Sidhani kama Mwarabu anahusika, yeye Loliondo kaichukulia kama sehemu ya kuficha uovu kulingana na maadili ya dini yake. Hana shida kimsingi.
helkopata ngapi ziko huso waso kusaidia kutafuta hao wauji au helkopta ziko kwa ajili ya kumsafirisha mbowe dar to arusha..
Huwa sipendi kusema uongo FF ukitaka niPM nitakujuza mwarabu anachokuja kukifanya Loliondo lakini si uwindani kama inavyofahamika.Wewe umeleta mada nzuri ya kutujuza yanayoendelea Loliondo mara ghafla umewarukia kuonesha mfano Waarabu na umeona haitoshi unaingiza na dini yao sasa? Wamekufanya nini Waarabu na dini yao? Na maovu yepi ya dini yao wanayokuja kuyaficha Loliondo?
Ndiyo hivyo ndugu yangu watu tunafikiria waarabu pekee ndiyo wanaweza kutenganisha vichwa na viwili wili kumbe hata bongo tumefikia huko!
Wangewaua wamiliki wa dowans si ingekuwa bora zaidi!
WanaJF,
Poleni na shughuli za ujenzi wa Taifa letu.
Habari ambazo nimezipata sasa hivi kutoka Loliondo kuwa hali ya mji huo imechafuka baada ya watu zaidi ya saba kuuwawa katika muda mfupi usiozidi mwezi mmoja! Vyanzo vya vifo hivyo bado havijawa wazi mpaka saizi! Mwanzo wa matukio ulianza hivi;
Mpaka sasa bado haijaeleweka nini chanzo cha mauaji hayo, maana awali kwa yule kijana wa karibu na Blue Park pamoja, Mwl wa shule ya msingi na hao vijana wawili ilidhaniwa labda ni biashara/ dili ambazo walidhulumiana! Lakini hili tukio la usiku wa kuamkia leo linazidi kuongeza mkanganyiko wa chanzo.
- Katikati ya mwezi wa tisa jamaa mmoja alipigwa risasi karibu kabisa na guest moja maarufu kama Blue Park. Ukiwa unaelekea guest hiyo ya Blue Park kuna kajiduka ka huyo marehemu ambapo alipigwa shaba na kufa hapo hapo! Kabla ya kumuua marehemu huyo, kulikuwa na mtu mwingine ambaye alikuwa na marehemu lakini yeye hao jamaa hawakumdhuru wala kuiba kitu chochote kile. Tukio hili lilitokea Loliondo mjini.
- Kabla ya tukio hilo halijakaa sawa, akapigwa tena shaba mwl wa Shule ya Msingi ambaye yeye alinusurika kifo baada ya kukikimbizwa hospitali ya Wasso kwa matibabu. Katika tukio hilo, mwalimu huyo alipigwa shaba maeneo ya tumboni ambapo risasi hiyo ilimjeruhi (kuparaza) na mguuni. Tukio hili lilitokea Wasso nje kidogo ya mji wa Loliondo kama 9Kms hivi, hali kadhalika matuhumiwa hao hawakuchukua kitu chochote na kutokomea kusikojulikana.
- Watu wakiwa wanajiuliza kunani, usiku wa tarehe 10.10.2011 vijana wawili tena walipigwa shaba na kufa hapo hapo! Tukio hili limetokea mji wa Waso.
- Usiku wa kuamkia leo ndiyo umeshuhudia mauaji ya kutisha baada ya watu watano kuuawa kwa kupigwa risasi na wengine kunjinjwa na kuacha majeruhi kadhaa ambao wapo hospitali ya Wasso wakiendelea na matibabu. Juhudi za kuwahoji majeruhi ziligonga mwamba baada ya kila walipohojiwa kushindwa kueleza chochote zaidi ya kulia tu, inatia huruma sana jamani!
Kutokana na hali jinsi ilivyo, watu saizi katika mji wa Wasso na Loliondo imejaa mashaka sana, yaani hofu tupu ya kuogopa kuuwawa!
Pamoja na hayo, vyombo vya ulinzi na usalama bado havijatoa tamko rasmi licha ya jitahada kubwa zinazoendelea za kutafuta wahusika wa matukio hayo yote.
Nawakalisha kwa masikitiko makubwa.
Nitazidi kuwajuza kwa kadri chanzo kitavyokuwa kinanyetisha toka Loliondo.
Kwa suala la babu na kikombe chake kwa kweli sijui imeishia wapi, ni imani yangu wagonjwa bado ni wengi lakini hali si kivile kama hapo awali.Babu si mtume wa Loliondo hawezi kuwaombea mji ukatulia? au na yeye kamba zake zimeisha
Huwa sipendi kusema uongo FF ukitaka niPM nitakujuza mwarabu anachokuja kukifanya Loliondo lakini si uwindani kama inavyofahamika.
Mwarabu wa Loliondo hana shida ya pesa, yeye ile ni sehemu yake ya kupumzikia tu. Ukifika muda wa kuja huku anakuja yupo full equipped basi ni kula raha kwa kwenda mbele.
Hebu tujuze nasi tujue kama sio uwindaji ni nini? au kunauchimbaji pia nini?
Mwarabu wa Loliondo hana shida ya pesa, yeye ile ni sehemu yake ya kupumzikia tu. Ukifika muda wa kuja huku anakuja yupo full equipped basi ni kula raha kwa kwenda mbele.
