General Mangi
JF-Expert Member
- Dec 21, 2013
- 15,301
- 23,024
Anaandika Tundu Lissu katika ukurasa wake wa Instagram:-
Naona Waziri Mkuu Majaliwa anazindua Kituo cha Afya kilichojengwa kwa ufadhili wa Acacia Mining Ltd. .
Mwaka jana tuliambiwa na Rais Magufuli kwamba Acacia walikuwa wezi, wanaendesha Migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi bila leseni, hawajasajiliwa na BRELA na wamekwepa kodi ya TAS trilioni 495, n.k. Leo Waziri Mkuu anafungua Kituo cha Afya kilichojengwa na Acacia. .
Nilisema bungeni mwaka jana kwamba Magufuli na watu wake wanatudanganya; kuwa Ripoti za Maprofesa Mruma na Osoro ni 'professorial rubbish', kwamba hawa wachimba dhahabu hawatatulipa chochote tunachoambiwa tunawadai. .
Leo nani anayeweza kusema hatukudanganywa na Magufuli. Badala ya trilioni 495 ni Kituo cha Afya. Na Magufuli atuambie makinikia yaliyokuwa yanashikiliwa bandarini kwa amri yake yako wapi na kama yamelipiwa ushuru aliosema tutalipwa!!!