Siku za hivi karibuni kumekuwa na wimbi kubwa la wanachama wa UKAWA kuvihama vyama vyao na kuhamia CCM, huku baadhi yao waki-sacrifice nafasi zao za uongozi ndani ya vyama hivyo au kupitia vyama hivyo, nafasi ambazo kwa kweli wametumia nguvu kubwa sana kuzipata; na zikiwa zinawapa maslahi mazuri kabisa.
Kama kawaida yao wana-UKAWA wamekuwa wakimnyoshea kidole jirani, kwamba ndiye anayehusika na hama hama hiyo. Wamekuwa wagumu sana kuyaona matatizo yao ya ndani na hasa kutoka kwa viongozi waandamizi wa vyama vyao, na cha ajabu sana kila aliyeongea lolote la kuwakosoa viongozi hao ameonekana ni mtu asiye na akili na hivyo kuambulia matusi ya ajabu ajabu.
Napenda kutoa wito kwa wana-UKAWA wote kujitathmini kwanza ndani kabla ya kumnyoshea kidole jirani. Hao wanaohama ni watu wenye akili zao timamu; wanajua gharama ya maamuzi yao. Wanajua ni nini watakikosa kwa kuchukua maamuzi hayo magumu. Acheni kujidanganya kwamba mnaongozwa na Miungu Watu, wasiokosea, wasiokuwa na tamaa za mali, wazalendo wa kweli; na badala yake wafanyieni tathmini viongozi wenu na hasa kwa kujiuliza ni wapi wanakotaka kuwapeleka. Kinyume na hapo tutarajie UKAWA kumomonyoka zaidi, na uchaguzi wa 2020, umoja huo utakuwa hoi kabisa.