Lissu, the grace period is over. Unataka maridhiano ya nini?

Chagu wa Malunde

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
8,708
5,711
Wakati wa kampeni alipokuwa Ikungi district, nyumbani kwao na aliyekuwa mgombea wa CHADEMA Rais Magufuli alitamka maneno ya msingi sana ambayo yalionyesha nia yake ya kutaka maridhiano na Wapinzani.

Rais Magufuli alitamka kwa upendo kabisa kuwa Lissu kama kijana ambaye amezaliwa Ikungi asipoteze muda kugombea Urais, sababu hawezi kushinda na hivyo sababu yeye ana mamlaka ya kuwapa watu kazi za kufanya kama mkuu wa Nchi, alisema atampatia Lissu kazi ya kufanya.

Lakini cha kushangaza Lissu alijibu mapigo kwa dharau na kebehi kubwa kuwa yeye hayuko tayari kupewa kazi na Rais Magufuli kwa kuwa yeye sio wa majalalani. Maneno haya yalitamkwa na ndugu Lissu huku akitunisha kifua na mbwembwe nyingi.

Jambo la kushangaza ni hivi majuzi Lissu akihojiwa na VOA nimemsikia akiongea kwa unyenyekevu kuwa anamshauri Mh Rais Magufuli afanye maridhiano na wapinzani. Swali la kujiuliza, je Lissu hakutambua kuwa Rais alimposema atampa kazi ilikuwa ndio hatua ya awali ya maridhiano yenyewe?

Kumbuka kuwa Lissu alizunguka nchi za Ulaya na Marekani akitoa maneno makali na ya kashfa dhidi ya Rais Magufuli na serikali yake. Lakini Rais alimezea na kuahidi kumpa kazi.

Sasa hayo maridhiano anayoyataka akiwa Brusele huku, aliondoka kwa mkwara kuwa anaenda kuendeleza mapambano huko ughaibuni ni maridhiano gani?
 
Maridhiano maana nyingine ni makubaliano na (siyo kuomba kazi)
Mfano yaweza kuwa maridhiano ya kurudia Uchanguzi au kufanya Serikali ya mseto nk

Alijibu kwa upole na siyo unyenyekevu,ulitaka amtukane?
Akitukana mtasema hana uzalendo.
Ukweni ukiwa CCM lazima uwe punguani.
Ivi mna mapepo huko,kila anayejiunga nanyi mapepo yanamuingia na kumpunguza akili?
 
NI NGUMU SANA DIE HARD KUELEWA.WEWE NI MMOJA WAO.

Lissu kukataa kazi si ajabu kwani kimtazamo na haiba hao wawili hawaendani.Ni kama mbingu na nchi. Pia haina maana kuwa Lissu anaomba kazi wala fadhila. Anachotaka ni kuunganisha nchi iliyopasuliwa vipande.Wapenda haki na demokrasia kule na waroho wa madaraka na vurugu huku. CCM ni kundi la pili.

Watu kutochukua hatua dhidi ya uhuni si kuwa hawana namna.Ni busara na subira tu ndiyo inazuia machafuko.Wale wasio na tunu hizo wamesha anza yao(kuchomwa nyumba na visa vingine vya namna hiyo ni ishara). Wenye kutumia akili zao wanajua ninacho maanisha ila wenye kutumia "masaburi" itawachukua muda hadi watakapoanza kutokwa damu masikioni kama kenge.
 
Natamani nimwambie mzee tubatilishe uraia wake Lissu. Kwa sababu zipo njia nyingi za kutatua madai yake.

Lakini anaenda kupiga umbea ambao matokeo yake yanaweza kuwaathiri hata hao wanaojiita wafuasi wake.

Kwa sababu Kama ni kupungua kwa fedha za miradi kwa nchi za umoja wa ulaya hapa kwetu na ufinyu wa bajeti yetu utatuathiri wote.

Kama vipi apige umbea alafu aje.
 
Sasa maridhiano ya nini? Mbona hali ni shwari tu.mbona kama mnalazimisha nchi kuwa kama ina tatizo ..wakati hakuna!.sasa hayo maridhiano angeomba akiwa yupo huku Tanzania,ameondoka kwenda kuongelea maridhiano huko ulaya...
 
Magufuli mnamuona kama Mungu. Yani akili yako inafikiri Lissu hawezi ishi bila mshahara wa Magufuli. Leo hii Lissu akisema tuwe tunampa mshahara kila mwezi kwa michango anaweza pata pesa mara 20 ya mshahara wa Magufuli kila mwezi.
 
Hiyo kazi aliyoahidiwa na Magufuli

Atakuwa anaikumbuka kwa mbalii...
We unakuja kuwadanganya wananchi unawaambia reli,ndege hazina maana..lazima watakunyima kura tu.
Chama kimoja kimeongoza miaka 59 lakini hoja zake kwenye kuomba kura ni elimu, afya na maji? What a shame! Sasa kama ndege na reli zimesaidia mbona ajira zimezidi kuwa ngumu na wakati miradi ndo kama hiyo? Au pato dogo?
 
Tunawapa somo vijana waliokuwa wanapoteza muda kumshabikia wajue kuwa hawajitambui
Nafuu hao vijana wanajitambua kuliko wewe, kuwa wanasimamia wanaachokiamini. Wewe umekalia kulamba viatu vya DIKTETA kwenye post zako zote .​


20201106_094220.jpg
 
25 Reactions
Reply
Back
Top Bottom