Live: Kutoka Mbamba bay mkutano wa Dk. Slaa

Chishango

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2008
Posts
875
Reaction score
363
Wakuu kama nilivyowaeleza jana kuwa kutakuwa na mkutano mkubwa hapa Mbamba Bay watu wanaendelea kumiminika uwanja wa Polisi hapa Mbamba Bay wakimsubiri Dk. Slaa.

Mch. msigwa ameshawasili hapa pamoja na viongozi wengine, katibu wa chama wilaya anamkaribisha mch. Msigwa naye anawasalimia wananchi na moja kwa moja anawaambia kuwa Rais wetu ni mtalii nchi ina rasilimali nyingi lakini inafilisiwa na wezi yaani CCM.

Bado dk. Slaa hajawasili.

UPDATE:
Dk slaa kawasili kwa helikopta analakiwa kwa vifijo na nderemo na vigelegele akina mama wanalala chini hali inayomzuia kuendelea kuelekea jukwaani ...hatimaye anapanda jukwaani anakaribishwa mara moja ili kwenda na wakati....anaanza kwa salaamu ya chama then anaomba radhi kwa kuchelewa anawaambia wanyasa kuhusu maendeleo chini ya serikali hii ya CCM wasahau kwani hawana jipya wamechoka hawana visheni....anagusia kuhusu safari za rais anawaambia wanyasa safari ya juzi ya JK ni ya 358 tangu aingie madarakani hana muda na watanzania na watz waliomchagua .......anaendelea.... CCM wana mpango a kuhujumu mchakato wa katiba mpya hawataki kuona katiba ya watanzania wote inapatikana....anawaambia wananchi kuwa zaidi ya 72% ya mapendekezo ya rasimu ya katiba mpya ni ya Chadema....anawaambia vijana wajitokeze kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la kudumu anamaliza na kuondoka kuendelea na ratiba maeneo mengine.




 

Attachments

  • 1085227_563193920438965_1701766001_n.jpg
    28.2 KB · Views: 1,864
  • 1558790_563194133772277_494047750_n.jpg
    27 KB · Views: 1,834
  • 1608747_563208360437521_1809778408_n.jpg
    44.9 KB · Views: 1,581
Na bado wale woote wakaanga sumu watazinywa wenyewe tutawakimbiza mpaka 2015.
 
Hii hatari kabisa, yaani msururu wote huo na Dr. bado kufika?
 
tupe update za kutosha pamoja na picha
 
Teh teh teh ccm chali,Nape wapi iyoooo hahahaaaa Kinana kimya baada ya Jk kutangaza baraza la Mawaziri...
 
Hongera Chadema Chama cha Walinzi wa Rasilimali za Taifa.

Hilo jina la Mbamba Bay linafanana kama Congo vile,
 
Hongera Chadema Chama cha Walinzi wa Rasilimali za Taifa.

Hilo jina la Mbamba Bay linafanana kama Congo vile,

Unaonekana kilaza wa kutupwa..CDM wamelinda rasilimali gani za taifa?

Na umesoma Jografia gani ya kuifananisha Mbamba bay na Congo?..dIV5 Loading.............
 
MIMI namtaka nape na KINANA na kamati kuu ya CCM waliafikiana vipi na JK kuendelea na mawaziri mizigo?hapo ndipo tunawataka waje kutueleza mawaziri mizigo ina maana JK yeye awaoni big up CHADEMA toeni elimu ya uraia
 
kamanda tunakushukuru sana kwa uaminifu wako , jana ulituahidi kutuletea live updates na leo umetimiza , ubarikiwe sana .
 
Watu weweeeeeeee!!!!!!!!!!chadema wamechachamaa cha! tupe mavitu kijana
wapi mwanamuziki komba nyoka kaingiga chumban lazima utoke
 
hiki chama kinanifurahisha huwa hakiishiwi mipango hata, Hakiishiwi rasilimali watu pia, wasaliti wameondoka sasa hivi kimekuwa chepesi kweli.
 
Tumaini Makene
Kurugenzi ya Habari
walipaswa kutupa live update
na picha za ukweli utashangaa hiyo kazi wanaachiwa ccm waweke picha za baada au kabla ya mikutano.
 
Last edited by a moderator:
mleta mada nakupa hongera ila picha zako hazina kiwango na hazichukui eneo kubwa la mkutano
 
Hiki chama kinanipa raha hatari.....lets keep on moving
 
hiki chama kinanifurahisha huwa hakiishiwi mipango hata, Hakiishiwi rasilimali watu pia, wasaliti wameondoka sasa hivi kimekuwa chepesi kweli.

hiyo ndiyo cdm mkuu , waliodhani tunatania wataisoma namba !
 
Makamanda tukotayari kukabidhiwa nchi na mah.uni, ya ccyem yanayopagawa yakisikia jina chadema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…