Live updates: Uzinduzi rasmi wa ACT-wazalendo - Diamond Jubilee Hall

Utatokwa sana na povu zito mwaka huu, endelea kubwabwaja. CHADEMA chama kubwa kama nguvu ya dola imeshindwa kuisambaratisha CHADEMA huyo msaliti Ayatollah Supreme Traitor kamwe hatafanikiwa....CHADEMA ni mfupa uliowashinda mafisi.....

Niliwambia Bavicha mnywe maji mengi na chakula cha kutosha ona sasa mnazidiwa na dozi...Hakika Saccos ina sambaratika...
 
Zitto apata pigo la kwanza,bado mapigo sita

Wakizindua chama alichokianzisha akiwa ndani ya CHADEMA kwa usiri mkubwa na Wenzake Samson Mwigamba,Kitila Mkumbo na akina Shonza,Chagulani na Kadawi Limbu,leo wamepata pigo.

Walitangaza kuwa uzinduzi wa ACT ungehudhuriwa na vyama rafiki,kile cha kijana Malema aliyeanzisha chama ndani ya ANC na kufukuzwa,Mh. Lipumba,vyama tawala vya Democrat,Labour,UMD, Mtoto wa Mwanzilishi wa Taifa la Ghana,viongozi kutoka nchi za kenya Rwanda na Sweden.

Pia alisema Mabalozi kutoka ujerumani wa SPD na CDU wangekuja.

Kilichotokea leo ni Thomas Ngawaiya na Ayatollah ndio waliofika.

Kiongozi mwingine aliyekuja pale ni mwakilishi wa CHAUMA.

Muda huu Zitto alisahau kuwa alishawahi kutangaza mali zake nusu,leo ndoo amemalizia,nadhani alikuwa akijiandaa kukwepa mzigo wa Tuhuma za magari ya kifahari na udhamini wa kurusha Mkutano huo.

Aidha Mh.Ibrahim Lipumba hakuhudhuria,hii inatafsiriwa na wachambuzi wa mambo kuwa,yeye Zitto mwaka jana wakati Vyama vya NCCR -Mageuzi,CHADEMA, CUF na NRA vilipoweka Mkataba wa ushirikiano kupinga katiba pendekezwa ya CCM na pia kuweka umoja katika kuwatetea watanzania dhidi ya madhila wanayoyapata.

Zitto aliuita Muungano ule ni wa viongozi na wasakatonge,hatajihusisha nao na ameandaa mkakati wa kuifuta CUF katika Mikoa ya Lindi,Mtwara,Tanga,Pwani,na pia atahakikisha CHADEMA inafutika Kigoma.Haya ndio yawezekana Ukawa wamesusia Mkutano huu.

Zitto ajue ndani ya bahari samaki ananguvu na ujanja Mwingi, sijui akivuliwa harafu ukamtosa ndani ya mto Mbwemkuru ,Ruvu au Malagarasi.

Naliona pigo,Maana Elyatonga Mrema amesusia?
 
Zito kwa miaka isiyozidi 15 ya UBunge, anamiliki mali nyingi kuliko Mwalimu Nyerere na utumishi wake wote aliotumikia Taifa na Mataifa
 
Mimi naona ACT kuwekeza kuipinga CDM ni aina nyingine ya utaahila. Unapowekeza kushambulia chama ambacho hakijashika dola ni umbumbumbu.

Kutangaza mali hizo ni unafiki, ni sawa na mganga njaa kubainisha njaa yake wakati anatafuta msosi akipata humwoni tena.

Kujisifia teja kujiunga na chama inaleta picha gani?
 
