Live updates: Tukio la Bomu Mbowe na JK watembelea Arusha

Live updates: Tukio la Bomu Mbowe na JK watembelea Arusha

Joined
Dec 11, 2010
Posts
3,321
Reaction score
6,331
Wakuu

mtakumbuka kuwa baada ya tukio la mlipuko wa bomu pale Arusha nchi imekuwa kwenye mtanziko hasa ukizingatia kuwa lilikuwa tukio la kigaidi.

Pamoja na majonzi ya tukio la bomu, there's a nice colour story here, namna ambavyo Rais Kikwete na Kiongozi wa Upinzani Bungeni Mheshimiwa Mbowe wanapishana hapa mjini Arusha, huyu akipita hivi, huyu anapita vile. Wote wamekuja kwenye tukio hilo la bomu.

• Kwa sasa JK yuko Mount Meru Hoteli (ndo ameanzia hapo), Mwenyekiti Mbowe ametoka kule eneo la tukio kanisani, kapita ofisi za chama, punde ataelekea, St. Elizabeth Hosp, kisha, Mount Meru Hospital kuwaona majeruhi na baadae anatarajiwa atakwenda kuwaona wafiwa (familia).

• Mwenyekiti Mbowe amezungumza na press pale Mt. Meru Hosp, baada ya kumaliza kuwajulia hali wagonjwa katika hospitali za St. Elizabeth na Mt. Meru akiwa ameanzia kanisani eneo la tukio.

• Sasa Mbowe anaelekea kwenda kuwaona wafiwa, akianzia eneo la Elerai, jijini Arusha.

• Ndo tumefika hapa kwenye famili yenye msiba, kwa Baba Furaha, aliyefariki alikuwa ni mtoto wake akiitwa Patricia, alikuwa anasoma darasa la 3 S/m Eliarai, alikuwa na umri wa miaka 9. Alikufa kutokana na mlipuko wa juzi kanisani.

• Tumekwenda familia moja, zingine mbili zilizobaki kesho mapema asubuhi!

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums.
 
Mambo ya kusubiria kulaani na kutoa pole wakati wanalea tatizo linalojulikana ni Ujinga tu,hakuna jipya wasubiri saa 2 usiku wajione kwenye Taarifa ya Habari.
 
Wanasiasa na viongozi wa dini ni chanzo cha matatizo

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Wewe mtoi umoteza credibility a kuripoti matukio, umezidiwa na mahaba ya kichadema mno, rais hawezi kwenda hotelini wakati alienda kwenye tukio la mabomu...wadanganye wajinga wenxio
 
Wakuu

mtakumbuka kuwa baada ya tukio la mlipuko wa bomu pale Arusha nchi imekuwa kwenye mtanziko hasa ukizingatia kuwa lilikuwa tukio la kigaidi.

Pamoja na majonzi ya tukio la bomu, there's a nice colour story here, namna ambavyo Rais Kikwete na Kiongozi wa Upinzani Bungeni Mheshimiwa Mbowe wanapishana hapa mjini Arusha, huyu akipita hivi, huyu anapita vile. Wote wamekuja kwenye tukio hilo la bomu.

• Kwa sasa JK yuko Mount Meru Hoteli (ndo ameanzia hapo), Mwenyekiti Mbowe ametoka kule eneo la tukio kanisani, kapita ofisi za chama, punde ataelekea, St. Elizabeth Hosp, kisha, Mount Meru Hospital kuwaona majeruhi na baadae anatarajiwa atakwenda kuwaona wafiwa (familia).

• Mwenyekiti Mbowe amezungumza na press pale Mt. Meru Hosp, baada ya kumaliza kuwajulia hali wagonjwa katika hospitali za St. Elizabeth na Mt. Meru akiwa ameanzia kanisani eneo la tukio.

• Sasa Mbowe anaelekea kwenda kuwaona wafiwa, akianzia eneo la Elerai, jijini Arusha.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums.

Lazima MBOWE awahi arusha na kumkanya LEMA asije akalikoroga tena kwa sababu yule anapenda kuona matukio kama hayo yakitokea ili ajipatie umaarufu.
 
Asante sana kwa taarifa mkuu Mohamedi Mtoi.Mungu awatangulie.
Mbowe hawezi kukubali kuonana na President kwa vile ameonesha udhaifu mkubwa wa kuongoza kambi ya upinzani bungeni jambo ambalo limepelekea wabunge wake wawe kama watoto wa vijiweni.
 
Tukio lilipangwa na lema, mbowe ameenda kuwazingua tu machalii wa a town
 
Uripoti wa matukio wa aina ya mtoi ni janga la kitaifa
mkuu ulitaka atubukize uongo wenu ule tuliouzoea? haya isomeke hivi "MBOWE apokelewa kwa maandamano makubwa kuliko JK" hapo vipi umejisikia raha? teh teh teh teh CHADEMA bwana kama mitoto vile.
 
Janga la taifa ni pamoja na kuwaza mabaya kwa niaba ya mwenzako.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums.

kweli kabisa mkuu, jamaa lipo kishari shari tu, na hizi ni dalili za kutokuwa na hoja.
 
Mohamedi
Mtoi
labda hii inaonesha kwakuwa Mbowe ni mkristo basi ana
huruma na watu halafu Jk ni muislamu kwa hiyo ni Gaidi amekwenda Mount
Meru kusherekea mauaji yaliyofamywa na ndugu zake.

mkuu, kwa hiyo jk ni mkristo? mbona aliyelipua lile bomu ni mkristo? wewe una ajenda ya kwako
 
Last edited by a moderator:
mtoi mimi sijaona kitu cha ajabu hapa sasa wewe unataka wote wafuatane kwani ni kumbikumbi hawa au ni maharusi ukikosa cha kuandika acha mkuu utashuka thamani.
 
wewe mzandiki kweli. kwa hiyo hapo mt meru hoteli ndo kwenye tukio? au ulitafuta tu jinsi ya kumpamba ndugu yako mbowe
 
Mambo ya kusubiria kulaani na kutoa pole wakati wanalea tatizo linalojulikana ni Ujinga tu,hakuna jipya wasubiri saa 2 usiku wajione kwenye Taarifa ya Habari.

Hasa huyu Mbowe anataka tu aonekane kwenye runninga.
 
Nasema na ntasema kunawatu wako milembe day,mohamed mtoi unatupeleka wapi post gani hizi sasa,utakuwa uko milembe day mda wote umekaa kiuchochezi tu na uchonganishi halafu we ni mtu mzima sana kwa nini usijiheshimu ulete post zenye kujenga,sasa hapa ulikuwa unataka kufikisha ujumbe gani kwa jamii.
 
Back
Top Bottom