Litizamwe upya tatizo la ajira kwa vijana - R.I.P Justin Kalikawe!

MUSSA ALLAN

JF-Expert Member
Oct 13, 2013
18,925
13,259
JUSTIN KALIKAWE, Aliwahi kusema hivi:

Litizamwe upya tatizo la ajira kwa ajira kwa vijana, Kwani sasa limekuwa la muda mrefu na sasa limezua kasheshe kwenye jamii yetu, Kasheshe yenyewe ni Wamachinga, kuhangaika mitaani, kupambana na vyombo na vyombo vya dola. Laiti pembejeo za kilimo zingepatikana kirahisi kuna maeneo maeneo mengi na vijana tungefanya kilimo, Laiti Michezo ingepewa kipaumbele wako vijana shupavu ambao wangehimili vishindo!

Nani apendaye kuhangaika mchana mchana kutwa, kutembea maeneo yote ya mjini kutafuta riziki? Sababu ya msukumo wa maisha ya sasa?
NB: Hivi Majuzi hapa Arusha tulishuhudia Wamachinga wakivunjiwa vibanda vyao na manispaa ya jiji la Arusha.

Mh.Edward Lowassa aliwahi kusema kuwa VIJANA KUTOKUWA NA AJIRA NI BOMU LINALOSUBIRIWA KULIPUKA!

kalikawe_b.jpg
 
Kwani zile ajira 1m tulizoahidiwa na chama tawala wakati wanaingia madarakani zipi wapi? Leo hii Msalani unalalamika wakati wewe ndie muhusika?
 
Huna hata aibu kusema haya, umekuwa ukiropoka kila siku kutetea chama chako na serikali yako hapa tunapoikosoa, leo unasema hayo??
 
Kwani zile ajira 1m tulizoahidiwa na chama tawala wakati wanaingia madarakani zipi wapi? Leo hii Msalani unalalamika wakati wewe ndie muhusika?

Ndugu zitaonekanaje ajira 1m wakati ambao hawana ajira ni zaidi ya 1m?
 
Ajira ya bodaboda kwa vijana wa kiume,ajira inayoendelea kuchukua uhai vijana wetu kila siku,na ile ya kujiuza usiku kwa dada zetu ajira atarishi,imeshika kasi katika serekali hii ya awamu ya 4 kutokana na ugumu wa maisha kuzidi. upunda ajira inayochafua jina la nnchi yetu kimataifa.Nenda kariakoo kaone mgambo wa jiji na polisi jamii wanavyowapa tabu wamachinga ambao kama wakiamua kurudi mtaani tu kutokana na kero za hayo majeshi mawili yasiyo na elimu kamili ya kufanya kazina hawa machinga.wakichoka hawa vijana tegemeeni watoto wa mmbwa kuzidi mtaani
 
Tatizo la serikali wanajijali wao na familia zao. Wamekazania wawekezaji tu ambao nao wanawaleta raia wa nchini mwao kwaajili ya kazi ambazo mtanzania anaweza kufanya.
Kinachotakiwa kufanyanyika na kama serikali ina nia thabiti ya kupunguza wimbi la ukosefu wa ajira. Wafufue viwanda walivyovizika, kuanzia mashuleni waanze kufundisha elimu ya ujasiriamali.

Kujifunza nchi zilizoweza kumaliza ama angalau kupunguza tatizo la ajira, pia hata ajira zilizopo kusiwe na urasimu wa kupatikana. Tugeukie hata kilimo tuachane na propaganda ya kilimo kwanza ambayo mpaka sasa hakuna kinachoendelea.
Mwisho waache siasa kuingiza kwenye mambo muhimu kama ajira na vingine.
 
Tatizo mnakosoa bila kutoa njia mbadala!

Kama CCM wanataka njia mbadala waondoke madarakani waoneshwe, wasing'ang'anie madarakani kwa msaada wa polisi na wasimamizi wauchaguzi. Chama kingine kikija kitawaonesha jinsi ya kukabiliana na tatizo la ajira.
 
Kwani zile ajira 1m tulizoahidiwa na chama tawala wakati wanaingia madarakani zipi wapi? Leo hii Msalani unalalamika wakati wewe ndie muhusika?

Katika kutekeleza ilani ya uchaguzi serikali imevuka lengo lake la kutoa ajira 1m kwa vijana na kufikia ajira kwa vijana 3m walio ajiliwa na viwanda vya kure use plastiki na ukipita kila mtaa kila mji utawaona vijana hao wakiokota chupa za maji na makopo mengine ya plastick sisi sio mimi Oyeeeeeeeee
 
Duuuu kama ajira ndio hizo za kuwafanya watoto wetu fagio la mitaa basi hizo afadhali wakawape watoto wao hao kina MSALANI
 
Ajira za ccm hizo ni aibu tupu,usisahau zile za yule mmbunge alotuambia tuchangamkie za kule uarabuni kwenda kufanya kazi za ndani
 
Duuuu kama ajira ndio hizo za kuwafanya watoto wetu fagio la mitaa basi hizo afadhali wakawape watoto wao hao kina MSALANI

Ngudu yangu mnyonge atabaki kuwa mnyonge tu watoto wao nenda kaulize majina ya wafanyakazi wa BoT utagundua kuwa kumbe taasisi kubwa na zenye maslahi makubwa ni kwa ajili ya vigogo tu sisi watoto wetu wataishia kuokota chupa kama machizi kumbe wanaisaka pesa.
 
Ni kweli si umesikia jana mtoto wa mkulu wa inchi hii kapitishwa agombee ubunge pale bwagamoyo? Maji yanafuata mkondo mzee.ila habari ya ajira wasiendelee kutudanganya eti oo ajira 1m, ziko wapi? Za kuokota chupa za maji mitaani?
 
Mwanafalsafa mmoja alisema "ni rahisi kumdanganya binadamu mara nyingi lakini ni vigumu kumdanganya siku zote dawa iko jikoni inachemka watainywa 2015 hapo ndipo watakapojua kuwa uongo ni mipango ya shetani.
 
Qualifier hata hiyo 2015 kama mtindo wenyewe ndio huu wa kukataa kuboresha daftari la wapiga kura, husitegemee changes zozote kwani wanajua kuwa wakiboresha hilo daftari watu wengi watajiandikisha hasa vijana ambao ndio sumu ya watawala.Jambo ambalo litawang'oa madarakani.wanalijua hasa!!!
 
Back
Top Bottom