.

"Wewe mama (akimweleza mwandishi wa Channel Ten), usitangaze kidogokidogo. Toa yote kama ulivyoyaona na kuyasikia," alisisitiza Leitura.

Naye Koya Timan alisema serikali imeanza kuzungumzia suala la fidia kwa waliopoteza mali. Mwanamke huyo aliuliza, "Fidia ni kitu gani? Watuache na ardhi yetu ili watoto hawa na watakaozaliwa wapate mahali pa kuishi. Inatosha tu kubakiwa na ardhi yetu."

"Mwambie rais arudishe Waarabu wake huko alikowatoa. Fikisha maneno haya kwamba sisi wanawake tumekutuma," alisema Timan.

Kauli ya Mwalimu Lukuine ilikuwa kavu na kali. "Serikali inatupeleka kama nyani; inaturudisha katika umasikini…hatuna imani na serikali hii."

Mwenyekiti wa kijiji cha Ololosokwan, Julius Kaura anasema, "Utaratibu wote wa ardhi umefuatwa. Kijiji kipo kisheria. Sisi tumezoea kufuata sheria. Lakini sasa serikali ndiyo haifuati sheria. Hii siyo sahihi," alisema Kaura.

Hiki ndicho kijiji pekee wilayani Ngorogoro ambacho kinajivunia wahitimu wawili wa chuo kikuu na ambacho kimetumia mapato yake yapatayo Sh. 146 milioni kusomesha wanafunzi 128 katika miaka minne iliyopita.

Eneo lililo chini ya Ortelo lina uwanja wa ndege kwenye eneo linaloitwa Mumbarashani. Kuna madai kuwa ndege huingia na kutoka bila kukaguliwa hasa wakati wa msimu wa kuwinda. Lakini mkuu wa mkoa anasema kama hilo lina mashaka "basi wizara husika italiangalia."

Katika mbuga hizo, kwenye kilima cha Masiendilo, ndiko kuna jumba kubwa la mfalme wa UAE ambako huwa anakaa wakati amekuja kuwinda.

Pia ipo kambi kubwa ya kufikia wageni wa mfalme na wengine wanaokwenda kuwinda, pamoja na karakana kubwa ya magari katika eneo la Limawani ili kukamilisha madoido yanayohitajika kumhudumia mfalme wa UAE na wageni wake.

Tangu mwaka 1992, mfame kutoka UAE na wageni wake, wamepata uhondo katika Loliondo, huku wafugaji wakipata kibano cha ama kusogezwa au kufukuzwa kabisa katika maeneo haya.

Msukumo wa sasa wa kufukuza wafugaji, hadi kuchoma moto makazi yao, unatokana na sheria mpya ya wanyamapori ya kutaka kutenganisha mbuga na makazi ya wananchi.

Katika hili, bila shaka Ortelo watapenda lifanyike haraka kabla sheria haijaanza kutumika ili eneo lake libaki pana.

Kuna taarifa kuwa Rais Jakaya Kikwete aliishafika kwenye jumba la mfalme kwenye kilima cha Masiendilo.

Wengi nilioongea nao walitaja ziara ya kustukiza ya Kikwete kwenye makazi ya mfalme, jambo ambalo linaweza kuongeza ugumu au kuleta wepesi wa kushughulikia maisha, mali na makazi ya wafugaji.

Kwa sasa mbuga ya wanyama ya Loliondo inabaki sehemu ya UAE kama tangazo la Zain linavyosema. Maana yake ni kwamba Wamasai wafugaji na raia hawana chao; kwenye ardhi yao na ndani ya nchi yao.

Kuna haja ya kuchukua hatua, hata kufuta sheria na mikataba – vyote vya kilafi na kifisadi – inayoharamisha makazi ya wazawa na kutukuza fedha za mwekezaji. Shabaha iwe kuheshimu na kulinda haki za wananchi wafugaji na wakazi.

Rais Kikwete ana uwezo mkubwa wa kuelewa hili; labda kama hataki na bila sababu yoyote. Kilio cha wananchi kilichorekodiwa hapa ni maarifa tosha kwa mwenye nia ya kuona haki inatendeka.
 
