Live updates: Uzinduzi rasmi wa ACT-wazalendo - Diamond Jubilee Hall

Mkuu mda mwingine huwa nafikiria ikitokea slaa akawa Rais lazima tuliingize kwenye matukio ya dunia ,,rais wa kwanza mwenye girlfriend kwa mda mrefu duniani.

Hahahaaa,hilo neno 'girlfriend' hua linanichekesha sana.Ni bora mchumba kidogo.
 

Viongozi wa act wanaupeo mdogo sana wa kufikiri
 
Kitila Mkumbo, Zitto Sasa tunachukua jimbo la kawe kwanza karibuni Kawe mimi niko tayari kutoa office ya Wilaya..ni PM
 
Leo kulikuwa na uzinduzi wa chama kipya cha zito kabwe diamond jb lakini cha kushangaza badala viongozi wa chama kutangaza sera za chama chao wanacheza ngoma na kuonyesha maigizo
 
Chama cha ACT-Wazalendo kimefanya uchaguzi wake pamoja na uzinduzi kama ambavyo ilikuwa ikitangazwa kwa muda mrefu sana. Pamoja na ulaghai juu ya wageni waalikwa kwenye uzinduzi wao, ila ukweli ni kuwa uzinduzi umefanyika. Kama mnavyojua, chama kilikuwa kikitangaza kuwa Prof. Lipumba, mtoto wa Nkhuruma na viongozi kadhaa wa Ghana, viongozi wa vyama kadhaa vya siasa vya ujerumani, nk. Pamoja na kick hiyo, hakuna hata kiongozi mmoja kwenye orodha iliyokuwa inasemwa ambaye amehudhuria. Mbaya zaidi hata Prof. Lipumba ambaye yupo mjini DSM amesusia. Hata hivyo hii sio hoja yangu kwasasa, nilikuwa najaribu kuonyesha ambavyo ulaghai au kukosa umakini kumeonekana hapa. Hoja yangu inakwenda moja kwa moja kwenye marekebisho ya katiba ya chama hiki ambapo sasa kutakuwa na Kiongozi mkuu kama mkuu wa taasisi, tofauti na ilivyozoeleka kwenye vyama vingi duniani. Gazeti la jana, kwenye moja ya habari zake ilisema, ACT WAMWANDALIA ZITTO NAFASI YA UONGOZI. Katika maelezo ya mwandishi, inaonekana kuwa mabadiliko ya katiba yalifanyika makusudi ili ndugu Zitto apate nafasi hiyo.

Hebu twende kwenye marekebisho hayo, ambayo yanataja sifa za kiongozi mkuu kama ifuatavyo:

1. Kiongozi Mkuu wa chama kwenye mikutano mikuu ya chama Taifa, mkutano mkuu, Halmashauri Kuu na Kamati Kuu
2. Mkuu wa siasa, mshauri na mwelekezaji kwa viongozi wote (Akiwemo Mwenyekiti) na maafisa wa ACT-Tanzania.
3. Kuteua wajumbe watano wa Kamati Kuu kwa mujibu wa Katiba hii
4. Mtoa tamko (Katibu Mwenezi) rasmi kuhusu masuala ya sera na mtazamo wa chama
5. Mtoa habari mahususi kwenye mkutano mkuu, Halmashauri Kuu na Kamati Kuu kuhusu hali ya kisiasa nchini na masuala mengine ya kitaifa na kimataifa.
6. Msimamzi wa Mafunzo na Mtoa maelekezo kuhusu shughuli zote za ACT-Tanzania
7. Ndiye Kiongozi Mkuu wa Chama.
8. Ni NURU na TASWIRA ya ACT-Tanzania

Ukitazama sifa na kazi za kiongozi mkuu, hakika ni CEO wa chama. Maana mwenyekiti hana nguvu yoyote juu ya kiongozi mkuu. Nibandika andiko moja siku chache zilizopita na kusema...ACT-Tanzania inarudia makosa ya vyama vya upinzani, kwa kujenga taasisi juu ya watu badala ya falsafa. Kilichotokea hapa, ni kujenga taasisi kwa CEO Zitto Kabwe. Kibaya zaidi, mkakati ulijengwa ili apatikane mwenyekiti dhaifu, ambaye atapelekwa kama roboti na huyu CEO ndugu Zitto Kabwe.

Kwa maono yangu, kwasasa Zitto Kabwe hana tofauti na Reginald Mengi, Mmiliki na Mkurugenzi mtendaji wa IPP au Bakhresa ambaye ni Mmiliki na Mkurugenzi mtendaji wa Bakhresa Group of Companies. Ndio Zitto Kabwe sasa ni CEO.

Nawasilisha!!!!
 
Leo kulikuwa na uzinduzi wa chama kipya cha zito kabwe diamond jb lakini cha kushangaza badala viongozi wa chama kutangaza sera za chama chao wanacheza ngoma na kuonyesha maigizo

Hii ni thread ya 10000 kwa leo tu kuhusu Zitto. Mtaweweseka sana.
 
Naona kuwatoa mafisadi hakupo tena!!! mmeungana na TLP enzi hizo ..ACT kuwatoa watanzania haiwezekani!! haitatokea ila tuungane kwa pamoja pasipo chuki tuwangoe MAGAMBA.
 
Niliwambia Bavicha mnywe maji mengi na chakula cha kutosha ona sasa mnazidiwa na dozi...Hakika Saccos ina sambaratika...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…