Jamani mke wangu haniamini kabsaaa. Nikienda ofisini nikachelewa kurudi anaamini nilikuwa kwa mademu. Nikichelewa ananifanyia suprise anakuja office bila taarifa ananikuta tena peke yangu, lakini bado haniamini. Hali hiyo imedumu kwa miaka mingi sana mpaka naona nimefika mwisho siwezi ivumilia. Issue inaanzania mbali kidogo, wakati bado sijamuoa aliwahi kunikuta na daftari la mshikaji wangu ambaye miandiko yetu inafanana. Hilo daftari jamaa alikuwa kaorodhesha mademu wote aliotembea nao. Sasa kulikuwa na column tatu NAMBA, JINA, na HALI. kwa mfano: NAMBA 1, JINA: Jenifa Kalalu, HALI: tight. Sasa idadi ilikuwa inafika 94 mpaka wakati huo. Wife anaamini list ilikuwa yangu, na kwenye list hiyo kulikuwa na majina ya watu wa karibu yake. Kila tukigombana ananitusi kuwa mie malaya sana na anauliza kuwa list yangu wamefika wangapi. Sasa mi naumia sana!! Ishu ya miaka kama 10 iliyopita halafu sio daftari langu lakini anafanya ndio reference kila tunapokwaruzana. Sasa sijui hata nimfanyeje??