WANA JF,

NIMEONA SI VIBAYA KUSHARE ARTICLE HII NANYI. KUNA MTU KANITUMIA. SAMAHANI KWA WALE AMBAO WAMESHA ISOMA

Wapendwa
im just accessing net now after the short but long and distressing trip to Loliondo some six hour roughest drive from Arusha town through Ngorongoro crater the so called seventh wonder of this world .. within and surrounding it is one of the saddest stories of Wamaasai pastoralist communities who have been victims and survivors of a century long international and national propaganda on conservation of natural resources and hence the introduction of powerful lobby and protectionist legal frameworks that have facilitated their systematic dispossession, displacement and what seems to be a final move towards complete eviction that started since July this year led by the state

the eviction led to a devastating impact to the whole community , in the affected area all their BOMAs have been burnt to ashes, one woman raped by seven militia but too afraid to admit .. one miscarried a seven month pregnancy no treatment to date ... women and children traumatized some hysterical , with a sound of an approaching car they just take off and run ......there is no water for them and the animals since they are now prohibited to graze in the evicted areas ... no food , no transport .. no health facility ...

General feeling is fear and despair ...all initiatives to organize on the ground have and are being silenced ...older and young men are now being apprehended and imprisoned under the pretext that they have/are destroying the environment ....women have tried to rally appealing to the District commissioner in vain ....


We were closely followed up by militia and security as we wanted to visit the United Arab Emirates Company that has been granted a contract to hunt in the affected area since 1992 .....What is strange is the fact that this company also seems to be/representing the UAE royal family .. as we approached the area sms on our phones welcomed us to the UAE meaning all correspondences were to use UAE code number ... practically its another sovereign state within Tanzania.... we were shocked to find out that this is a private company that has been guarded by state machinery ...police and security 24 hours seven days since 1992! More shock when the police and security told us that the area was the UAE ---PALACE!!!!!!!!!!!!!!!!! and we were not allowed in without permission ........cso on ground told us that the UAE royal king visits on an annual basis complete with festivals and unparalled sex work and workers from the East all flown in directly no immigration nothing ..............communities claim that some flights carry back live animals no one know how many since 1992 and who is getting what out of this .........there are some shoddy contract between surrounding eight villages and the company initially they were given
3 million tshs a year which was all of a sudden raised to 25 and 50 before eviction............. place is complete town with airstrip/ airport capacity of Boeing 747...cars with UAE registration numbers flown in directly ....the question is who is destroying the environment ?.....

In the meantime the DC and security made follow up on us asking whether we took pictures at the royal palace ..............to them this is the most important concern and not the Maasai.... its sad and shameful! Biggest question is how can we rise towards accountable leadership in Tanzania , Afrika?

We were a team of 22 under the leadership of FemAct with CSO in Arusha ,in Loliondo and the media ... full report is being prepared to be submitted Tuesday for input and a plan for feedback with Fem Act Directors / chairpersons on Wednesday or Thursday......... when we will also chart out a plan to move forward this struggle and for full blown advocacy at all levels .....


there are immediate , medium and long term needs on the ground ... social services, legal , medical and psychological support to the survivors while tackling the larger question on the legality of the eviction, land and livelihood .......... plans were made to provide some immediate though limited legal support .........but much was brainstormed to be included in the report to be shared with Fem Act next week.....will keep you updated..........



Usu
 

Attachments

  • Initial Reflections on Loliondo Trip.doc
    27.5 KB · Views: 104
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

TAMKO LA MUUNGANO WA ASASI ZA KIRAIA (FemAct) NA MITANDAO YA WAFUGAJIKUHUSU KUKIUKWA KWA HAKI ZA BINADAMU NA HAKI ZA RAIA KATIKA WILAYA YA NGORONGORO KWA MASLAHI YA MWEKEZAJI; KAMPUNI YA ORTELLO BUSINESS CORPORATION (OBC)

Sisi Muungano wa Asasi za Kiraia zinazotetea Usawa wa jinsia, haki za binadamu na maendeleo na ukombozi wa wanawake kimapinduzi (FemAct) kwa pamoja na Mitandao ya Wafugaji mkoa wa Arusha tumeguswa na kusikitishwa na vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu, haki za raia na uvujaji wa sheria katika kutekeleza oparesheni ya kuhamisha wafugaji wakaazi wa jamii za Kimaasai unaoendelea katika wilaya ya Ngorongoro, Tarafa ya Loliondo inayofanywa na vyombo vya dola kwa maslahi ya mwekezaji kutoka Uarabuni, Kampuni ya Ortello Business Corporation (OBC).

Baada ya taarifa za kushitua za watendaji wa serikali kukiuka haki za binadamu dhidi ya jamii za kimasaai kutangazwa katika vyombo vya habari kadhaa ndani na nje ya nchini, FemAct na Mitandao ya Wafugaji, tuliamua kufuatilia kwa karibu ili kubaini usahihi wa taarifa hizo. Kati ya Agosti 19 na 23 2009, viongozi wa mashirika wanachama wa FemAct walifanya ziara maalum katika vijiji vya Ololosokwan, Soitsambu, Olorien – Magaiduru na Arash, pamoja na kutembelea kambi ya Oterloo Business Corporation (OBC) na uongozi wa wilaya ya Ngorongoro kwa lengo la kubaini na kuthibitisha kiwango na namna watendaji wa serikali wanavyoshirikiana na mwekezaji wa OBC kunyanyasa na kutesa raia wakaazi wa vijiji vilivyotajwa hapo juu.

FemAct na Mitandao ya Wafugaji wamebaini kuwa kampuni ya OBC ilipewa kitalu cha uwindaji mwaka 1992 na serikali kupitia wizara ya maliasili. Hatua hii ilipingwa kwa nguvu zote na kuibua mjadala wa kitaifa ulioitwa “Loliondogate scandal”. Kitalu hiki kiko katika eneo linalomilikiwa kisheria na vijiji vya Loliondo, hivyo wafugaji wanaishi kihalali katika eneo hilo. Aidha, imebainika kuwa serikali kwa kutumia jeshi la polisi, hususan kikosi cha kutuliza ghasia cha FFU, wakishirikiana na askari wa OBC, kuanzia mwanzoni mwa mwezi julai, wamekuwa wakihamisha kwa nguvu, raia wenyeji na wakaazi wa jamii za kimaasai kwa kisingizio cha kudhibiti uharibifu wa mazingira, bila kujali uhalali wao wa ukaazi kisheria. Kuwaondoa kwa nguvu wafugaji na wakaazi wa jamii za kimasaai katika vijiji vyao vya asili, pasipo kuzingatia uhalali wa uwepo wao, ni ukiukwaji mkubwa wa haki za raia, haki za binadamu na ukiukwaji wa sheria na katiba ya nchi.

Wakati wa ziara ya kikazi ya viongozi wa FemAct na Mitandao ya Wafugaji tumebaini na kuthibitisha yafuatayo: -

1. Kwamba oparesheni za serikali na OBC zinafanyika katika maeneo ya wakaazi ambao wanayamiliki kihalali kwa mujibu wa sheria ya Ardhi ya Vijiji ya 1999 hivyo Wamaasai siyo wavamizi kama inavyodaiwa na serikali na kampuni ya OBC;


2. Kwamba kuna ukiukwaji uliokithiri wa haki za binadamu, haki za raia na sheria ikiwa ni pamoja na kuchoma maboma (nyumba za kiasili za Kimaasai) pasipo kuwapa makazi mbadala; ubakaji na udhalilishaji wa wanawake ikiwa ni pamoja na vitendo vilivyopelekea baadhi ya wanawake wajawazito kutoka mimba, watu kukamatwa na kuteswa, chakula kuharibiwa, na mchakato nzima kutofuata sheria na taratibu;


3. Kwamba madai ya serikali na mwekezaji kuwa wananchi wa jamii za wafugaji za kimaasai wanaharibu mazingira ni madai ya uongo. Isipokuwa, uharibifu wa mazingira uliopo katika eneo la mgogoro ni ule unaosababishwa na kampuni ya OBC, kama vile kujenga kiwanja cha ndege katika mapito na mazalio ya wanyama pori, kelele zinazosababishwa na kutua na kuruka kwa ndege, kujenga majengo ya kudumu katika maeneo ya hifadhi ya wanyama, na uchukuaji wa maji kutoka katika vyanzo vya maji vya mbugani; na


