Live updates: Uzinduzi rasmi wa ACT-wazalendo - Diamond Jubilee Hall

Mkuu mda mwingine huwa nafikiria ikitokea slaa akawa Rais lazima tuliingize kwenye matukio ya dunia ,,rais wa kwanza mwenye girlfriend kwa mda mrefu duniani.

Hahahaaa,hilo neno 'girlfriend' hua linanichekesha sana.Ni bora mchumba kidogo.
 
Leo ni tukio la kihstoria hapa nchini ambapo Chama cha ACT-WAZALENDO kinazinduliwa rasmi,, tafadhari fuatilia uzi huu kwa live updates.
Updates..sijakimbia wazalendo.nilikabwa na majukum hapa ukumbini..no mafuriko...nyomi..with kibaoo..viongozi wakitaifa wameshawasili hivi sasa in utambulisho.

Updates 2.
Mshereheshaji anaeleza masuala kadhaa muhimu ktk chama ikiwa ni pamoja na uchaguzi ndani ya chama.uzinduzi Wa chama na uenezi wake.
Muongoza ratiba anaelezea milima na mabonde ndani ya chama tangu kimeanzishwa na jinsi uchaguzi ulivyofanikiwa hadi Jana ambapo chama kimehitimisha kwa kufanya uchaguzi wa kitaifa...
Updates..mdada machachari ktk kuimba anatoa burudani Kali hapa ukumbini

Sasa in utambulisho Wa viongozi waliochaguliwa Jana....ametambulishwa mwenyekiti Anna mughwira ..KATIBU MKUU Samson MWIGAMBA..makam bara na visiwani
Makan mwenyekiti bara SHABANI mambo ameeleza hivi sasa kwamba act ni ya watz wazalendo na ameomba wananchi wrote tuiunge mkono

Updates...mwenyekiti TAIFA Anna mughwira anahutubia hivi salsa .anasema act ni ya watz na ni chama kinachoweka maslahi ya TAIFA kwanza...kwamba act imetanguliza utu kwanza.

Updates...
Mwenyekiti anasrma act ni chama taasisi..in chama kinachojali maslahi ya TAIFA na kimebainisha ktk ilani kwamba kinawaenzi waasisi Wa TAIFA Mwl julius k.NYERERE na abeid karume..

Updates...anasema act imeandika historia katika TAIFA kwa kumchagua mwenyekiti Wa kwanza mwanamke...act imeanzia nyumbani hivyo tukiunge mkono
Updates...
Afande Sele ndani ya nyumba anatumbuiza
Zitti KABWE anahutuvia sasa anasema ni miaka 54 sasa tangu tupate Uhuru ndoto za waasisi w TAIFA hili hazijafikiwa badala Yake ni jinamizi la ufukara limelikumba taifa
Anasema act unaenda kurudisha misingi ya mwalim NYERERE

Act inataka kurejesha siasa za kizalendo na nchi irudi kwa wananchi.kuondoa mamlaka ya siasa kw wafanyabiashara kurudi kwa wananchi...
Viongozi Wa act kuweka hadharani Mali zao na kutangaza Mali na madeni Yake.
...updates...viongozi Wa chama TAIFA wanatia saini mikataba ya Ku surrender mali zao hadharani...

Viongozi wa act wanaupeo mdogo sana wa kufikiri
 
Kitila Mkumbo, Zitto Sasa tunachukua jimbo la kawe kwanza karibuni Kawe mimi niko tayari kutoa office ya Wilaya..ni PM
 
Leo kulikuwa na uzinduzi wa chama kipya cha zito kabwe diamond jb lakini cha kushangaza badala viongozi wa chama kutangaza sera za chama chao wanacheza ngoma na kuonyesha maigizo
 
