Loliondo kwachafuka, watu wauana na kuchinjana kama kuku! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Loliondo kwachafuka, watu wauana na kuchinjana kama kuku!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mzee wa Rula, Oct 12, 2011.

 1. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #1
  Oct 12, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  UPDATES:
  Taarifa zisizo na mashaka zinasema chanzo cha ugomvi ulipelekea mauaji ni MGOGORO WA ARDHI BAINA YA WASONJO NA WAMASAI. Wamasai wa kijiji cha Magaiduru waliwaua vijana wawili wa kisonjo kwa kutumia bunduki aina ya SMG. Wasonjo nao wa kijiji cha Mgongo Mageri walikwenda kulipiza kisasi cha kuuwawa ndugu zao. Vijiji hivi vya Magaiduru na Mgongo Mageri ni vijiji vilivyo karibu. Katika zoezi hilo la kulipa kisasi watu watano waliuawa ambao ni vibarua wawili (Wairaq), Mgeni mmoja (Mmasai), Mama mmoja na mtoto mmoja ambao wote ni wakazi wa kijiji cha Magaiduru. Zoezi la kusuluhisha mgogoro huo wa ardhi linaendelea kwa viongozi wa serikali toka Arusha kuelekea Loliondo na wale waliopo Loliondo lakini suluhu bado haijapatika.
  Kuhusu wapi wanapozipata hizo silaha, taarifa zinaweka wazi kuwa silaha zinanunuliwa toka Kenya. Kutoka Loliondo hadi mpakani na Kenya haizidi 100kms na barabara ipo ambayo inapitika bila shida karibu kipindi chote cha mwaka.

  Kwa wale yule kijana niliyesema ameuwa karibu na Blue Park guest vyanzo vinatema kuwa ni mambo ya kibiashara ambapo inaonekana walidhulumiana


  WanaJF,
  Poleni na shughuli za ujenzi wa Taifa letu.
  Habari ambazo nimezipata sasa hivi kutoka Loliondo kuwa hali ya mji huo imechafuka baada ya watu zaidi ya saba kuuwawa katika muda mfupi usiozidi mwezi mmoja! Vyanzo vya vifo hivyo bado havijawa wazi mpaka saizi! Mwanzo wa matukio ulianza hivi;

  • Katikati ya mwezi wa tisa jamaa mmoja alipigwa risasi karibu kabisa na guest moja maarufu kama Blue Park. Ukiwa unaelekea guest hiyo ya Blue Park kuna kajiduka ka huyo marehemu ambapo alipigwa shaba na kufa hapo hapo! Kabla ya kumuua marehemu huyo, kulikuwa na mtu mwingine ambaye alikuwa na marehemu lakini yeye hao jamaa hawakumdhuru wala kuiba kitu chochote kile. Tukio hili lilitokea Loliondo mjini.
  • Kabla ya tukio hilo halijakaa sawa, akapigwa tena shaba mwl wa Shule ya Msingi ambaye yeye alinusurika kifo baada ya kukikimbizwa hospitali ya Wasso kwa matibabu. Katika tukio hilo, mwalimu huyo alipigwa shaba maeneo ya tumboni ambapo risasi hiyo ilimjeruhi (kuparaza) na mguuni. Tukio hili lilitokea Wasso nje kidogo ya mji wa Loliondo kama 9Kms hivi, hali kadhalika matuhumiwa hao hawakuchukua kitu chochote na kutokomea kusikojulikana.
  • Watu wakiwa wanajiuliza kunani, usiku wa tarehe 10.10.2011 vijana wawili tena walipigwa shaba na kufa hapo hapo! Tukio hili limetokea mji wa Waso.
  • Usiku wa kuamkia leo ndiyo umeshuhudia mauaji ya kutisha baada ya watu watano kuuawa kwa kupigwa risasi na wengine kunjinjwa na kuacha majeruhi kadhaa ambao wapo hospitali ya Wasso wakiendelea na matibabu. Juhudi za kuwahoji majeruhi ziligonga mwamba baada ya kila walipohojiwa kushindwa kueleza chochote zaidi ya kulia tu, inatia huruma sana jamani!
  Mpaka sasa bado haijaeleweka nini chanzo cha mauaji hayo, maana awali kwa yule kijana wa karibu na Blue Park pamoja, Mwl wa shule ya msingi na hao vijana wawili ilidhaniwa labda ni biashara/ dili ambazo walidhulumiana! Lakini hili tukio la usiku wa kuamkia leo linazidi kuongeza mkanganyiko wa chanzo.
  Kutokana na hali jinsi ilivyo, watu saizi katika mji wa Wasso na Loliondo imejaa mashaka sana, yaani hofu tupu ya kuogopa kuuwawa!
  Pamoja na hayo, vyombo vya ulinzi na usalama bado havijatoa tamko rasmi licha ya jitahada kubwa zinazoendelea za kutafuta wahusika wa matukio hayo yote.
  Nawakalisha kwa masikitiko makubwa.

  Nitazidi kuwajuza kwa kadri chanzo kitavyokuwa kinanyetisha toka Loliondo.
   