4. Kwamba kuna mapungufu mengi ya taratibu za ki-sheria ikiwa ni pamoja:-
a) Uingiaji wa mikataba kati ya OBC na Serikali za Vijiji, mikataba ambao inaonyesha serikali imesaini mikataba na vijiji kwa niaba ya OBC iliyosaini kama shahidi katika mikataba hiyo.
b) Kutekwa kwa mawasiliano ya makampuni ya simu ya Tanzania katika maeneo yaliyo karibu na kitalu cha OBC ambacho hakina mipaka inayoonekana. Mfano, ukiwa eneo hilo unapata ujumbe mfupi was simu (sms) kutoka kampuni ya ETISALAT unaokukaribisha na kusema, “karibu katika Umoja wa Nchi za Falme za Kiarabu”.
c) Kujenga kiwanja cha ndege na kuwepo kwa mawasiliano ya Anga ya moja kwa moja kutoka eneo la kitalu kwenda nchi za nje. Kiwanja hicho hutua ndege kubwa zenye uwezo wa kubeba takribani watu mia nne na magari kadhaa.
d) Kutokueleweka utaratibu wa ukusanyaji wa kodi mbalimbali kwa sababu hakuna taarifa zinazoonyesha iwapo Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) yanakusanya mapato kutokana na magari yanayoingizwa na kutumika nchini yakiwa na namba za usajili wa Nchi za Falme za Kiarabu pamoja na rasilimali zinazochukuliwa moja kwa moja kupitia uwanja huo.
e) Kampuni ya OBC inapewa hadhi ya kidiplomasia na wakati ni kampuni iliyosajiliwa kama kampuni nyingine. Mfano, kambi ya kampuni hiyo inalindwa na FFU, jeshi la polisi na chombo cha dola! Aidha kuna vikundi-kazi vya serikali katika ngazi za wilaya hadi taifa vilivyoundwa kuratibu shughuli za kitalu hicho. Viongozi wa FemAct pamoja na Mitandao ya Wafugaji walikataliwa kuingia ndani ya kambi ya kampuni husika ila, badala yake, waliondoshwa kwa kusindikizwa na FFU na baadaye kusimamishwa na kuhojiwa na FFU walioagizwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha na Wilaya ya Ngorongoro.

5. Kwa matukio haya FemAct inarejerea na kuthibitisha kauli yake ya Mei 22 mwaka huu kuwa dola ya Tanzania imetekwa na hivyo kuwatumikia wachache; wawekezaji wenye mitaji na hata mafisadi kwa gharama ya wananchi waliowengi wanaoteseka.

Kutokana na hayo tuliyoyabaini na kuthibitisha, FemAct na Mitandao ya Wafugaji, wanadai:

1) Serikali isimamishe mara moja oparesheni zinazoendelea kuamisha wafugaji katika Wilaya ya Loliondo na sehemu nyingine , ambazo zinakiuka kwa kiwango kikubwa haki za binadamu na za kiraia na taratibu za ki-sheria;
2) Serikali iwajibike kuchukua hatua za ki-sheria dhidi ya watendaji wake wote watakaobainika kuhusika na ukiukwaji wa haki za binadamu na ukiukwaji wa sheria na katiba ya nchi dhidi ya wananchi wakaazi katika wilaya ya Ngorongoro;
3) Wahanga wa operasheni katika wilaya ya Ngorongoro wapelekewe misaada ya ya dharura ya kibinaadamu haraka sana iwezekanavyo, hususan maji na huduma za matibabu kwa akina mama, chakula na mahema;
4) Wahanga wote wa operesheni walipwe fidia kutokana na kuharibiwa na kupotelewa kwa mali zao;
5) Serikali iwajibike kufafanua sababu za kuipa kampuni ya OBC hadhi ya kidiplomasia;
6) Serikali itoe maelezo ya kina juu ya usimamizi na ufuatiliaji wa mapato (TRA), uendeshaji wa shughuli za mawasiliano ya simu (TCRA) na matumizi ya anga ya Tanzania (TCAA), na hadhi ya ukaazi wa wageni (IDARA YA UHAMIAJI) wanoendesha kampuni ya OBC;
7) Serikali itoe tamko rasmi kuhusu hatma ya wafugaji Tanzania; na
8) Serikali kutoa ufafanuzi wa kina wa mgongano wa ki-sheria kati ya Sheria za ardhi na Sheria za wanyapori, hususani Sheria ya Ardhi ya Vijiji ya 1999 na Sheria ya Hifadhi ya Mamlaka ya Ngorongoro ya 1959.
9) Wanaharakati na wananchi wote katika ujumla wetu tujitokeze waziwazi kupinga vitendo vinavyofanywa na serikali dhidi ya wananchi wa jamii za wafugaji na wakaazi wengine katika wilaya ya Ngorongoro.
10) Vyombo vya habari viendelee kufichua maovu yote ya kukiukwa kwa haki za raia na haki za binadamu yanayofanywa na watendaji wa serikali kwa kushirikiana na mwekezaji wa kampuni ya OBC dhidi wananchi wakaazi wa jamii za wafugaji katika wilaya ya Ngorongoro.
Serikali ifuatilie na kusimamisha mara moja vitisho vinavyotolewa kwa viongozi wa mashirika yasiyo ya kiserikali na wananchi wanaojaribu kukataa ukatili huu na ukiukwaji wa haki za binadamu na haki za raia

Imetolewa na FemAct na kusainiwa na
1. Tanzania Gender Networking Programme (TGNP)
2. Legal and Human Rights Centre (LHRC)
3. Concern for Development Initiatives in Africa (ForDIA)
4. Youth Action Volunteers (YAV)
5. The Leadership Forum (TLF)
6. Coast Youth Vision Association (CYVA)
7. Walio Katika Mapambano na AIDS Tanzania (WAMATA)
8. Tanzania Media Women’s Association (TAMWA)
9. Youth Partnership Countrywide (YPC)
10. Tanzania Human Rights Fountain (TAHURIFO).
11. HakiArdhi
12. Women Legal Aid Centre (WLAC) (WILDAF)
13. Lawyers’ Environmental Action Team (LEAT)
14. Tanzania Ecumenical Dialogue Group (TEDG)
15. HAKIELIMU
16. Women Fighting Against Aids in Tanzania Trust Fund (WOFATA)
17. Taaluma Women Group (TWG)
18. Marcus Garvey Foundation (MGF)
19. Tanzania Coalition on Debt and Development (TCDD)
20. ENVIROCARE
21. Pastoralists Forum
22. Women’s Dignity (WD)
23. Pastoralists Indigenous NGO’s Forum (PINGO’S FORUM)
24. Ngorongoro NGOs Network (NGONET)
25. Ujamaa Community Resource Trust (UCRP)

27 Agosti 2009
 
"Dear Guest, welcome to the UAE, enjoy the best network coverage...

For Directory service call 181 and for GPRS, MMS, 3G call Etisalate...


Have a Pleasant stay at UAE"
Hayo ni maneno utakayo pokelewa nayo kwenye simu yako ya mkononi na mabango ukiingia eneo la Loliondo liliouzwa kwa kampuni ya OBC (Ortello Business Company).

Hawa ndugu zetu wamasai wamezaliwa hapo na wamekulia hapo lakini hawana haki ndani ya nchi yao?

Kibaya zaidi FFU ndo wanalinda hiyo sehemu, FFU wanatumia magari ya waarabu.

Tanzania imevamiwa au Imeuzwa? Yaaani nchi ndani ya nchi nyingine?
 
Haaa, pole kwa kuyajua hayo leo. Uliza wizarani wana landrover ngapi za huyo Ortello!
 
Last edited:
Mkuu,

Ya Loliondo mbona ni zaidi ya decade sasa!

Unataka Stan K afufuke?

Loliondo iliuzwa na Mzee wa Ruhusa miaka hiyooooo!
 
nadhani kuja haja ya kuweka kamati ya ukombozi ili hayo maeneo yote yakombolewe tena na yarudi Tanzania
 
Anyway sioni hapo tatizo lipo wapi, kwa sababu umesemea hayo maneno na mabango unayapata mara uingiapo kny eneo lililo uzwa (nafikiri hata hili si kweli, ukweli unatakuwa lililokodishwa-leased). Kama ni kweli, wakazi wa eneo hilo, na watumiaji wa eneo hilo ni hao waarabu wa UAE, so watakuwa wameweka mitambo ya mawasiliano ambayo inaweza kuwaunganisha wao na nyumbani kwao UAE!

Baada ya kuisha lease yao na kama serikali haitataka kurenew, basi hao jamaa itabidi waachie eneo warudi zao UAE!

Kwa uelewa wangu set ups za aina hii ni common sana sehemu za migodi, mashamba makubwa, vitaru vya utalii (kama kule Grumeti Hotels Serengeti) etc

Can't see a problem here, labda tatizo kama hiyo mitambo yao inawaathiri wananchi wanaoyazunguka hayo maeneo. Vinginevyo tatizo kuu litakuwa lile kuruhusu ubinafsishwaji wa rasilimali za taifa, kama hatukuwa tayari kufanya hivyo, vinginevyo kama umekubali kubinafsisha rasirimali, lazima ukubali pia hao wawekezaji wanapotumia rasirimali hizo kutokana na mikataba tuliyosainiana!
 
Anyway sioni hapo tatizo lipo wapi, kwa sababu umesemea hayo maneno na mabango unayapata mara uingiapo kny eneo lililo uzwa (nafikiri hata hili si kweli, ukweli unatakuwa lililokodishwa-leased). Kama ni kweli, wakazi wa eneo hilo, na watumiaji wa eneo hilo ni hao waarabu wa UAE, so watakuwa wameweka mitambo ya mawasiliano ambayo inaweza kuwaunganisha wao na nyumbani kwao UAE!

Baada ya kuisha lease yao na kama serikali haitataka kurenew, basi hao jamaa itabidi waachie eneo warudi zao UAE!

Kwa uelewa wangu set ups za aina hii ni common sana sehemu za migodi, mashamba makubwa, vitaru vya utalii (kama kule Grumeti Hotels Serengeti) etc

Can't see a problem here, labda tatizo kama hiyo mitambo yao inawaathiri wananchi wanaoyazunguka hayo maeneo. Vinginevyo tatizo kuu litakuwa lile kuruhusu ubinafsishwaji wa rasilimali za taifa, kama hatukuwa tayari kufanya hivyo, vinginevyo kama umekubali kubinafsisha rasirimali, lazima ukubali pia hao wawekezaji wanapotumia rasirimali hizo kutokana na mikataba tuliyosainiana!

huu ni ukosefu wa adabu na kitendo cha dharau na kuuingilia uhuru wetu.

sidhani kama ukienda Chinatown US basi utakutana na Welcome to china kinds of S"&*T just because hiyo sehemu kuna wachina wengi.

there are thousands of chinese san fransisco,lakini verizon,AT&T,FCC etc hawajaruhusu huu upuuzi.

ndio ubaya wa kuwa ombaomba.dignity ya mtanzania iko lowest.i reminisce the good old days when we used to be counted as a nation(nyerere times) despite our poverty.we had respect.

it seems our current administration favors sifa za kijinga za "ideal investment" country to national sovereign and nation respect.
 
Anyway sioni hapo tatizo lipo wapi, kwa sababu umesemea hayo maneno na mabango unayapata mara uingiapo kny eneo lililo uzwa (nafikiri hata hili si kweli, ukweli unatakuwa lililokodishwa-leased). Kama ni kweli, wakazi wa eneo hilo, na watumiaji wa eneo hilo ni hao waarabu wa UAE, so watakuwa wameweka mitambo ya mawasiliano ambayo inaweza kuwaunganisha wao na nyumbani kwao UAE!

Baada ya kuisha lease yao na kama serikali haitataka kurenew, basi hao jamaa itabidi waachie eneo warudi zao UAE!

Kwa uelewa wangu set ups za aina hii ni common sana sehemu za migodi, mashamba makubwa, vitaru vya utalii (kama kule Grumeti Hotels Serengeti) etc

Can't see a problem here, labda tatizo kama hiyo mitambo yao inawaathiri wananchi wanaoyazunguka hayo maeneo. Vinginevyo tatizo kuu litakuwa lile kuruhusu ubinafsishwaji wa rasilimali za taifa, kama hatukuwa tayari kufanya hivyo, vinginevyo kama umekubali kubinafsisha rasirimali, lazima ukubali pia hao wawekezaji wanapotumia rasirimali hizo kutokana na mikataba tuliyosainiana!

Mmeshanyweka brother hapo hutemi dawa.Mama Siti Mwinyi alishainywa mazee waulize watu waliofukuzwa kazi akina Babu Director wa uwindaji na wanyama pori kipindi hicho na kumwekwa muislamu mwenzao Ndolanga na kuasaini mikataba kwani Babu alikataa akisema hakusomea uharibifu wa mazingira, akafukuzwa kazi bila mafao. Huu ni upuuzi mtupu nina hasira sana na ile Loliondo.
 
suala ni kujiunga pamoja kwa kura tuwatoe madarakani,la sivyo tutabaki kung'aka bila chochote kufanyika,ni aibu ujinga na ubinafsi wa mafisadi papa na uchwara wanaopewa mil 100 kusaini.Tuamke
 
Malyamungu, Kimweri

Ndo maana mimi kifupi nikasema, tatizo si hicho tunanachoona hawa the so called wawekezaji wanafanya, issue ni kuruhusu huo ubinafsishwaji wa hizo mali tena kwa makubaliano na mikataba isiyo na kichwa wala miguu. Matokeo yake ndo haya tunayo yaona, mala wengine wanaachia sumu kny vyanzo vya mito etc

Lakini tungekuwa makini, haya malalamiko hayangekuwapo sasa! So hili tunallliona sasa si tatizo...tatizo ni namna gani hawa jamaa wameweza kujipenyeza Tz na kufanya hayo wanayofanya! Unavyowalalamikia hao wa Loliondo, on background wengine wanapewa almost the same mikataba huko Serengeti, Selous etc!
 
