Chagu wa Malunde
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 8,708
- 5,711
Wakati wa kampeni alipokuwa Ikungi district, nyumbani kwao na aliyekuwa mgombea wa CHADEMA Rais Magufuli alitamka maneno ya msingi sana ambayo yalionyesha nia yake ya kutaka maridhiano na Wapinzani.
Rais Magufuli alitamka kwa upendo kabisa kuwa Lissu kama kijana ambaye amezaliwa Ikungi asipoteze muda kugombea Urais, sababu hawezi kushinda na hivyo sababu yeye ana mamlaka ya kuwapa watu kazi za kufanya kama mkuu wa Nchi, alisema atampatia Lissu kazi ya kufanya.
Lakini cha kushangaza Lissu alijibu mapigo kwa dharau na kebehi kubwa kuwa yeye hayuko tayari kupewa kazi na Rais Magufuli kwa kuwa yeye sio wa majalalani. Maneno haya yalitamkwa na ndugu Lissu huku akitunisha kifua na mbwembwe nyingi.
Jambo la kushangaza ni hivi majuzi Lissu akihojiwa na VOA nimemsikia akiongea kwa unyenyekevu kuwa anamshauri Mh Rais Magufuli afanye maridhiano na wapinzani. Swali la kujiuliza, je Lissu hakutambua kuwa Rais alimposema atampa kazi ilikuwa ndio hatua ya awali ya maridhiano yenyewe?
Kumbuka kuwa Lissu alizunguka nchi za Ulaya na Marekani akitoa maneno makali na ya kashfa dhidi ya Rais Magufuli na serikali yake. Lakini Rais alimezea na kuahidi kumpa kazi.
Sasa hayo maridhiano anayoyataka akiwa Brusele huku, aliondoka kwa mkwara kuwa anaenda kuendeleza mapambano huko ughaibuni ni maridhiano gani?