HOTUBA YA KIONGOZI WA CHAMA CHA ACT-WAZALENDO KATIKA UZINDUZI WA CHAMA na Ndugu ZITTO KABWE,,,, Watanzania wenzangu, wageni waalikwa
Nawashukuru kwa kuwa pamoja nasi siku hii ya
kihistoria.
Karibu Miaka 54 iliyopita tulipopata uhuru, Muasisi
na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere alikuwa kijana mwenye umri wa miaka 39,
mwenye matumaini makubwa na taifa jipya na
alikuwa na ndoto! Ndoto yake ilikuwa imejikita
katika kuhakikisha taifa letu litakuwa taifa lisilo na
umaskini, dhiki, ufukara; taifa lisilo na tofauti
kubwa kati ya maskini na tajiri; taifa lenye usawa,
haki na maendeleo, ambapo watoto wote
wanasoma shule bila kujali kipato cha mzazi; taifa
ambalo wananchi wake wanamiliki uchumi wao.
Ndoto hii aliiamini kwa dhati na wananchi wote
walikubali na kuota nae ndoto hii. Alilisimamia kwa
maneno na vitendo kupitia Azimio la Arusha, sera
zake na uongozi wake wa kizalendo. Mpaka mauti
ilipomkuta aliamini katika misingi hii aliyojitahidi
kuturithisha. Lakini miaka 16 baada ya kifo chake,
ndoto yake imeyeyuka!
Tulilonalo ni jinamizi alilolihofu Nyerere.
Leo hii:
Watanzania wachache wameondoka katika unyonge
na dhiki.
Watanzania wengi bado wapo katika hali ya dhiki.
Watanzania wachache wameshikilia uchumi:
Warasimu, Wanasiasa na Matajiri wachache wenye
mitaji.
Watanzania wengi bado kama Mwalimu Nyerere
alivyosema “wananyonywa kiasi cha kutosha;
wanapuuzwa kiasi cha kutosha”.
Ndoto ya Mwalimu Nyerere bado haijawafikia
wananchi.
Sasa ndio wakati wa mabadiliko ya kimapinduzi.
Sasa ndio wakati wa kujenga Uchumi shirikishi
ambao utaruhusu kila mwananchi kupata fursa ya
kuboresha maisha yake;
Sasa ndio wakati dola imara ipate nafasi ya
kusimamia uchumi;
Sasa ndio wakati kwa wananchi kuwa na uhuru wa
kweli wa mawazo, fikra, kushirikiana, kuabudu;
Sasa ndio wakati wananchi kuwa na nguvu ya
kuwawajibisha viongozi wao;
Sasa ndio wakati wetu watanzania kujirithisha upya
nchi yetu!
Huu ndio wakati wa kubomoa uchumi wa
kinyonyaji na kifisadi na kujenga uchumi wa
wananchi. Haya ndio mabadiliko ya kimapinduzi
tunayoyataka. Hii ndiyo ilikuwa ndoto ya Mwalimu
Nyerere, na muda umefika wananchi turejeshe nchi
mikononi mwetu!
Haya yamekuwa mawazo yangu kwa muda mrefu
kwa sababu mimi ni zao la ndoto ya Mwalimu
Nyerere. Nililelewa na mama yangu mzazi pekee
mwenye ulemavu; nimeanza kusoma shule ya
msingi nikiwa naenda peku. Lakini kutokana na
kufaulu mitihani vizuri, sikuhitaji kuwa tajiri
kusoma mpaka chuo kikuu. Leo hii kutokana na
elimu bora niliyoipata bure, nimesafiri na kufika
katika nchi zaidi ya 70; nikiwa kama kiongozi
nimekutana na kubadilishana mawazo na watu
muhimu duniani kama vile wakuu wa nchi. Sio
mimi peke yangu bali tupo maelfu tuliofaidika na
mfumo huu. Lakini muhimu kupita yote, nimeweza
kutumikia wananchi wa Kigoma na watanzania
bungeni kwa miaka 10. Kama hii si ndoto iliyokuja
kuwa kweli, ni nini?
Zitto Zuberi Kabwe angezaliwa mwaka 2000,
angekuwa kijana ambaye hajakamilisha elimu yake,
haelewi lugha za kigeni kama kiingereza, hana
ujuzi wowote na kama Mungu angeendelea
kuninyima kipaji cha kuimba kama sasa
ningeshindwa hata kutoka kama Diamond na
Mwana FA! Mwalimu Nyerere asingepigania ndoto
yake miaka ya 60 na 70, ningekuwa kama
mamilioni ya vijana leo ambao wanahangaika
kutafuta ajira na kipato bila ujuzi na elimu.
Na ndiyo maana siku ya leo ni muhimu kwangu.
Nina furaha na heshima kubwa kuwa katika familia
yangu mpya ya kisiasa. Familia inayoaamini katika
itikadi, misingi na tunu ninazoziamini.
Nimezungumza mara kadhaa kuhusu sababu za
kujiunga na chama hiki. Chama cha Wazalendo
ACT- Tanzania inaongozwa na misingi ya
Uzalendo, Demokarsia, Uhuru wa fikra na matendo,