Chama cha ACT-Wazalendo kimefanya uchaguzi wake pamoja na uzinduzi kama ambavyo ilikuwa ikitangazwa kwa muda mrefu sana. Pamoja na ulaghai juu ya wageni waalikwa kwenye uzinduzi wao, ila ukweli ni kuwa uzinduzi umefanyika. Kama mnavyojua, chama kilikuwa kikitangaza kuwa Prof. Lipumba, mtoto wa Nkhuruma na viongozi kadhaa wa Ghana, viongozi wa vyama kadhaa vya siasa vya ujerumani, nk. Pamoja na kick hiyo, hakuna hata kiongozi mmoja kwenye orodha iliyokuwa inasemwa ambaye amehudhuria. Mbaya zaidi hata Prof. Lipumba ambaye yupo mjini DSM amesusia. Hata hivyo hii sio hoja yangu kwasasa, nilikuwa najaribu kuonyesha ambavyo ulaghai au kukosa umakini kumeonekana hapa. Hoja yangu inakwenda moja kwa moja kwenye marekebisho ya katiba ya chama hiki ambapo sasa kutakuwa na Kiongozi mkuu kama mkuu wa taasisi, tofauti na ilivyozoeleka kwenye vyama vingi duniani. Gazeti la jana, kwenye moja ya habari zake ilisema, ACT WAMWANDALIA ZITTO NAFASI YA UONGOZI. Katika maelezo ya mwandishi, inaonekana kuwa mabadiliko ya katiba yalifanyika makusudi ili ndugu Zitto apate nafasi hiyo.

Hebu twende kwenye marekebisho hayo, ambayo yanataja sifa za kiongozi mkuu kama ifuatavyo:

1. Kiongozi Mkuu wa chama kwenye mikutano mikuu ya chama Taifa, mkutano mkuu, Halmashauri Kuu na Kamati Kuu
2. Mkuu wa siasa, mshauri na mwelekezaji kwa viongozi wote (Akiwemo Mwenyekiti) na maafisa wa ACT-Tanzania.
3. Kuteua wajumbe watano wa Kamati Kuu kwa mujibu wa Katiba hii
4. Mtoa tamko (Katibu Mwenezi) rasmi kuhusu masuala ya sera na mtazamo wa chama
5. Mtoa habari mahususi kwenye mkutano mkuu, Halmashauri Kuu na Kamati Kuu kuhusu hali ya kisiasa nchini na masuala mengine ya kitaifa na kimataifa.
6. Msimamzi wa Mafunzo na Mtoa maelekezo kuhusu shughuli zote za ACT-Tanzania
7. Ndiye Kiongozi Mkuu wa Chama.
8. Ni NURU na TASWIRA ya ACT-Tanzania

Ukitazama sifa na kazi za kiongozi mkuu, hakika ni CEO wa chama. Maana mwenyekiti hana nguvu yoyote juu ya kiongozi mkuu. Nibandika andiko moja siku chache zilizopita na kusema...ACT-Tanzania inarudia makosa ya vyama vya upinzani, kwa kujenga taasisi juu ya watu badala ya falsafa. Kilichotokea hapa, ni kujenga taasisi kwa CEO Zitto Kabwe. Kibaya zaidi, mkakati ulijengwa ili apatikane mwenyekiti dhaifu, ambaye atapelekwa kama roboti na huyu CEO ndugu Zitto Kabwe.

Kwa maono yangu, kwasasa Zitto Kabwe hana tofauti na Reginald Mengi, Mmiliki na Mkurugenzi mtendaji wa IPP au Bakhresa ambaye ni Mmiliki na Mkurugenzi mtendaji wa Bakhresa Group of Companies. Ndio Zitto Kabwe sasa ni CEO.

Nawasilisha!!!!
 
Leo kulikuwa na uzinduzi wa chama kipya cha zito kabwe diamond jb lakini cha kushangaza badala viongozi wa chama kutangaza sera za chama chao wanacheza ngoma na kuonyesha maigizo

Hii ni thread ya 10000 kwa leo tu kuhusu Zitto. Mtaweweseka sana.
 
Naona kuwatoa mafisadi hakupo tena!!! mmeungana na TLP enzi hizo ..ACT kuwatoa watanzania haiwezekani!! haitatokea ila tuungane kwa pamoja pasipo chuki tuwangoe MAGAMBA.
 
Niliwambia Bavicha mnywe maji mengi na chakula cha kutosha ona sasa mnazidiwa na dozi...Hakika Saccos ina sambaratika...
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom