LIVE: Dakika 45 ITV na Maalim Seif

Mshume Kiyate

JF-Expert Member
Feb 27, 2011
6,766
894
Maalim Seif Sharif Ahmad, anaonge anaelezea habari za Zanzibar, na CUF, CCM, zilivyounda serikali ya umoja wa kitaifa
 
Anasema Tanzania kuna vyama 18 vya siasa lakini vyama viwili ndio vimepata nafasi ya kuunda serikali ya mseto kwa mujibu wa katiba
 
Namuona anafananisha muafaka wa Zanzibar kama muafaka wa Meya Arusha, anuliza jee, Chadema sasa siyo opposition tena kwa kufikia muafaka Arusha?
 
Anasema CDM wana hoja ya Msingi kupinga posho, pia polisi bara waache kutumia nguvu kwa raia pia wasifuate matakwa ya kisiasa
 
Maalin Seif akihojiwa katika kipindi cha 'Dakika 45' ITV amesema hoja ya CDM kuhusu posho za wabunge ni hoja ya nguvu. Ameifagilia. Anasema yeye yuko serikalini,inabidi ajiulize kazii yake ni nini. Kwa hiyo posho ya nini kwa kazi aifanyayo kisheria. Ameitaka serikali isiipuze hoja hiyo, vinginevyo serikali ije na hoja yenye nguvu kuliko ya CDM. Amesema wananchi wanataka kuona hoja za nguvu kama hiyo ya CDM.
 
Namuona anafananisha muafaka wa Zanzibar kama muafaka wa Meya Arusha, anuliza jee, Chadema sasa siyo opposition tena kwa kufikia muafaka Arusha?
hakuna muafaka Arusha madiwani wamerubuniwa wakauza kiti cha umeya, wanashughulikiwa!
 
Maalin Seif akihojiwa katika kipindi cha 'Dakika 45' ITV amesema hoja ya CDM kuhusu posho za wabunge ni hoja ya nguvu. Ameifagilia. Anasema yeye yuko serikalini,inabidi ajiulize kazii yake ni nini. Kwa hiyo posho ya nini kwa kazi aifanyayo kisheria. Ameitaka serikali isiipuze hoja hiyo, vinginevyo serikali ije na hoja yenye nguvu kuliko ya CDM. Amesema wananchi wanataka kuona hoja za nguvu kama hiyo ya CDM.
Hongera kwa hilo sharif..bora umesema vichwa ngumu kuelewa wa magamba watajiuliza kwanini amesema hivyo..Pinda, Shibuda na wote mliopinga posho mnasemaje?
 
Kaulizwa vipi ipo siku unaweza kusema sasa mimi basi Cuf narudisha kadi, Maalim akasema ni ndoto yeye kurudisha kadi ya Cuf..baada ya hapo akaleta jokes
 
huyo jamaa kwisha nguvu yake, sasaivi ni sehemu ya serikali hawezi tena kupingana na serikali ambayo yeye ni sehemu ya serikali hiyo...
 
anafaa kuwa rais wa jamhuri ya muungano ni mtu mkweli, msemakweli na ana penda umoja uliokuwa thabiti.
 
Maalin Seif akihojiwa katika kipindi cha 'Dakika 45' ITV amesema hoja ya CDM kuhusu posho za wabunge ni hoja ya nguvu. Ameifagilia. Anasema yeye yuko serikalini,inabidi ajiulize kazii yake ni nini. Kwa hiyo posho ya nini kwa kazi aifanyayo kisheria. Ameitaka serikali isiipuze hoja hiyo, vinginevyo serikali ije na hoja yenye nguvu kuliko ya CDM. Amesema wananchi wanataka kuona hoja za nguvu kama hiyo ya CDM.

Yani yuko kimya kama hayumo serikalini vile,,,,,, ama kweli huyu jamaa ni jembe linalolima juu ya jiwe ili apande mpunga....
 
Nilipata bahati ya kumsikiliza jana, anaonekana ni mtu aliyekata tamaa sana. Vile vile amechoka sana. Atakuwa ana msongo wa mawazo au matatizo yanayo msumbua sana huyu mzee!
 
Back
Top Bottom