Utu, Usawa, Uadilifu, Uwazi, Uwajibikaji na Umoja
katika kila kitu. Chama hiki ni cha wananchi si
wenyenchi wa sasa waliojimilikisha taifa. Chama
hiki ni cha watanzania wote bila kujali kabila, dini,
jinsia, rangi ya ngozi au hali ya ulemavu!
Tunapojadili wananchi kujimilikisha upya nchi yetu
ni kupitia usimamizi wa sheria utakaohakikisha
kuwa kuna uwazi na uwajibikaji wa viongozi.
Uwazi tunaouamini ni ule utakaohakikisha kila
mwananchi anapata taarifa za fedha zao, mikataba
ambayo Serikali inaingia kwa niaba yao na taarifa
za maslahi, mali na madeni ya viongozi wao.
Tunataka uwazi katika uendeshaji wa Serikali na
sisi tutaanza na uwazi katika uendeshaji wa chama
chetu. Tunataka wananchi sio tu wajione kuwa
sehemu ya uendeshaji wa nchi yao, bali pia wawe
sehemu ya uendeshaji wa nchi yao.
Tunataka uwazi utakaoruhusu uhuru wa mawazo
na uhuru wa wananchi kujieleza bila kuhofu
Serikali kuwachukulia hatua kwa kutoa mawazo
yao. Ndio maana ACT Wazalendo tunapinga vikali
miswada ya sheria ambayo Serikali ya CCM
imeiwasilisha bungeni katika mkutano
unaoendelea. Miswada hii kama vile muswada wa
Haki ya kupata taarifa, vyombo vya habari na ule
wa makosa ya mtandao, inalenga kuminya na
kunyima haki za wananchi kuwasiliana kwa uhuru
na kutoa mawazo yao kama inavyoainishwa katika
katiba ya nchi.
Tunapojadili wananchi kurejesha taifa mikononi
mwao tunazungumzia uwajibikaji. Ripoti ya Tume
ya Marekebisho ya Katiba ilieleza moja ya sababu
kubwa ya kushamiri rushwa, ufisadi na ubadhirifu
nchini ni nanukuu ‘kukosekana kwa mfumo
madhubuti wa uwajibikaji’ nchini kwetu. Sababu
kubwa ya ACT Wazalendo kupinga Katiba
inayopendekezwa ni kwamba Katiba hiyo
imechakachua nia hii ya kuweka mfumo wa
uwajibikaji. Ndio maana tunawaambia wananchi
waikatae Katiba hiyo kwa nguvu zao zote! Katiba
inayoepndekezwa inastahili kadi nyekundu, tuikatae
na kura ya hapana!
Iwapo wananchi hawawezi kuwawajibisha viongozi
kwa matendo yao hatuwezi kujenga jamii ya watu
wanaoheshimiana na kutii sheria za nchi.
Kila Mtanzania bila ya kujali cheo chake ni lazima
awe chini ya sheria. Uwajibikaji ni lazima uanze na
viongozi. Mnajua kuwa katika maisha yangu ya
kisiasa hili ndio limekuwa jukwaa langu. Kwa
bahati mbaya tunaishi katika kipindi ambacho
wanasiasa wengi wamekuwa wakikumbwa na
kashfa mbalimbali za kifisadi na matokeo yake
inajengwa picha kuwa kila mwanasiasa ni fisadi.
Mfumo wa Uwajibikaji wenye uwazi utasaidia
wananchi kutofautisha wanasiasa wanaosimamia
maslahi ya umma na wale wanaosimamia maslahi
yao binafsi na vyama vyao vya siasa.
Mwungwana ni vitendo; nimewajibisha watu
kwenye Buzwagi na mikataba ya madini, kwenye
matumizi mabaya ya fedha za umma na juzi juzi
kwenye akaunti ya Tegeta Escrow. Lakini matukio
haya machache hayatoshi kujenga mfumo
madhubuti wa Uwajibikaji. Ni lazima kufanya
mapinduzi ya mfumo mzima wa uchumi wa nchi
yetu na kujenga mfumo mpya unaohudumia kila
Mtanzania na ambao kila Mtanzania anajivunia
kuujenga. Hatuwezi kuwa Taifa linaloshikiliwa na
vikundi vya wafanyabishara wachache na
wanasiasa wanaofadhiliwa na wafanyabishara hao.
ACT Wazalendo inataka kujenga Taifa ambalo
viongozi wake wanawajibika kwa wananchi. Hii
ndio fikra tunayotaka kurejesha. Hizi ndizo siasa
zilizoasisi Taifa letu. Hatuna budi, ni lazima kurudi
kwenye misingi na kuanza upya!
Kwa sababu ACT Wazalendo imejikita kwenye
misingi hii, tumelihuisha Azimio la Arusha.
Sio tu tumeweka miiko ya uongozi lakini pia
tumetunga kanuni za kutekeleza miiko hiyo na
kuifanya kuwa sehemu ya Katiba ya chama chetu.
Hitaji moja kubwa la Kanuni zetu za Maadili ni
kutaka kila Kiongozi wa ACT Wazalendo kuweka
