LIVE : Channel Ten - Mauaji ya Daud Mwangosi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

LIVE : Channel Ten - Mauaji ya Daud Mwangosi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Baraka F.K, Sep 3, 2012.

 1. Baraka F.K

  Baraka F.K Member

  #1
  Sep 3, 2012
  Joined: Aug 28, 2012
  Messages: 79
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Jeneral Ulimwengu anaendesha kipindi cha Jeneral on Monday,
  Mada ni Mauaji ya Mwngosi - Nyororo
  Wachagiaji jaji Mihayo na mwenyekiti wa baraza la Waandishi wa habari
   
 2. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #2
  Sep 3, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,596
  Likes Received: 18,593
  Trophy Points: 280
  Wanabodi

  Wale wenye access, please watch kipindi cha Jenerali on Monday live on Channel Ten, wanazungunzia kifo cha Mwanahabari Daudi Mwangosi.

  Discusants ni Jaji Mstaafu Thomas Mihayo, Katibu wa MCT, Kajubi Mukajanga na bosi fulani wa polisi!.

  keep watching!.

  Pasco.
   
 3. Mwanaukweli

  Mwanaukweli JF-Expert Member

  #3
  Sep 3, 2012
  Joined: May 18, 2007
  Messages: 4,451
  Likes Received: 288
  Trophy Points: 180
  Mkuu wengine tuko mbali tunabeba maboksi. Tujulishe kadri mjadala unavyoendelea.
   
 4. s

  step Senior Member

  #4
  Sep 3, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 190
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  The most important thing to discuss should be the secrets behind the series of killings on opposition rallies. Someone (perhaps high ranking gov officials) who is/are quite should be questioned now. Police receives orders, who gives orders?
   
 5. lutayega

  lutayega JF-Expert Member

  #5
  Sep 3, 2012
  Joined: Feb 29, 2012
  Messages: 1,216
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Jaji mihayo ameulizwa km sheria zinaruhusu jesh la polis kushtakiwa, amesema inahusiwa na amewasii wanasheria wajitokeze kuisaidia familia kulishtaki jeshi la polisi
   
 6. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #6
  Sep 3, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,768
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  nafikiri kwa hapa tulipofikia ni bora jeshi hili lishtakiwe,maybe wanaweza kupunguza hasira za kutuua manake naona kabla ya 2015 tutaisha wote
   
 7. Maganga Mkweli

  Maganga Mkweli JF-Expert Member

  #7
  Sep 3, 2012
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 2,097
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  nawafuatialia kwa karibu sana kwa kweli wenye acess ya television tune channel ten ...
  jeshi la polisi ni tatizo ..
  hakuna kiongozi wakumuwajibisha IGP..?
  kwanini polisi wetu badala ya kutekeleza sheria ya kulinda amani na usalama waanze kwa kupiga wananchi ? -jaji mihayo
   
 8. lutayega

  lutayega JF-Expert Member

  #8
  Sep 3, 2012
  Joined: Feb 29, 2012
  Messages: 1,216
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Katibu mkuu wa baraza la habari anasema mauaji ya daud yalipangwa mapema kwa sababu daudi alimuliza rpc swali lililomkera na rpc alivyolijubu alisababisha baadhi ya waandishi kuacha kwenda kwenye mkutano wa cdm kwa kuhofia maisha yao
   
 9. Maganga Mkweli

  Maganga Mkweli JF-Expert Member

  #9
  Sep 3, 2012
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 2,097
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  polisi sasa hivi hawana aibu wanapiga waziwazi bila uficho... anasema ingekuwa kama vurugu za london za mwaka jana zingetokea tanzania kungekuwa na mauaji ya kutisha kwa upeo wa jeshi la polisi-jaji mihayo
   
 10. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #10
  Sep 3, 2012
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,594
  Likes Received: 1,974
  Trophy Points: 280
  Kama kuna mtu aliniamisha kuwa mauwaji ya mwandishi yule yalipangwa,basi ni wewe mkuu,nadhani ulisema mnafahamiana toka kitambo,na kama unavyojuwa,watu wenye msimamo hawapendwi kabisa na watawala.Je bado unadhani walipanga hii kitu?ni mambo gani ambayo yalikufanya useme kuwa ni mtu mwenye msimamo isiyoyumba?ebu tupe wasifu wake kidogo mkuu wangu.Kama kuna thread ya wasifu wake,basi ntakuja huko kuona inputs zako kuhusu mhanga huyu.Natanguliza shukran.
   
