LIVE UPDATES: Mkutano wa CCM Morogoro

Haya ni mawazo yako, CCM inasonga mbele. Kama kwenu wanawake wenye mikorogo hawatakiwi kuwa wanachama, wapenzi au mashabiki wa chama. kwa CCM wanakaribishwa kwa sababu tunaamini BINADAMU WOTE NI SAWA, na HATUBAGUI MTU YOYOTE KUTOKA PANDE YOYOTE ILE YA TANZANIA.

Ujumbe wako naona umefika. kwa CHADEMA, hawatakiwi watu wenye mkorogo.


 
Mkuu hawa jamaa ni janga la taifa,
Wengine wameacha hata kufanya kazi wanasubiri 2015
 
Wanahangaika na picha wakati mkutano ulikuwa LIVE kwenye TV na pia kwenye radio.

Hakuna cha spinning hapa, kama ni lugha ya picha tunaifahamu sana.

Wasije tu wakapatwa na ghafiriko la moyo. inabidi waanze kuzoea mapema.

Hii ni CCM na inasonga mbele.

Wao wakiwa bado wanafikiria nani atakuwa mwenyekiti na katibu wa chama taifa baada ya 2013, sisi tunajiandaa na zoezi lililo mbele yetu la mchakato wa katiba.
 
Kinana ameimaliza Chadema Morogoro kwa kuwaeleza wananchi namna inavyoshiriki mambo ya hovyo hovyo, ikiwemo uzushi na vurugu.
Mie naomba unitajie jina la Mbunge wa CHADEMA ambae jana ulituambia kwamba angejiunga CCM leo wakati wa mkutano wa Morogoro!!Bila shaka ameshajiunga tayari; ni nani?
 
Ukitaka kujua CCM ni nani angalia uchaguzi wa madiwani mwishoni mwa mwaka jana utapata jibu
 

Angalia AKILI ndogo hii, HIvi bila Nyerere kutoka BUTIAMA, MREMA si anangesha wanyonga MACCM wote.
yani hata Historia ya 95 tu huijuhi.
kweli wewe mgonjwa!
 
pamoja na kuwepo thread zaidi ya ishirini zilizoripoti juu ya mkutano wa CCM MOROGORO, pia live update ya mkutano imepata uchangiaji mkubwa kuliko ile Chadema! Je hii inaashiria chadema hawana mvuto tena kwa wanaJF au yanayoongelewa na chadema kwa sasa ni yale yale kiasi kwamba watu wakatega masikio Morogoro!
 
Mkuu hawa jamaa ni janga la taifa,
Wengine wameacha hata kufanya kazi wanasubiri 2015
Kwa mawazo waliyonayo, baadhi yako hakuna hata maana ya kuwasikitikia. Wako kwenye ndoto za mchana ambazo zimeisha kuwa kama gundi.

2016 itawafundisha mengi pale watakapo uona ukweli wa neno CCM yasonga mbele.
 
Angalia AKILI ndogo hii, HIvi bila Nyerere kutoka BUTIAMA, MREMA si anangesha wanyonga MACCM wote.
yani hata Historia ya 95 tu huijuhi.
kweli wewe mgonjwa!
Sikatai Mrema alikuwa na nguvu sana na bila kuingia Mwl Nyerere mchuano ungekuwa mkali lakini ni sehemu ya CCM na Kinana ndie alieongoza kampeni,
Anyway wewe kinakuuma nini ya upande wetu? nyie endeleeni kushughulikia suala la Lwakatare
Kwanza nimeanza kuamini kuwa kwa namna moja au nyingine suala la Uli mnahusika, Ningekuwa bado kwenye kazi yangu ya zamani lazima ningeomba nimweo kwenye timu inayopeleleza hii kesi....
 