hadharani Maslahi yake, Mali na Madeni yake.
Katika chama hiki huo ndio utamaduni wa kisiasa
tunaotaka kuujenga. Kutenda tunachohubiri hata
kabla ya kuingia kwenye uongozi wa Dola.
Chama cha ACT Wazalendo kimeelekeza kikanuni
kwamba kila Kiongozi wa chama lazima atangaze
Mali zake na Madeni yake. Kila Kiongozi lazima
aweke wazi maslahi yake ya kibiashara na
mengineyo wazi ili kila anapotenda au kusema
jambo wananchi wajue maslahi aliyonayo au la
katika suala husika. Viongozi wote wa kitaifa wa
ACT Wazalendo wamefanya hivyo na tutaweka saini
zetu mbele yenu kama mashahidi. Naomba
Mwanasheria wetu aje hapa tutekeleze matakwa
haya ya kikanuni.
Fomu hizi zitakuwa kwenye tovuti ya chama ndani
ya muda mfupi ujao ili kila mtanzaina aone. Kila
Kiongozi wa Chama ambaye Miiko ya Uongozi
inamtaja anapaswa kuwa amejaza fomu hizi na
kuziwasilisha kwa Katibu wa Kamati ya Uadilifu
katika ifikapo tarehe 30 Juni 2015. Tunapopinga
Viongozi wa Umma kufanya Biashara na Serikali na
hivyo kuwa na mgongano wa kimaslahi na
kushamiri kwa ufisadi, hivyo hivyo tunapinga
Viongozi wa Chama chetu kufanya Biashara na
Chama. Ni Marufuku Serikali kugeuzwa kuwa
genge la watu wachache wanaopora rasilimali za
Umma. Uadilifu tunaoutaka Serikalini ni lazima
uanzie kwetu tunaohubiri.
Tutafanya haya kwa kubadilisha siasa zetu
kuelekea kwenye masuala yanayowahusu
wananchi; Wakulima, Wafanyakazi,
Wafanyabiashara ndogo ndogo, Vijana, Wanawake
na Wazee wetu.
Tunataka kurejesha nchi yetu Tanzania kwa
kujenga uchumi wa wote. Tunaporejea kwenye
Azimio, hatusemi tunakwenda kutaifisha kila kitu na
Serikali kuendesha shughuli zote za kiuchumi.
Tunaheshimu na kuthamini sekta binafsi na
mchango wake katika kukuza uchumi na kuleta
maendeleo. Tunamaanisha kuwa ni lazima Dola
isimamie uchumi. Sio kazi ya Serikali kufanya
biashara. Lakini tunamaanisha kuwa ni lazima
kurekebisha baadhi ya makosa yaliyofanyika
kwenye ubinafsishaji na hususan ubinafsishaji
holela uliofanyika kwenye sekta ya Kilimo na
kupora ardhi ya wananchi wetu na kuwageuza
kuwa manamba kwenye ardhi yao wenyewe.
Tunataka kutomokeza ukwepaji kodi.
Tanzania inapoteza 15% ya makusanyo katika
forodha kwa sababu ya ukwepaji wa kodi. Hii ni
sawa na tshs 490 bilioni kwa mwaka, fedha
ambazo zingeweza kuchangia wananchi milioni 4
kwenye hifadhi ya Jamii. Tanzania inapoteza
takribani tshs 2 trilioni kila mwaka kwenye
misamaha ya kodi. Hii ni fedha ambayo ingeweza
kujenga reli mpya ya kati ya kisasa kutoka Dar
mpaka Mwanza na Kigoma ndani ya miaka mitatu.
Ili kuondoa upotevu huu ni lazima kupanua wigo
wa kodi, kurahisisha kodi, kupunguza baadhi ya
kodi kama ( PAYE) na kutumia teknolojia kuziba
mianya ya ukwepaji wa kodi.
Vile vile ni muhimu kuimarisha mfumo wetu wa
kodi za kimataifa ili kuzuia utoroshaji mkubwa
unaofanywa na makampuni ya kigeni. Ili
tujitegemee kama Taifa ni lazima kukusanya
mapato ya ndani ya kutosha. Ili kukusanya mapato
ya ndani ya kutosha ni lazima kuweka mazingira
mazuri ya biashara hasa kwa wafanyabishara
ndogo ndogo kwani ndio wazalishaji wakubwa wa
ajira.
Kwa Vijana, Taifa hili ni lenu. Asilimia 75 ya
Watanzania wapo chini ya miaka 40. Asilimia 65 ya
wapiga kura wapo chini ya miaka 40. Nusu ya
Watanzania ni watoto chini ya miaka 18. Kurejesha
nchi kwenye misingi ni wajibu wa kujenga maisha
yenu. Haikubaliki Vijana kuwa mzigo kwa wazazi
kwa sababu tu uchumi hauzalishi ajira za kutosha.
ACT Wazalendo ndio jukwaa lenu la kufanya
mapinduzi ya mfumo wa uchumi ili kujenga
uchumi shirikishi unaozalisha ajira. ACT Wazalendo
inataka kuwajengea mfumo wa hifadhi ya jamii
ambapo mtakapokuwa Wazee msipate tabu za
pensheni na matibabu wanazopata Wazee wetu hivi