 11. lutayega

  lutayega JF-Expert Member

  #11
  Sep 3, 2012
  Joined: Feb 29, 2012
  Messages: 1,216
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Kajubi anasema baraza linataka kuanza kutoa mafunzo ya kuchukua taarifa kta mazingira hatarishi kwa kuwa mikutano ya siasa imekuwa sehem hatari, pia ameshauri wahariri kuanza kurinda wandishi wao
   
 12. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #12
  Sep 3, 2012
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,594
  Likes Received: 1,974
  Trophy Points: 280
  Mkuu ni kauli gani hiyo?maana kuna thread ambayo imeshafungwa,ambayo ilisema polisi wamepanga kufanya mauwaji huko Iringa,kweli haukupita muda,mauwaji yakatokea ya mwandishi ndugu Mwangosi.
   
 13. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #13
  Sep 3, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,768
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  Mkuu mushi namfaham sana Mwangosi,nimefanya naye kazi Tanesco miaka ya 90,kipindi kile alikuwa ni mtu mwenye misimamo asiyetetereka,kumbuka miezi mitatu au minne iliyopita waandishi wa habari wa Iringa waliandamana kuelekea kwa RPC kupeleka madai ya kusumbuliwa na polisi?issue ilanzia pale,naamini na najua Mwangosi ametafutiwa nafasi ya kuuliwa muda mrefu na wameipata,kwa kuwa hakuna siri hapa duniani tutajua kila kitu
   
 14. S

  Sobangeja Senior Member

  #14
  Sep 3, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 183
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Du! tulitegemea jeshi letu baada ya kuingia Said Mwema, IGP, msomi,na aliyefanya shughuli za kimataifa,lingekuwa la kisasa lakini mambo yalinayofanyika na jeshi la polisi na yanayoendelea yameonyesha mapungufu makubwa kwa Mwema.Tunaendelea kusikiliza Channel 10!
   
 15. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #15
  Sep 3, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,317
  Likes Received: 5,610
  Trophy Points: 280
  Hata mimi nilikuwa na imani kubwa sana kwa IGP Said Mwema,ila baada ya kutokota nimeshamtoa thamani kabisaaa!!hafai na jeshi limemshinda anawaachia wapuuzi walisemeeeee jeshi kina Chagonja (mpiga ramli) wa jeshi
   
 16. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #16
  Sep 3, 2012
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,594
  Likes Received: 1,974
  Trophy Points: 280
  Mkuu naamini kabisa unachokisema,very sad indeed!RPC aliona kwa macho yake akipigwa na polisi,na kama unavyojuwa,tayari walikuwa wamemkamata mwandishi mmoja,nadhani kwasababu walijuwa yeye ndo mwenyekiti wao,basi walijuwa lazima aende kujaribu kufahamu kulikoni akamatwe.Na polisi walipokuwa wakimpa kichapo,RPC anayemfahamu,akajidai hata hamfahamu,akayafumbia macho,sawa na pilato aliponawa mikono,wahuni hao wanaojiita polisi,wakammalizia pale pale.Mbele ya macho ya RPC na OCD,wakijuwa kuwa wanawafurahisha mabosi wao.Na kuna taarifa za waandishi waliokuwa wamejibanza kwenye kona,ambao walisikia polisi wakijigamba kuwa lazima wauwe siku hiyo,kumbe walijuwa kabisa ni nani wanakwenda kumwua?Then ccm bado wana balls za kusingizia amani tena?labda amani ina maana ya tofauti kwao.
   