 
Angalia AKILI ndogo hii, HIvi bila Nyerere kutoka BUTIAMA, MREMA si anangesha wanyonga MACCM wote.
yani hata Historia ya 95 tu huijuhi.
kweli wewe mgonjwa!
Kwani nani aliyekuwa master plan wa kumuingiza Mwl Nyerere kwenye kampeni za Rais Mkapa baada ya kubaini mapungufu kwenye kampeni. Think bigger.
 
Kwa mawazo waliyonayo, baadhi yako hakuna hata maana ya kuwasikitikia. Wako kwenye ndoto za mchana ambazo zimeisha kuwa kama gundi.

2016 itawafundisha mengi pale watakapo uona ukweli wa neno CCM yasonga mbele.
Mkubwa ninachoogopa ni baada ya 2015 hawa vijana watafanya nini kwani wengi watakuwa wameisha kata tamaa ya maisha
Inabidi serikali ijiandae na mlipuko wa watu kujinyonga
 
Mkuu, Inawezekan ni mmoja wa vijana wa CHADEMA DIGITAL. Hajui nani aliyekuwa kinara wa kampeni 1995 ambaye ndiye aliyeona umuhimu wa kumuingiza Mwl. Nyerere kwenye kampeni na wakaenda kumuomba kufanya hivyo.
 
aibu ilianzia jana, kwani kutokana na hofu ya watu kutojitokeza katika mkutano huo, gari la matangazo lilizunguka mji mzima lilikuwa likirudia kuwa ''msanii diamond atakuwepo kutoa burudani'' naamini hii ilikuwa ili kuwavutia ''watoto'' wajae.!
leo toka asubuhi mbunge wa morogoro mijini aziz aboud alitoa magari yake kusomba watu kutoka kila kona ya mkoa.!
lakini wapi, mpaka mkutano unaanza watu walikuwa wachache sana. watu waliongezeka idadi kidogo mara baada ya msanii diamond kuanza kutumbuiza , lakini alipomaliza watu wakaanza kutimka na ndipo nape aliingilia kati na kuwasihi watu ''jamani tutamkaribsha tena diamond baada ya katibu mkuu kuhutubia''..!!
kwa kifupi idadi ya watu ilikuwa ni kama vile ''mkutano wa mtaa'', watu almost wote tulipata viti vya kukaa.!
cha ajabu zaidi ni hotuba za viongozi: mwenyekiti wa mwenyekiti wa morogoro mjini yeye baada ya kusalimia tu neno lilofuat ni ''chadema'' na hotuba yake yote ilihusu chadema. nape yeye nadhani wote mnamfahmu hakuwa na chochote cha kuongea zaidi ya cdm cdm cdm.! angalau mbunge mhe. aboud kidogo yeye alijitahidi neno chadema alikusikika kabisa kinywani kwake.
yeye kinana baada ya kukaribishwa alianza hotuba yake poa kidogo lakini alipofikia katikati ali-lose track nayeye akaanza kuimba chadema.! na huo ndio ukawa wimbo wake kwa hotuba yake yote.!

PICHA HIZI HAPA...!!!



 
Mkuu, Inawezekan ni mmoja wa vijana wa CHADEMA DIGITAL. Hajui nani aliyekuwa kinara wa kampeni 1995 ambaye ndiye aliyeona umuhimu wa kumuingiza Mwl. Nyerere kwenye kampeni na wakaenda kumuomba kufanya hivyo.
Hawa makamanda makamasi noma sana
Lakini mkuu Mwana Diwani inabidi tuishauri serikali ifungue hospitali maalumu ya kutibu magonjwa ya moyo na depression kwani nina uhakika mwaka 2015 Makamanda wengi watajirusha kutoka ghorofa ya kwanza na kujiua kama sio kupata mshtuko wa moyo au zubaiko la akili
 
Katibu wa ccm mkoa wa moro sixtus mapunda anasema watu 4300 wamejiunga na ccm ktk ziara ya kinana mkoani moro

Kwa kupika data hatuwawezi. Ndio nyir mnaosema inflation iko 10% wakati uhalisia ni 17%
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…