Mshindi wa Vita
JF-Expert Member
- Mar 5, 2025
- 260
- 98
View: https://www.youtube.com/live/0oisjyeeiTk?si=ZyTQ-O1IFxIhOKkd
MDAHALO KUHUSU UENDESHAJI ENDELEVU WA BANDARI UNAENDELEA PEACOCK HOTEL
Baraza la Wasafirishaji Tanzania (Tanzania Shippers’ Council – TSC) leo linaendesha mdahalo wa ngazi ya juu wa Sekta ya Umma na Binafsi (Public–Private Dialogue) unaolenga kujadili uendeshaji endelevu wa bandari na maendeleo ya miundombinu ya biashara nchini.
Mdahalo huo unaendelea leo katika Hoteli ya Peacock, jijini Dar es Salaam, kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni, ukiwakutanisha zaidi ya wadau 100 kutoka taasisi za serikali, mamlaka za bandari na usafirishaji, watoa huduma za lojistiki, waingizaji na wasafirishaji wa bidhaa pamoja na wamiliki wa mizigo.
Mdahalo huu unaongozwa na kaulimbiu isemayo:
“Kukuza Uendeshaji Endelevu wa Bandari Kupitia Ushirikiano wa Sekta ya Umma na Binafsi.”
Mzungumzaji mkuu katika mdahalo huu ni Bw. David Kafullila, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ushirikiano kati ya Sekta ya Umma na Binafsi (Public-Private Partnership Centre – PPPC), ambaye anatoa hotuba kuhusu namna ushirikiano wa sekta ya umma na binafsi unavyoweza kuimarisha miundombinu ya biashara na kuongeza ufanisi wa bandari.
Aidha, Kanali (Mst.) Joseph Leon Simbakalia anatoa mada ya kiufundi inayolenga kuimarisha miundombinu ya uagizaji na usafirishaji wa bidhaa kwa ajili ya ushindani wa biashara ya kikanda na kimataifa.
Mdahalo huu pia unamshirikisha Bi. Bona Felix, Meneja wa Uendeshaji wa Terminal wa Tanzania East Africa Gateway Terminal Ltd (TEAGTL) na Mwenyekiti wa Women in Logistics Association (WILA), huku Mdahalo ukiratibiwa na Mhandisi Patrick Magai.
Miongoni mwa masuala yanayojadiliwa katika mdahalo huu unaoendelea ni pamoja na:
Kwanza, Ufanisi wa bandari na uendelevu wa uendeshaji wake
Changamoto za biashara na lojistiki katika bandari za Tanzania
Pili, Suluhisho za vitendo kupitia ushirikiano wa sekta ya umma na binafsi
Tatu, Urahisishaji wa biashara na maendeleo ya miundombinu.
Hata hivyo Baraza la Wasafirishaji Tanzania linaamini kuwa mdahalo huu utaongeza uelewa wa pamoja, kuimarisha ushirikiano kati ya sekta ya umma na binafsi, na kutoa mapendekezo yatakayochangia kuboresha uendeshaji wa bandari na kuchochea ukuaji wa biashara na uchumi wa taifa kwa ujumla.
Imetolewa na:
Baraza la Wasafirishaji Tanzania (TSC)
Kwa mawasiliano zaidi:
📞 0769 404 145
Josephine Elington
Katibu Mkuu – TSC