Taratibu kaka. Mbona unawaogopa sana hao tigo ambao hawatulindi kwa lolote?
Hauwezi kui trace kwa vile simu inasema "Locating your iPhone on a map is disabled. Turn on Location Services to enable it." Na hiyo setting haibadilishiki bila kuwa na code, ambayo sina. Sasa watai trace vipi hiyo simu? Na hata kama ingekuwa iko turned on hiyo feature, bado huwezi kui trace kama haijaingia on line. Hiyo iCloud lock ina e-mail address, nimemtumia e-mail kumwambia kuna simu yako hapa, mtu hajibu, jina lenyewe la kijapani sijui kichina, sasa nifanyeje hapa? Najaribu kutafuta solution ya tatizo, simu ndo nishanunua, panicking haitasaidia.
Motherboard ndio engine ya simu, wazo la kubadilisha motherboard ni sawa na kubadilisha engine kwenye gari, utasemaje ni sawa na kubadilisha site mirror? Mzee hebu tulia kidogo kabla huja post unachofikiria ku post. Hapa ni sawa na kuagiza gari ukakuta engine kaput, kufikiria kufunga engine mpya iweje ni wazo baya?
Wengi hapa tumewahi kuagiza magari kwa kutuma mamilioni oversees kwa watu ambao hatuwajui, na magari yakafika, na wengine bahati mbaya wamelizwa. Maishani ni lazima uchukue a leap of faith sometimes. Unachukua risk na tahadhari lakini sometime una boogie step. Kupoteza laki nne tano siwezi kukaa nalia au najilaumu, mwanamme unaamka, unatulia, unaangalia kama kuna tatuzi na unauliza wanaume wenzako vile vile. Kama hakuna unaendelea na maisha, naweza kuuza hii simu kwa spare, LCD yake na housing bei zaidi ya nusu hasara yangu, sasa nusu hasara itaniua? Nini cha ku panick hapa?