Loliondo itaangamiza watanzania

emrema

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
268
42
Wana jf, nilikua nyumbani kwa siku 5 zilizopita kwa pasaka. Nilijumuika na ndugu na rafiki zangu kuanzia Jumamosi hadi jumatatu. Haya ndio nilioyaona.Jamaa zangu wa karibu ni ma dealers wa madini ya Tanzanite hivyo mkwanja sio haba. siku za nyuma walikua wanajihisi hisi na kaugonjwa haka kakali basi miezi 2 iliyopita walikuwa wa kwanza kwanza kutinga Samunge na kupata ki cup. Nakikubali kikombe sababu wazazi wangu wamepona moyo na miguu.

Jumamosi tukawa club AQ tulikuwa 6 hivi basi staili ya kuchukua totoz ni 'aah mi nimeshapata kikombe bwana so anti usijali sina ngoma, demu nae aah hata mimi nimetoka wiki iliyopita kwa hiyo niko safi' Wakaanza kusimuliana ya Loliondo .muda ukafika wakaondoka jamaa zangu 3 kwa staili hiyo na kilevi tena. nadhani wote hawakutumia tena kale kakinga ketu. mi mgeni nikalala doro.

Jumapili tukawa pale Triple A mambo kama ya jana yake ila mademu wengine kabisa. Mh kengele zikavuma kichwani kwangu. nikajua ndio kawaida ya baadhi ya vijana wa A town.

wajameni kikombe hakitolewi mara 2 na haina maana kurudia maisha yale ya nyuma. Baada ya kikombe TUBADILIKE. Bado sijaenda kwa kikombe ila siku ikifika ntaaga wanajf.
 
duh kikombeeeeeeeeee!!hadi kufika mwezi june cd4 zitabakia wastani wa 4-10!!
 
Wazungu hapa Ulaya wameshapata taarifa ya kikombe na wooote wanakuja, andae usafiri na vyumba vya wageni Arusha.
 
Emrema,ni kweli kuna watu kikombe kimewasaidia,ila kuna wengine kimewaletea u mauti ndani ya siku saba toka wakinywe,si vizuri kutaja majina ya marehemu kwenye jf,vinginevyo ningewataja.
 
Kikombe si mchezo mama mwenye nyumba nnakokaa alikuwa ame paralyze for 5 yrs hakuweza kunyanyuka alikuwa analala chali kitandani tuu, nilipoenda kulipa kodi mwaka jana alikuwa hata kuongea shida, alikuwa pia na kisukari mwili ulikuwa umeisha alikuwa mweusi saana kwa kweli ilinisikitisha saana, lkn LEO hii nasema LEo hii nimeenda kwakwe nimemkuta amekaa kwenye kiti, amenenepa amekuwa mweupe anazungumza vizuri akaniambia mwanangu mwaka wa tano huu nilikuwa nalala tu toka atoke kwa babu anawezaa kukaa, anaongea vizuri anaweza kusimama kwa kujishikia ukutani mkono wa kushoto unafanya kazi vizuri ila mguu wa kulia na mkono wa kulia bado, mwenyewe anafanya mazoezi kila siku anasema mpaka disemba atarudi kazini hiyo ni kazi ya KIKOmbe
 
kweli ee??!
 
Watu wangu wamekuwa kondoo waliopotea, wachungaji wao wamewapoteza; wamewapotosha milimani; wamekwenda toka mlima hata kilima, wamesahau mahali pao pa kupumzika.
Yeremia 50:6
 
emrema, nakushangaa!! Unaisifia tiba ya babu!! We ni; (a)Mkristo, (b)mkristu, (c)mpagani.? Au! Unaufaham uponyaji wa Mungu aliye hai? Siyo Mungu wa Ambilikile! Wa Yesu. Uponyaji wa Yesu lazima kwanza Injili waamini kisha wapone, Marko16:16-20. Hao watu unaowasema lazima waangamie tu na wengine wote waliopata hicho kicup. Haijalish ni kiongozi gani wa dini unaye muamini kuwa alipata kcup! Uponyaji wa Mungu aliye hai lazima uambatane na ondoleo la dhambi. Marko2:5 Zabur103:3. Sasa hao walihubiriwa injili wakatubu dhambi na kuziacha? Nipe na nyie majibu yenu. Weka maandiko, ili kwa mashahidi wawili au watatu neno na lithibitike. Ni hayo mkuu.
 
Pamoja na hayo soma 2Waflme1:1-4
 
Sijakisifia kikombe ila nimeonyesha vile waliopata wanavyojiamini nakutenda uovu uleule uliowafanya waishi kwa mashaka. Hasa ngono zembe na wengine kutumia vyakula vilivyowadhuru. Wazazi wangu wamepona so lazima niamini kuwa kinatibu. ila baada ya kukinywa TUBADILIKE. Kama huamini tulia wanaokiamini wanywe..... na wawe weupeeee!
 
emrema, nakushangaa!! Unaisifia tiba ya babu!! We ni; (a)Mkristo, (b)mkristu, (c)mpagani.? Au! Unaufaham uponyaji wa Mungu aliye hai? Siyo Mungu wa Ambilikile! Wa Yesu. Uponyaji wa Yesu lazima kwanza Injili waamini kisha wapone, Marko16:16-20. Hao watu unaowasema lazima waangamie tu na wengine wote waliopata hicho kicup. Haijalish ni kiongozi gani wa dini unaye muamini kuwa alipata kcup! Uponyaji wa Mungu aliye hai lazima uambatane na ondoleo la dhambi. Marko2:5 Zabur103:3. Sasa hao walihubiriwa injili wakatubu dhambi na kuziacha? Nipe na nyie majibu yenu. Weka maandiko, ili kwa mashahidi wawili au watatu neno na lithibitike. Ni hayo mkuu.

Χριστὸς, {Christós} Kigiriki = Kristo
Christus = kilatini = Kristu

So, usipotoshe.
 
Back
Top Bottom