Mkuu naamini kabisa unachokisema,very sad indeed!RPC aliona kwa macho yake akipigwa na polisi,na kama unavyojuwa,tayari walikuwa wamemkamata mwandishi mmoja,nadhani kwasababu walijuwa yeye ndo mwenyekiti wao,basi walijuwa lazima aende kujaribu kufahamu kulikoni akamatwe.Na polisi walipokuwa wakimpa kichapo,RPC anayemfahamu,akajidai hata hamfahamu,akayafumbia macho,sawa na pilato aliponawa mikono,wahunu wanaojiita polisi,wakammalizia pale pale.Mbele ya mchacho ya RPC na OCD,wakijuwa kuwa wanawafurahisha mabosi wao.Na kuna taarifa za waandishi waliokuwa wamejibanza kwenye kona,ambao walisikia polisi wakijigamba kuwa lazima wauwe siku hiyo,kumbe walijuwa kabisa ni nani wanakwenda kumwua?Then ccm bado wana balls za kusingizia amani tena?labda amani ina maana ya tofauti kwao.
Dude la ajabu ndo nini, jini au?. Polisi waache upumbavu wao, Mwangosi kauliwa na bomu la machozi alilolipuliwa nao na polisisiemu. Kuna mwananchi anayemiliki bomu la machozi?Subirin Postmoterm report kwanza nauhakika huyo mwandishi aliuliwa na dude fulan la ajabu sana lililorushwa na wafanya fujo toka mbeya!
3. Kwa matukio ya aina hii, tunadhani wakati mwafaka kwa uongozi wa Jeshi la Polisi nchini kuwajibika, kuazia kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa na uongozi wa Makao Mkuu, akiwamo Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Saidi Mwema.TAARIFA YA JUKWAA LA WAHARIRI (TEF)
KWA VYOBO VYA HABARI
KUHUSU KUUAWA KWA MWANDISHI DAUDI MWANGOSI
8. Kwa maana hiyo, mbali na uchunguzi ambao utafanywa na polisi, tunatoa wito kwa Serikali kuunda chombo huru, ambacho kitabaini ukweli, na matokeo yake yatangazwe kwa umma, huku wahusika wa aibu hiyo wakichukuliwa hatua za kisheria. Tunasema hivyo, tukifahamu kwamba tayari kuna jitihada za kuficha ukweli na kueneza propaganda za uongo kuhusu tukio zima.
IMETOLEWA NA:
NEVILLE MEENA,
KATIBU MKUU JUKWAA LA WAHARIRI TANZANIA (TEF)
SEPTEMBA 3, 2012
Dude la ajabu ndo nini, jini au?. Polisi waache upumbavu wao, Mwangosi kauliwa na bomu la machozi alilolipuliwa nao na polisisiemu. Kuna mwananchi anayemiliki bomu la machozi?
Kajubi anasema baraza linataka kuanza kutoa mafunzo ya kuchukua taarifa kta mazingira hatarishi kwa kuwa mikutano ya siasa imekuwa sehem hatari, pia ameshauri wahariri kuanza kurinda wandishi wao
Sima uhakika kama ni kweli Al-shabaab wanaweza kutumia mabomu ya machozi ktk shughuli zao za kigaidi, ili iweje? Unategemea polisi hao hao waliomuua mwandishi wa habari watoe report ambayo ni fair?. Nashukuru hakuna ndugu yangu wa karibu anaefanya kazi hii ya polisi, ni afadhali ya panzi hutumia akili yake kujifikirisha kuliko polisi anayeamrishwa kila kitu hata kikiwa kibaya.alishababu wanayo kibao kaka.....subiri report ya police utaona
Du! tulitegemea jeshi letu baada ya kuingia Said Mwema, IGP, msomi,na aliyefanya shughuli za kimataifa,lingekuwa la kisasa lakini mambo yalinayofanyika na jeshi la polisi na yanayoendelea yameonyesha mapungufu makubwa kwa Mwema.Tunaendelea kusikiliza Channel 10!
The most important thing to discuss should be the secrets behind the series of killings on opposition rallies. Someone (perhaps high ranking gov officials) who is/are quite should be questioned now. Police receives orders, who gives orders?
yule askari aliyemwekea bunduki tumboni alishapewa kazi ya kummaliza Mwangosi,haiwezekani askari afanye vile wakati boss wake RPC akijaribu kumwokoa,nimefurahi kwa sababu hawakujua wapiga picha wanachukua kila tukio,taarifa tulizo nazo zinasema baadhi ya askari hawatoki pale na wameandaliwa kutoka background mbovu kabisa walikotoka,kumbuka kuna ile picha ya mwisho askari amesimama akimshangaa Mwangosi wakati ameshakufa??yule kwa roho yake asingeweza kufanya vile,aliwekwa kwenye lile kundi bila kujua mipango nini kinaendelea,yule aliyempiga bomu ndiye alitumwa kwa kazi ile maalam,amini usiamini sio askari wote wanafurahia mambo yanayofanywa na jeshi hili dhalimu,Mwisho wa huyu MwemA utakuwa kama wa Bilal,yote haya tunayajua kwa kuwa tunaona mbali kuliko waanavyofikiri