sasa. Shiriki kujijengea Taifa litakalohakikisha
maisha yako ya sasa nay a baadae na ya kizazi
kijacho.
Kwa Wanawake, Ninyi ndio mhimili wa Taifa hili,
wazalishaji wakuu na walezi wa Taifa letu.
Kurejesha nchi kwenye misingi ni wajibu wa
kutambua nafasi yenu stahili katika jamii. Nikiwa
nimelelewa na Mwanamke mwenye ulemavu na
mpiganaji wa kweli wa haki za wananchi walio
pembezoni, sina namna kutoa heshima yangu zaidi
ya kuongoza chama chenye misingi thabiti ya
kumkomboa mwanamke. Msitarajie watu wengine
kuwapigania mnapaswa kuchukua hatua kupitia
jukwaa hili la ACT Wazalendo.
Kwa wafanyabishara, ninyi ndio mnachochea
shughuli za Uchumi na kuzalisha ajira. Kuanzia
kwa wamiliki wa maduka madogo mitaani mpaka
kwa mameneja wa maduka makubwa; kutoka kwa
wachuuzi na mama lishe mpaka kwa wamiliki wa
viwanda na biashara; mnaamka kila siku asubuhi
kujenga Taifa hili kwa kuzalisha mali na huduma.
Baadhi yenu ambao mnamiliki viwanda, mashirika
makubwa na kutoa ajira kwa maelfu ya wananchi,
mmeanza mkiwa mnashona viatu na sare za shule,
au mkitengeneza na kuuza mkate. Mmepata utajiri
wenu na mali zenu kwa juhudi na jasho lenu na
kutokana na fursa za kiuchumi zilizokuwepo
kipindi hicho ambacho hakikuangalia dini, kabila,
uwezo wa kifedha au rangi ya ngozi. ACT
Wazalendo inataka kuwawekea mazingira bora ya
biashara halali lakini pia kuhakikisha mnalipa kodi
zenu na kutonyonya wafanyakazi wenu. Tunataka
kuwawekea mfumo rahisi wa kodi, wenye
kueleweka na unaowapa motisha kuzalisha zaidi ili
kuongeza ajira zaidi na kupanua Pato la Taifa.
Msipotimiza wajibu wenu biashara zenu
hazitashamiri. Kurudi kwenye misingi ya Taifa hili
ni kurejesha maadili katika biashara zenu.
Kwa Wakulima, Wafugaji na Wavuvi, ninyi ndio
mnaolilisha Taifa letu na kuleta fedha nyingi za
kigeni kupitia mauzo nje. Kwa miongo mitatu sera
za nchi zimewaweka pembeni na hivyo uchumi
wenu kusinyaa. Viwanda vyote vya kusindika
mazao yenu vimeuzwa kwa bei ya kutupwa licha
ya kwamba jasho lenu ndio lilitumika kuvijenga.
Miundombinu ya barabara, maji, umeme na
mawasiliano haiwafikii ili muweze kupata masoko.
Hamna hifadhi ya jamii wala bima ya mazao yenu.
Ardhi yenu wamepewa wawekezaji na
mnakodishiwa, mnapanga kwenye ardhi yenu
wenyewe. Mmeachwa mkijihangaikia. Kurejesha
nchi kwenye misingi kutawarudishia heshima yenu
katika nchi yetu. ACT Wazalendo ndio jukwaa
sahihi kwenu kuhakikisha kuwa tunajenga uchumi
shirikishi ambao mtafaidika na jasho lenu. Hamna
cha kupoteza isipokuwa minyororo ya kinyonyaji.
Kwa Watanzania wote mnaonisikiliza leo, katika
ukumbi huu na popote mlipo kupitia vyombo vya
habari, mnamo mwaka 1978 Baba wa Taifa
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alitangaza vita
dhidi ya nduli Idi Amini na kusema;
“Tutampiga. Sababu za kumpiga tunazo, nia
tunayo, uwezo wa kumpiga tunao”.
Tanzania ipo katika vita hivi sasa.
Vita dhidi ya Ufisadi,
vita dhidi ya uporaji wa rasilimali zetu,
vita dhidi ya Siasa chafu.
Vita dhidi ya Uchumi wa kinyonyaji.
Vita dhidi ya kuporomoka kwa Utaifa wetu.
Tunapaswa kufanya jambo moja tu, nalo ni
kupigana vita hizi. Ni vita kwa ajili ya kurejesha
ndoto tuliyoota miaka 54 iliyopita na Muasisi wetu
Mwalimu Julius Nyerere. Tunataka kurejesha nchi
kwa wananchi, tunataka kujimilikisha nchi yetu.
Wananchi wawe WENYE nchi! Tutimize ndoto yetu
ya kuona;
Tanzania yenye Dola madhubuti,
Tanzania yenye Wananchi wenye mwamko,
Tanzania yenye sekta binafsi iliyochangamka,
Tanzania yenye uchumi unaonufaisha watu wote.
Sababu tunazo, nia tunayo na uwezo tunao.
Twendeni tukajenge Chama kitakachorejesha
misingi ya Taifa letu.
Asanteni sana
Mzalendo Zitto Kabwe
 