 17. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #17
  Sep 3, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,596
  Likes Received: 18,593
  Trophy Points: 280
 18. princeamos

  princeamos Member

  #18
  Sep 3, 2012
  Joined: Feb 24, 2012
  Messages: 52
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [h=3][/h]
  [FONT=&quot]TAARIFA YA JUKWAA LA WAHARIRI (TEF) [/FONT]
  [FONT=&quot]KWA VYOBO VYA HABARI[/FONT]
  [FONT=&quot]KUHUSU KUUAWA KWA MWANDISHI DAUDI MWANGOSI[/FONT]

  [FONT=&quot]UTANGULIZI:[/FONT]
  [FONT=&quot]1. [/FONT][FONT=&quot] Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), limepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha mwandishi wa habari wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, mkoani Iringa, Daudi Mwangosi. [/FONT]


  [FONT=&quot]2. [/FONT][FONT=&quot] Mwangosi ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari mkoa wa Iringa (IPC), aliuawa akiwa kazini jana, Septemba 2, 2012, wakati polisi walipokuwa wakiwadhibiti wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).[/FONT]


  [FONT=&quot]3. [/FONT][FONT=&quot] Tukio hili linaiingiza Tanzania katika historia mbaya ya ukiukwaji na ukandamizwaji wa uhuru wa habari, kwani ni kwa mara ya kwanza tunashuhudia mwandishi wa habari AKIUAWA WAKATI AKITEKELEZA MAJUKUMU YAKE YA KIHABARI.[/FONT]


  [FONT=&quot]4. [/FONT][FONT=&quot] Taarifa za awali zinaonyesha kuwa Mwangosi kabla ya kufikwa na mauti saa 9.30 alasiri katika kijiji cha Nyololo, Mufindi, alizingirwa na kushambuliwa na polisi waliokuwa katika eneo la tukio. Na hata alipopiga kelele za kuomba msaada, hakusikilizwa na matokeo yake aliuawa na kitu kinachodhaniwa kuwa ni bomu.[/FONT]


  [FONT=&quot]5. [/FONT][FONT=&quot] Kwa kushirikiana na Baraza la Habari Tanzania, TEF tumechukua hatua za haraka za kuunda timu ya uchunguzi wa suala hilo, ambayo itakwenda mkoani Iringa mapema kadri itakavyowezekana, ili kubaini ukweli wa tukio hilo. Lengo la uchunguzi huo ni kuweka kumbukumbu sahihi (documentation) ya tukio hilo la aina yake katika historia ya nchi yetu.[/FONT]


  [FONT=&quot]6. [/FONT][FONT=&quot] Matokeo ya uchunguzi huo pamoja na mwingine unaofanywa na Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), ndiyo yatakayotoa mwelekeo wa hatua ambazo TEF inachukua dhidi ya Jeshi la Polisi katika siku chache zijazo. [/FONT]


  [FONT=&quot]MTIZAMO NA MSIMAMO WA TEF[/FONT]
  [FONT=&quot]Kwa kuzingatia taarifa kutoka Iringa na zile za vyombo vya habari vya jana (Jumapili, Septemba 02, 2012) na leo (Jumatatu, Septemba 03, 2012), TEF ina mtizamo na msimamo kama ifuatavyo:[/FONT]


  [FONT=&quot]1. [/FONT][FONT=&quot] Kwanza tunalaani vikali tukio la kupigwa, kisha kuuwawa kwa mwandishi Daudi Mwangosi ambalo limeigusa tasnia ya habari kwamba sasa pengine waandishi wa habari ni malengo “target ya polisi” wanapokuwa kwenye kazi zao.[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]2. [/FONT][FONT=&quot] Ieleweke wazi kwamba matukio haya siyo yanaondoa imani ya waandishi wa habari kwa jeshi la polisi tu, bali yanaweza kuwa chanzo cha uhasama na ufa mkubwa ambao utawanyima wananchi nafasi ya kutumikiwa na pande mbili ambazo zinategemeana.[/FONT]


  [FONT=&quot]3. [/FONT][FONT=&quot] Kwa matukio ya aina hii, tunadhani wakati mwafaka kwa uongozi wa Jeshi la Polisi nchini kuwajibika, kuazia kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa na uongozi wa Makao Mkuu, akiwamo Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Saidi Mwema.[/FONT]


