Albedo
JF-Expert Member
- Feb 24, 2008
- 5,559
- 1,452
Tukiwa tumebakiza mwaka mmoja kabla kufanyika kwa Uchaguzi mkuu wa
Wabunge, Rais na Madiwani, joto la kisiasa linazidi kupanda katika nchi yetu, katika kipindi cha Miaka Minne kumekuwa na Mapambano makali dhidi ya Ufisadi( Wizi) na Mafisadi ( Wezi) wa rasilimali katika nchi yetu, sote tutakumbuka viti hii ilipata kasi pale Mwembechai pale Dr. Slaa na Wapambanaji wengine walipotoa kile walichokiita list of Shame, ni tukio ambalo kwa kweli liliweza kuwapatia wapinzani hasa CHADEMA attention kubwa miongoni mwa wapiga kura wa nchi hii ( Tumeshuhudia impact yake katika chaguzi ndogo zilizofuatia). Baada ya tukio lile tumeshuhudia watu mbali mbali wametokea na kujipambanua kama wapinga Ufisadi na Mafisadi katika nchi hii, kundi moja wapo ni lile Linalojiita Wapiganaji ambalo linaundwa na wabunge 11 wa chama cha Mapinduzi.
Katika kutafakari juu ya Vita hii nimekuwa najiuliza maswali kadhaa
1: Itakuwaje kama CCM watawatumia hawa Wapiganaji katika Kampeni zao za mwaka 2010 katika kuhakikisha kwamba Waanzilishi wa Mapambano haya akina Slaa, Zitto na wengine hawarejei Bungeni? Je Mnafikiri hili jambo haliwezi kutokea? Na Kama hili lkitokea, je Wapinzani wana mkakati wowote ku counter kishindo cha Wapiganaji kama wataamua kuzunguka nchi nzima kuiuza CCM?
2: Je ikitokea kwamba Wapambanaji akina Dr. Slaa, Zitto na wengine wakingolewa na Wapiganaji pamoja na wanaotwa Mafisadi wakirudi Bungeni, je nini itakuwa hatma ya Vita dhidi ya Ufisadi katika Serikali ya 2010/15?
Im traying to think Loudly ila nadhani nimesikika!