nahisi vyama hivi vimeonesha tabia ya kutokomaa kisiasa za kitoto,kisasi,chuki,wivu,na uoga ni tabia MBAYA,vimewazuia wabunge wake pamoja na kumshinikiza prof. kutohudhuria uzinduz wa ACT Leo n tabia mbaya,ni dalili za chama hicho kufa
 
Mkuu umewahi sana kutoa huu uzi, na bado mambo wanayotegemea kutoka kwa zito wakiyakosa watajua kuwa zito ni zaidi ya msaliti
 
Hizo ndizo changamoto zenyewe, MWANZO MGUMU NA ACT HAIKUJIANDAA KUCHEZA LELEMAMA!
NB: KAMA ULIVYOSHUHUDIA, UMATI ULIOHUDHURIA SI HABA, UKIACHA WENGI TULIOHUDHURIA KWA NJIA YA LUNINGA. THE MESSAGE HAS BEEN SENT!
 
Mkuu, kama unamrejelea ZZK kuhamia chama kingine, ZZK hakuhama CDM ila afukuzwa automatically baada ya kukipeleka chama mahakamani kinyume na katiba ya chama.

HAKUNG'ATUKA, ALIFUKUZWA
Wapi imeandikuwa kuwa ukishakuwa mwanachama wa chama fulani hutakiwi kuhama na kwenda kwingine?

Wapi imeelezwa kuwa raia haruhusiwi kujifananisha na Kiongozi wake wa kwanza as long as ni mzalendo?

Btw, nimeambiwa kuwa Gf wa slaa nae yupo! hahahaaa!

Chadema kazi mnayo..
 
UKAWA vyupi vimewajaa mizigo kutokana na kusahau kwenda maliwatoni ha haaaa!
 
Naona vyama hivi vina siasa za kitoto,kisasi na kuzira kama tabia za zamani kike maana hata tabia za mwanamke wa leo anajitambua na anafanya vyema,CHADEMA kuwazuia wabunge wake kutohudhuria uzinduz wa ACT Leo n tabia mbaya,na ni dalili za chama hicho kufa

Unalo hilo limekukaa, ulitegemea chama kilicho anzishwa kupambana na wapinzani wa ccm kiheshimiwe na nani kama siyo wafuasi wa zito pekee?
 
Back
Top Bottom