..Hivi huko si ndiko kuna wakati walikuwa wanatawaliwa na wasomali kutoka Kenya na polisi walishindwa kupambana na hao wasomali hadi JWTZ wakapelekwa ndio kukawa na amani? Yaelekea watu wa huko kulipuana shaba ndio zao...Polisi bado wanaendelea na uchunguzi, na siyo polisi bali kamati nzima ya ulinzi na usalama inahaha kutafuta chanzo sahihi cha mauaji hayo na kikubwa zaidi ni kuwakikishia raia kuwa hali imerejea kama awali.
Ndiyo hivyo ndugu yangu watu tunafikiria waarabu pekee ndiyo wanaweza kutenganisha vichwa na viwili wili kumbe hata bongo tumefikia huko!
UPDATES:
Taarifa zisizo na mashaka zinasema chanzo cha ugomvi ulipelekea mauaji ni MGOGORO WA ARDHI BAINA YA WASONJO NA WAMASAI. Wamasai wa kijiji cha Magaiduru waliwaua vijana wawili wa kisonjo kwa kutumia bunduki aina ya SMG. Wasonjo nao wa kijiji cha Mgongo Mageri walikwenda kulipiza kisasi cha kuuwawa ndugu zao. Vijiji hivi vya Magaiduru na Mgongo Mageri ni vijiji vilivyo karibu. Katika zoezi hilo la kulipa kisasi watu watano waliuawa ambao ni vibarua wawili (Wairaq), Mgeni mmoja (Mmasai), Mama mmoja na mtoto mmoja ambao wote ni wakazi wa kijiji cha Magaiduru. Zoezi la kusuluhisha mgogoro huo wa ardhi linaendelea kwa viongozi wa serikali toka Arusha kuelekea Loliondo na wale waliopo Loliondo lakini suluhu bado haijapatika.
Kuhusu wapi wanapozipata hizo silaha, taarifa zinaweka wazi kuwa silaha zinanunuliwa toka Kenya. Kutoka Loliondo hadi mpakani na Kenya haizidi 100kms na barabara ipo ambayo inapitika bila shida karibu kipindi chote cha mwaka.
Kwa wale yule kijana niliyesema ameuwa karibu na Blue Park guest vyanzo vinatema kuwa ni mambo ya kibiashara ambapo inaonekana walidhulumiana
WanaJF,
Poleni na shughuli za ujenzi wa Taifa letu.
Habari ambazo nimezipata sasa hivi kutoka Loliondo kuwa hali ya mji huo imechafuka baada ya watu zaidi ya saba kuuwawa katika muda mfupi usiozidi mwezi mmoja! Vyanzo vya vifo hivyo bado havijawa wazi mpaka saizi! Mwanzo wa matukio ulianza hivi;
Mpaka sasa bado haijaeleweka nini chanzo cha mauaji hayo, maana awali kwa yule kijana wa karibu na Blue Park pamoja, Mwl wa shule ya msingi na hao vijana wawili ilidhaniwa labda ni biashara/ dili ambazo walidhulumiana! Lakini hili tukio la usiku wa kuamkia leo linazidi kuongeza mkanganyiko wa chanzo.
- Katikati ya mwezi wa tisa jamaa mmoja alipigwa risasi karibu kabisa na guest moja maarufu kama Blue Park. Ukiwa unaelekea guest hiyo ya Blue Park kuna kajiduka ka huyo marehemu ambapo alipigwa shaba na kufa hapo hapo! Kabla ya kumuua marehemu huyo, kulikuwa na mtu mwingine ambaye alikuwa na marehemu lakini yeye hao jamaa hawakumdhuru wala kuiba kitu chochote kile. Tukio hili lilitokea Loliondo mjini.
- Kabla ya tukio hilo halijakaa sawa, akapigwa tena shaba mwl wa Shule ya Msingi ambaye yeye alinusurika kifo baada ya kukikimbizwa hospitali ya Wasso kwa matibabu. Katika tukio hilo, mwalimu huyo alipigwa shaba maeneo ya tumboni ambapo risasi hiyo ilimjeruhi (kuparaza) na mguuni. Tukio hili lilitokea Wasso nje kidogo ya mji wa Loliondo kama 9Kms hivi, hali kadhalika matuhumiwa hao hawakuchukua kitu chochote na kutokomea kusikojulikana.
- Watu wakiwa wanajiuliza kunani, usiku wa tarehe 10.10.2011 vijana wawili tena walipigwa shaba na kufa hapo hapo! Tukio hili limetokea mji wa Waso.
- Usiku wa kuamkia leo ndiyo umeshuhudia mauaji ya kutisha baada ya watu watano kuuawa kwa kupigwa risasi na wengine kunjinjwa na kuacha majeruhi kadhaa ambao wapo hospitali ya Wasso wakiendelea na matibabu. Juhudi za kuwahoji majeruhi ziligonga mwamba baada ya kila walipohojiwa kushindwa kueleza chochote zaidi ya kulia tu, inatia huruma sana jamani!
Kutokana na hali jinsi ilivyo, watu saizi katika mji wa Wasso na Loliondo imejaa mashaka sana, yaani hofu tupu ya kuogopa kuuwawa!
Pamoja na hayo, vyombo vya ulinzi na usalama bado havijatoa tamko rasmi licha ya jitahada kubwa zinazoendelea za kutafuta wahusika wa matukio hayo yote.
Nawakalisha kwa masikitiko makubwa.
Nitazidi kuwajuza kwa kadri chanzo kitavyokuwa kinanyetisha toka Loliondo.
Chanzo hakikufanikiwa kupata picha, samahani kwa hilo.Mzee kuna picha yoyote kutoka huko Loliondo kuhusiana na mauaji haya mfululizo????????????????