Anyway sioni hapo tatizo lipo wapi, kwa sababu umesemea hayo maneno na mabango unayapata mara uingiapo kny eneo lililo uzwa (nafikiri hata hili si kweli, ukweli unatakuwa lililokodishwa-leased). Kama ni kweli, wakazi wa eneo hilo, na watumiaji wa eneo hilo ni hao waarabu wa UAE, so watakuwa wameweka mitambo ya mawasiliano ambayo inaweza kuwaunganisha wao na nyumbani kwao UAE!

Baada ya kuisha lease yao na kama serikali haitataka kurenew, basi hao jamaa itabidi waachie eneo warudi zao UAE!

Kwa uelewa wangu set ups za aina hii ni common sana sehemu za migodi, mashamba makubwa, vitaru vya utalii (kama kule Grumeti Hotels Serengeti) etc

Can't see a problem here, labda tatizo kama hiyo mitambo yao inawaathiri wananchi wanaoyazunguka hayo maeneo. Vinginevyo tatizo kuu litakuwa lile kuruhusu ubinafsishwaji wa rasilimali za taifa, kama hatukuwa tayari kufanya hivyo, vinginevyo kama umekubali kubinafsisha rasirimali, lazima ukubali pia hao wawekezaji wanapotumia rasirimali hizo kutokana na mikataba tuliyosainiana!

NL,

Acha hizo madharau kabisa, yaani unaubinafsisha uhuru wako hivihivi.

Yaani ndani ya Tanzania kuna ka nchi(labda tuite ufalme) kenye uhuru kamili wa kufanya mambo yake tena kanawabugudhi mno wananchi wazawa wa eneo husika,mbaya zaidi ni hatua ya serikali kuwasulubu wananchi wake kwa kuwahamisha kwenye makazi yao ya asili na kuwaharibia mali zao.

Waarabu wamejenga uwanja wa ndege mkubwa kuliko KIA na JNIA.

Hizo set up unazozizungumzia kwamba zipo GRUMETI, ni GRUMETI ya wapi hiyo? kama ni ya serengeti sio sahihi, hakuna himaya ya namna hiyo(ya welcome to UAE) hata ukienda hadi mahoteli ya kempiski hakuna kitu kama hicho.

kwahiyo usichekelee kwa wamasai kugeuzwa watumwa ndani ya ardhi yao, nchi yao ya asili kwa uamuzi uliofanywa na watanzania wachache kwa manufaa yao binafsi.
 
..... uamuzi uliofanywa na watanzania wachache kwa manufaa yao binafsi.

MM,

Yote uliyoongea mwisho wake umekuja kny hoja yangu ya msingi.......UBINAFSISHAJI USIO KUWA NA TIJA KWA TAIFA...soma tena post zangu mbili hapo juu, hilo ndilo ninalo lilaumu mimi!

Kuweka kibao kikisema ''Welcome to UAE'' hata mtanzania yeyote anaweza kuweka kibao kikasomeka hivyo, so issue hapo kwangu mimi sio kuweka hicho kibao au hayo mawasiliano ya simu yanayofanyika huko, tatizo langu mimi ni hao waliowaruhusu kufanya hayo wanayofanya!

Nimesema kinachotokea Loliondo kinatokea sehemu nyingi sana ambapo kuna hao the so called wawekezaji, though sehemu nyingine udhalilishaji wa watanzania huwezi kuona kwa macho ya nje hivi hivi, kama huko Grumeti ambako mi binafsi nimeshafanya kazi pale, na pale kuna air strip pia.....! Wananchi wanaozunguka hotel zile wanapata unyanyaswaji wa hali ya juu sana...sielewi unabisha nini hapa!

Ukienda huko kwenye migodi the same thing is happening. Kuna hotel moja huko manyara (jina limenitoka), walikuwa wanaruhusiwa foreigners tu kupata huduma hapo, hiyo hotel hivi karibuni ilitembelewa na Waziri Mwangunga......sasa wewe bado anayaona ya Loliondo tu!

Kwahiyo point yangu ni hao wawekezaji wanachokifanya ni halali pengine ktuokana na mikataba au makubaliano waliyoingia pamoja na serikali na pia wanabebwa sana na wadosi wa serikali kwa maslahi yao binafsi! So kitu cha kwanza tunachotakiwa kufanya kuondokana na haya, ni kuwaong'oa hawa viongozi ambao wanaiendesha serikali kwa manufaa yao binafsi then pili kufanya marekebisho makubwa kwenye sheria na taratibu za uwekezaji ikiwa ni pamoja na kuiangalia upya mikataba iliyopo!
 