  [FONT=&quot]4. [/FONT][FONT=&quot] Tunasema hivi kwani kuna kila dalili kwamba polisi wanahusika kwa namna moja au nyingine na tukio au/na matukio yaliyosababisha kifo cha Mwangosi, kwani kitendo cha kumzingira tu na kumshambulia kinathibitisha kwamba hawakuwa na nia njema hata kidogo dhidi ya mwandishi huyu.[/FONT]


  [FONT=&quot]5. [/FONT][FONT=&quot] Taarifa ambazo TEF tunazo, pia zinadai kwamba kulikuwa na mpango wa polisi wa “kuwashughulikia waandishi wa habari watatu” (Mwangosi) akiwa mmojawapo na hilo lilionekana likitekelezwa kwa polisi kumshambulia mwandishi huyo, baadaye alipoteza maisha katika mazingira ya kutatanisha.[/FONT]


  [FONT=&quot]6. [/FONT][FONT=&quot] Hili linatiliwa nguvu na tukio jingine la polisi kumpiga na kumjeruhi mwandishi mwingine, Godfrey Mushi ambaye ni mwakilishi wa gazeti la Nipashe mkoani Iringa. Mwandishi wa tatu ambaye hadi tunapoandika taarifa hiyo yumo katika mpango wa ‘kushughulikiwa na polisi’ ni Francis Godwin ambaye ni mwandishi wa habari wa kujitegemea.[/FONT]


  [FONT=&quot]7. [/FONT][FONT=&quot] Vitendo vya aina hii havivumiliki na havipaswi kuachwa kuendelea kwani ni hatari kwa ustawi wa demokrasia na uhuru wa habari nchini. Hatuwezi kuendelea katika mazingira ambayo polisi wanageuka kuwa chombo cha mauaji ya raia badala ya kuwa walinzi wa raia.[/FONT]


  [FONT=&quot]8. [/FONT][FONT=&quot] Kwa maana hiyo, mbali na uchunguzi ambao utafanywa na polisi, tunatoa wito kwa Serikali kuunda chombo huru, ambacho kitabaini ukweli, na matokeo yake yatangazwe kwa umma, huku wahusika wa aibu hiyo wakichukuliwa hatua za kisheria. Tunasema hivyo, tukifahamu kwamba tayari kuna jitihada za kuficha ukweli na kueneza propaganda za uongo kuhusu tukio zima.[/FONT]


  [FONT=&quot]9. [/FONT][FONT=&quot] Mwenendo wa aina hii wa chombo cha dola kuamua kutumia silaha kuua na baadaye kupanga mbinu chafu za kuficha ukweli ni hatari kwa Taifa, na unaiweka demokraisia ya nchi yetu njia panda, huku tukielekea katika hatari ya Taifa kutumbukia katika uovu.[/FONT]
  [FONT=&quot]IMETOLEWA NA:[/FONT]


  [FONT=&quot]NEVILLE MEENA,[/FONT]
  [FONT=&quot]KATIBU MKUU – JUKWAA LA WAHARIRI TANZANIA (TEF)[/FONT]
  [FONT=&quot]SEPTEMBA 3, 2012[/FONT]
   
 19. r

  raymg JF-Expert Member

  #19
  Sep 3, 2012
  Joined: Jun 30, 2012
  Messages: 845
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Subirin Postmoterm report kwanza nauhakika huyo mwandishi aliuliwa na dude fulan la ajabu sana lililorushwa na wafanya fujo toka mbeya!
   
 20. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #20
  Sep 3, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,641
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  'Sifa kuu ya kiongozi dhaifu ni kuwa katili (brutal), sifa ya kiongozi mwenye nguvu (powerful) si kuwa katili'. Ukiona kiongozi anatisha sana watu kwa vyombo vyake vya dola ujue ni kiongozi dhaifu. Anaogopa wananchi wakijua haki zao atakuwa hana cha kuwadanganya.
  Rip Mwangosi, leo wanakusafirisha kwenda kukuzika kwenu tukuyu.
   
Loading...