 2. m

  mzee wandimu JF-Expert Member

  #2
  Oct 12, 2011
  Joined: Sep 23, 2011
  Messages: 441
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  nilizani inamhusu yule babu wa kikombe!

  poleni sana mkuu mzee wa rula!
  vipi uchunguzi wa polisi unasemaje?
   
 3. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #3
  Oct 12, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,987
  Likes Received: 691
  Trophy Points: 280
  Walisema watamfanya mbaya babu wa loliondo, labda wameamua kufyeka watu .... Hawana uhusiano na babu hao watu waliouwawa?
   
 4. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #4
  Oct 12, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Hawana uhusiano na babu wa Loliondo, babu anaishi 68Kms kutoka Loliondo mji unaoitwa Samunge na matukio haya yote yametokea mjini Loliondo na Wasso. Inawezekana ikawa ni visasi vya kikabila na kudhulumiana lakini bado hiajawa confirmed.
   
 5. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #5
  Oct 12, 2011
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,367
  Likes Received: 7,008
  Trophy Points: 280
  Duh ni habari ya kusikitisha kwa kweli,
   
 6. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #6
  Oct 12, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Polisi bado wanaendelea na uchunguzi, na siyo polisi bali kamati nzima ya ulinzi na usalama inahaha kutafuta chanzo sahihi cha mauaji hayo na kikubwa zaidi ni kuwakikishia raia kuwa hali imerejea kama awali.
   
 7. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #7
  Oct 12, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
  NDIO BONGO tulikofikia sasa baada ya 50 years of ignorance..
   
 8. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #8
  Oct 12, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Ndiyo hivyo ndugu yangu watu tunafikiria waarabu pekee ndiyo wanaweza kutenganisha vichwa na viwili wili kumbe hata bongo tumefikia huko!
   
 9. SnowBall

  SnowBall JF-Expert Member

  #9
  Oct 12, 2011
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 3,067
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Duh poleni sana!!
   
 10. BABU CHONDO

  BABU CHONDO JF-Expert Member

  #10
  Oct 12, 2011
  Joined: Jun 6, 2011
  Messages: 859
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Hao waarabu wamenza kuunda kajeshi
  Poleni sana inauma kwakweli.
   
 11. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #11
  Oct 12, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Asante mkuu, ila hali ndiyo hiyo.
   
 12. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #12
  Oct 12, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Sidhani kama Mwarabu anahusika, yeye Loliondo kaichukulia kama sehemu ya kuficha uovu kulingana na maadili ya dini yake. Hana shida kimsingi.
   
 13. Puppy

  Puppy JF-Expert Member

  #13
  Oct 12, 2011
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 2,280
  Likes Received: 667
  Trophy Points: 280
  Geografia ya Panapotokea Matukia Na Kwa Babu Ni Mbali Sana. Huko Ni Waso Na Kwa Babu ni samunge. Waso Ndio Wako Wale jamaa wenye haki ya miaka 100 wanaojibebea wanyama, ni mji mdogo...

  Jamaa wangeletwa mjini kutibiwa au wangepelekwa mahali inigine salama.. Kama wauaji wako hapo hapo si watawamalizia tu kirahisi?

  Roho zao zipumzike kwa amani
   
 14. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #14
  Oct 12, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Duhh poleni
  Au hao jamaa wanajifunza kulenga shabaha?
   
 15. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #15
  Oct 12, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Wasso kuna hospitali nzuri kiasi, lakini umbali wa kutoka Loliondo - Arusha ni 420kms kati ya hizo toa 177kms (Arusha - Ngorongoro getini) ambazo ndizo zina lami. Unaweza kuona hali kwa jinsi ilivyo,
   
 16. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #16
  Oct 12, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Hata kama hawajifunzi kulenga shabaha lakini umbali wa mita kama 5-10 utashindwa kulenga mkuu? Halafu bunduki inayosadikiwa kutumika ni aidha SMG au SAR ambayo ni kubwa na ina shabaha ya kutosha tofauti na bastola.
   
 17. Puppy

  Puppy JF-Expert Member

  #17
  Oct 12, 2011
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 2,280
  Likes Received: 667
  Trophy Points: 280
  Sure thing mzee wa rula, lakini kwa zile 4x4 za wanyamapori ingesaidia kufika somewhere.... Uoga wangu sio uwezo wa hospital bali ni usalama wao kama wauaji bado wapo
   
 18. Biohazard

  Biohazard JF-Expert Member

  #18
  Oct 12, 2011
  Joined: Aug 21, 2011
  Messages: 2,002
  Likes Received: 287
  Trophy Points: 180
  EEEhhh Mungu naomba uturehemu
   
 19. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #19
  Oct 12, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Nakubaliana nawe lakini hiyo ni temporarily solution, dawa ni kuwapata hao jamaa ambao saizi wanasakwa kwa udi na uvumba. Jioni nitakujuza zaidi juhudi zimefikia wapi kuwapata hao wahusika maana tukio hilo limeifedhehesha serikali na wananchi kwa ujumla hivyo ni imani yangu wananchi wakishirikiana na vyombo vya dola watafikia mahali pazuri.
   
 20. BORNCV

  BORNCV JF-Expert Member

  #20
  Oct 12, 2011
  Joined: Oct 11, 2011
  Messages: 243
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Duh! Kunani tena huko?
  Pole yao sana.
   
Loading...