Anyway sioni hapo tatizo lipo wapi, kwa sababu umesemea hayo maneno na mabango unayapata mara uingiapo kny eneo lililo uzwa (nafikiri hata hili si kweli, ukweli unatakuwa lililokodishwa-leased). Kama ni kweli, wakazi wa eneo hilo, na watumiaji wa eneo hilo ni hao waarabu wa UAE, so watakuwa wameweka mitambo ya mawasiliano ambayo inaweza kuwaunganisha wao na nyumbani kwao UAE!

Baada ya kuisha lease yao na kama serikali haitataka kurenew, basi hao jamaa itabidi waachie eneo warudi zao UAE!

Kwa uelewa wangu set ups za aina hii ni common sana sehemu za migodi, mashamba makubwa, vitaru vya utalii (kama kule Grumeti Hotels Serengeti) etc

Can't see a problem here, labda tatizo kama hiyo mitambo yao inawaathiri wananchi wanaoyazunguka hayo maeneo. Vinginevyo tatizo kuu litakuwa lile kuruhusu ubinafsishwaji wa rasilimali za taifa, kama hatukuwa tayari kufanya hivyo, vinginevyo kama umekubali kubinafsisha rasirimali, lazima ukubali pia hao wawekezaji wanapotumia rasirimali hizo kutokana na mikataba tuliyosainiana!

Tatizo lipo kaka, tena kubwa tu na tukiliendekeza kila mtu atakuja kukodisha maeneo ya uwekezaji hapa nchini, atakuja mtu na pesa yake akodishe kigamboni na afunge mitambo yake ya mawasiliano, mwingine akodishe zanzibar, mwingine mbeya, arusha, kilimanjanro, dodoma, dar, etc mbona itakuwa fujo? akija mwenye dau kubwa atakodisha tanzania yote. Nakumbuka enzi ile Iddi Amin alitaka kukodisha Kagera unajua kilicho mpata? Tukiindekeza hii tabia tutauza utu na heshima yetu.
Hii ni aibu kwetu na kwa taifa.
 
Tatizo ni kubwa wewe Next level mwenyewe you are problem!

Ni kawaida ya watu wa sisiemu ndivyo mlivyo!! Baada ya kuukimbiza mwenge na kula mnavyopewa hizo chauro hamtaweza kuona kuna tatizo. Let us go with facts and figures ni nani katika hizi serikali tatu anaweza akanipatia takwimu,,kwa miaka 18 ya Ortelo na vitalu vyote ni kiasi gani tumepata!! Kama ningekua mtawala kwanza biahara ya kuwinda kitallii haihitaji mtaji mkubwa ningesema ni kwa watanzania tena weusi tu akija mmanga haruhusiwi acha waniite mbaguzi. Ukitaka kuona wababe tambea mwanangu uone kuanzia Dubai mapaka Hawaii wazawa kwanza!!! Ukinibishia nakutafuta nikutie chale au nikate sikio kieleweke!!!
 
Hatuna viongozi wenye kutetea maslahi ya taifa wapo wa kutetea maslahi ya familia zao tu
 
Wananchi wa maeneo hayo wakitaka kupika nyama mpaka waombe kibali, kuna msako wa FFU kila mara kukagua vyungu kama wamepika nyama kwa kuua wanyama wa UAE waliopo TANZANIA. Nakulilia sana Tanzania .....Huwa ninajiuliza hivi mtu ukiwa kiongozi utu unapotea? Huoni ? Husikii? Wewe ni kiongozi wa nani?
Mimi naona wakati mwingine labda ni vigumu sana kumwajibisha Rais, labda tuwabane wakuu wa wilaya na mikoa. Wengine tutasema siyo kazi zao, au siyo wao waliotia sahihi mikataba, lakini damn it KAZI YAO NAMBA MOJA ni kulinda amani na usalama wa raia.Siyo kulinda usalama wa makabaila. Kama wao wanaona manyanyaso haya na hawana uwezo wa kuyatatua, the least they can do ni kujiuluzu, where is your dignity people?
Leo kodi yetu inatumika kukagua vyungu vya wananchi wamepika nini? Next time wataingia mkataba wa kujenga kiwanda cha nguo na UAE, mwisho wake tutaanza kukaguliwa chupi kama zimetengenezwa na kiwanda cha nguo cha UAE !!
Tufanye nini?? Wanajamii wa maeneo hayo wekeni namba za simu au emails za mkuu wa wilaya, mkuu wa mkoa na mbunge pia,and let us send them a lot of emails and lots of phone calls, to make their lives a living hell just like these wananchi, i am very very mad !!!
 
Back
Top Bottom