Live on Star TV: Bajeti 2012/13 utekelezaji na utashi wa kisiasa

Unapokuwa na Viongozi wenye uwezo mdogo wa kufikiri kwa kuamini kwamba misaada ya wafadhili iwe ya kutegemewa saana kuliko kutafuta mbinu mbadala za namna ya kupata fedha (Kodi) ya ndani, imepelekea kuwa na Bajeti ya Maneno kuliko Bajeti halisi, kwa sababu huwezi kutegemea wafadhili kupanga mipango yako ya maendeleo.

Wanaona sifa kusema tumepata Msaada kutoka kwa wafadhili hii ni aibu kwa nchi na wananchi wake ni udhalilishaji mkubwa na hakuna maendeleo yanayoweza kupatikana kwa kutegemea misaada, Tuna kila kitu ni aibu kutegemea misaada
 
Yahya,
Hongera kwa mjadala mzuri...
Bajeti zilizopita (ukitoa kindi cha mwl JK), bajeti hii na bajeti zijazo kamwe hazitaweza kumsaidia mwananchi wa kawaida! hii ni kutokana na ukweli kuwa;-

1. Mipango yetu mingi tunapangiwa na nchi za kibeberu kupitia wabakaji wao wa kiuchumi yaani Economic Hit Man (EHM). Hawa wabakaji ndio tuliowapa dhamana ya kutuendeshea uchumi wetu tukiwaona kuwa ni wasomi wenye exprnce za WB na IMF.
2. Sera zote za maendeleo tunaandikiwa na hao EHM mfano sera ya madini, fedha, BOT act nk
3.Sisi kama nchi tunafumbia macho mambo yenye maslahi ya kitaifa mfano ktk bajeti hii imetoa misamaha ya kodi kwa vifaa vya kuchimbia madini eti emaamuliwa na nchi wanachama wa EA! hivi hizi nchi jirani tulioungana nazo wanachimba madini kwa kiasi gani kwa ujumla wao ukilinganisha na sisi?...

.... kama nchi tuwe na sera na mikakati yetu wenyewe japo itakuwa ni vigumu sana kuwazuia hawa EHM ambao tumewapa dhamana ya kututawala kwa sasa...
Maoni yako yamesomwa,

Leo ndo nimekumbuka kuwa Mkullo alienda Marekani "kuandaa bajeti". Tunaburuzwa tu
 
Yahya, ruzuku kwa vyama vya siasa ni suala linahitaji mjadala, wapo watu kama marcus na nape wanaoamini vyama vya siasa viendelee kukunja zaidi ya bilioni 1.2 kwa mwezi tupo sie kina uswege tunaoamini hii si sahihi hata kidogo.

tunaomba jumapili moja utuwekee hii mada
 
Back
Top Bottom