SIKU YA VIJANA 2022: Rais Samia na suala la Ajira kwa Vijana

kevylameck

Member
Nov 3, 2013
18
19
183B9344-40FC-4082-96A9-5213A673C539.jpeg

Na Kevin Lameck


Siku ya Kimataifa ya Vijana inaadhimishwa leo na kila mwaka tarehe 12 Agosti, ikileta maswala ya vijana kwa jamii ya kimataifa na kusherehekea uwezo wa vijana kama washirika katika jamii ya leo.

Vijana ni kundi muhimu katika taifa lolote lile duniani. Hii ni kutokana na ukweli kuwa takwimu zinaeleza wazi wingi wa vijana ulivyo mkubwa hasa katika bara la Afrika.

Nchini Tanzania kulingana na Sensa ya mwaka 2012. Katika kila watu Kumi nchini, wanne ni vijana ambao wana umri kati ya miaka 15-34- Makadirio ni kuwa Vijana wanafikia milioni 21 nchini Tanzania.

Mbali ya takwimu hizo vijana ni nguvu kazi ya Taifa, ni walinzi wa Taifa, ni wabunifu, wana uthubutu, ni wajasiri na ndiyo waliobeba maono na matarajio ya Taifa.

Mara zote Uhai, Usalama, Maendeleo na ustawi wa Taifa lolote lile duniani unategemea vijana na hakuna Taifa linaloweza kwenda mbele bila ya nguvu na utashi wa Vijana.

Mbali ya sifa hizo, Zipo changamoto nyingi ambazo zimekuwa kikwazo kwa vijana wa Kitanzania. Kubwa la kukumbuka leo ni kwamba tayari zipo hatua zinazochukuliwa na Serikali ya Rais Wetu Mama Samia Suluhu Hassan.

Changamoto kubwa zaidi ni Tatizo La Ajira Nchini; Hili ni tatizo la dunia nzima kwa vijana na wastani unasema asilimia 11.4 ya vijana wenye uwezo wa kufanya kazi hawana ajira.

Serikali yetu imeendelea kuchukua hatua mbalimbali kupambana na hali hiyo ikiwemo kuendelea kuajiri vijana serikalini ikiwa kama muajiri Mkuu na nambari moja nchini.

Serikali pia inatengeneza fursa za ajira kupitia utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati ambayo inatoa ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja.

Miongoni mwa miradi hiyo ni ujenzi wa reli ya kisasa, bwawa la umeme, barabara, madaraja, ukarabati na ujenzi wa meli mpya, upanuzi wa viwanja vya ndege na mradi wa bomba la mafuta.

Njia nyingine muhimu inayotumika na serikali ya Rais Samia ni pamoja na kutengeneza mazingira mazuri ya kukuza sekta binafsi ili kujenga viwanda na kuwekeza sehemu mbalimbali na kutoa ajira kwa vijana.

Serikali inatengeneza mazingira pia ya vijana kujiajiri wenyewe kwa kufuta tozo kwenye kilimo na kuweka Ruzuku za mabilioni kwenye sekta ya kilimo na ufugaji.

Serikali ya Rais Samia imerahisisha pia taratibu za biashara ikiwamo kutoa leseni kwa njia ya mtandao na kufuta tozo na kodi za kero kama OSHA, Zimamoto Nk.

Serikali ya Rais Samia pia imefuta tozo na kodi mbalimbali kwenye madini na kutenga maeneo ya wachimbaji wadogo yenye ukubwa wa zakdi ha hekta 38,567.

Serikali pia imeboresha mazingira na kuongeza fursa za ajira kwenye sekta ya utalii, ambapo kumeanzishwa hifadhi tano mpya na kununua ndege kubwa zaidi ya 11.

Serikali ya Rais Samia pia imepunguza ada ya leseni ya biashara ya utalii kwa wakala wa kusafirisha watalii yenye idadi ya magari chini ya manne kutoka dola za Marekani 2,000 hadi Dola 500.

Serikali ya Rais Samia pia imewekeza kiasi kikubwa kwenye Mkongo wa Taifa na kujenga kituo cha kisasa cha kutunza Taarifa (Dara Center). Hii ni fursa kwa vijana wa Kitanzania kunufaika na uchumi wa kimtandao kupata ajira.

Eneo jingine ambalo kazi kubwa imefanywa na Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan ni katika michezo, sanaa na utamaduni, muziki pamoja na filamu.

Miongoni mwa hatua zilizochukuliwa ni kuimarisha sekta hii ili iendelee kutengeneza ajira ikiwa ni pamoja na kuimarisha usimamizi wa hatimiliki na ulipwaji wa mirabaha kutokana na kutumiwa kwa kazi za sanaa ya muziki.

Rais Samia pia ameanzisha mfuko wa maendeleo ya michezo ili kusaidia maandalizi ya timu zetu za Taifa, kufuta VAT kwenye nyasi bandia na maboresho ya viwanja vinavyotumika kwenye michezo.

Serikali ya Rais Samia imetoa bure mashamba makubwa kwa vijana, Pembejeo za kilimo pamoja na Mikopo ili kuhamasisha vijana kujiingiza kwenye kilimo wapate kujiajiri na kujiingizia kipato chao.

Serikali ya Rais Samia pia imefanikisha kurejesha mahusiano ya kidiplomasia na nchi marafiki, suala ambalo limechangia kuongeza masoko ya bidhaa za kilimo na ufugaji kutoka nchini Tanzania.


Kazi Iendelee....
 
Ajira bila mifumo imara ni Bure.

RASIMU alosimamia Judge WARIOBA irudi mezani mjadala uanzie hapo.

Tuanzie ilipoishia Rasimu ya Judge Warioba kabla haijawa KATIBA PENDEKEZWA.

Mzee wetu AAPISHWE Ili akamilishe KAZI aliyoianza.

Mnyika endelea na HARAKATI wakati maridhiano yakiendelea.

Ameeeen
 
Back
Top Bottom