Lissu: Si mara ya kwanza tunaahidiwa kuwekewa mikataba wazi. Kumuunga mkono Rais si lazima

Sawa, kama ni hivyo basi, uwasilishaji si mzuri. Maana alipaswa kuanza kuunga mkono kwamba sasa Mzee umeanza, safi, lakini ongeza na mikataba mingine, shughulikia na hawa nk.
Mbona rais yeye naye hataki kukubali kuwa kuna errors za kimaamuzi ila yeye anataka kuungwa tu mkono...nafikiri pia hawa ni watani wa jadi, waamini wa vyama viwili tofauti ambao kukubaliana itakuwa mshikemshike sana!!!
 
Mbona rais yeye naye hataki kukubali kuwa kuna errors za kimaamuzi ila yeye anataka kuungwa tu mkono...nafikiri pia hawa ni watani wa jadi, waamini wa vyama viwili tofauti ambao kukubaliana itakuwa mshikemshike sana!!!
Rais ni sawa na baba yako mzazi, huwezi kushindwa Ku support kwa jambo zuri analofanya kwa familia yake eti mpaka akiri madhaifu yake.
 
Lisu the only Tanzanian anayeweza kudadavua kwa data na evidence za kufa MTU. Nakuadmire sana. Mtanzania pekee awezae kukosoa mkuu was kaya
 
Tundu lisu huwa namwaelewa nasa anaongea kwa kitu ushahidi. Long life TL
 
Kwa hiyo anatakaje huyo lisu anataka je kweli rushwa Leo lissu anamtetea mkapa na kikwete si walisema legelege anataka magu aache au lissu anamajivuno sana ndo maana jana mvuto
 
The pillock is walking on sound bites!

Ninachosoma ni hoja zilizojaa jazba , kejeli na masuala ambayo kwa sasa ni dead letter.

Mkubali tu kuwa ajenda ya uzalendo mliuza siku ambayo mlimpokea yule mlituambia ni fisadi papa na genge lake.

Mzalendo gani anayetuambia kwa miaka minane kuwa fulani ni fisadi na anashangaa kwa nini anapewa fomu za kugombea Urais halafu baada ya huyo fisadi kukatwa, yeye ndie anamchukua na kumfanya mgombea Uraia.

Pesa zikiwekwa mezani uzalendo wake unakuwa historia.

Mzalendo Lissu wa sasa hawezi hata kudiriki kuwataja mawaziri wakuu waliokuwepo wakati wa utawala wa marais Mkapa na Kikwete. Chezea pesa wewe!

Naona Lissu anakomaa eti serikali ikajiondoe kwenye MIGA na BITs. Huu ni ushauri wa kijinga. Unataka mipango ya uwekezaji/wawekezaji nchini isifanikiwe. Serikali imesema haijiondoi kwenye MIGA na BITs kwa sababu ya kampuni moja.

Suala la ushauri wake kuhusu MIGA and BITs niliwahi kulielezea hapa;

GONGA LINK>>Ushauri wa Tundu Lissu kwa serikali niwa kijinga na serikali itakuwa ya kijinga kuukubali

Hii dhana ya kusema ''mimi nilipigania sana hizi sheria zifutwe'' ni unafiki fulani kwa maslahi na mtaji wa kisiasa. Kwa hiyo kama alipigania ndio wengine wasipiganie?

Kwa wakiristo wanafahamu hata Sauli (Paulo) aliyekuwa falisayo kwenye biblia alishangaza hata mitume wa Yesu achilia mbali wayahudi wengine kwa sababu ya kuanza kutenda mambo ambayo kabla yake alikuwa anawaua wale waliokuwa wanayatenda. Kwa leo hii ni mmoja wa mitume wa Yesu waliofanya kazi kubwa ya kueneza neno la Mungu (Matendo Ya Mitume 8:1-14)

Rais Magufuli kuanza kushughulikia kikamilifu sekta ya malighafi haina tofauti na alichokifanya Sauli (Paulo) huku akiwashangaza CCM na wapinzani.
Mmmh! Kweli watanzania hawana chao.
Inatia hasira sana, inasikitisha sanaa
Siku watanzania wakiamua ndio utakua mwanzo wa mabadiliko nchanya.
 
Naamini katika msuguano huu ndio suluhisho na maendeleo yatapatikana hata nchi zilizoendelea walipitia katika haya hivyo lissu endeleo kuisimamia serikali na serikali iwe ya utendaji na waache ya awamu zilizopita tulikosea sana

Sent from my TECNO-J5 using JamiiForums mobile app
 
Kweli kabisa mnatuchanganya
Yaan shida niliyoiona ni kwamba mtu ukiitwa mpinzan bac unapinga kila kitu, hii ni aibu jaman kwahiyo kwa maelezo yakd alitaka kika raisi aendelee kulifumbia macho suala hili?

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
Lissu ana ufahamu wa hali ya juu na ni mzalendo sio mpiga makofi kama wale ndugu zangu wasaka tonge mjengoni
 
oooh magu anayetaka kusifiwa tuuu nakujiona st
matendo anayofanyia wenzake ni yakishetani ngoja Israel amshukie siku moja atajuta
 
Yanayohojiwa na Lissu ndio iliyo mipango ya sasa ya Mheshimiwa wetu, Namshauri tuu avute subra tuone muda utatuambia, makofi na vigelegele siku zote hupingwa mwisho wa ngoma, sina tabia ya kumshabikia mwanasiasa lakini huyu anaongea toka moyoni, hawa wengine walioko madarakani hawana msimamo, mara leo hivi kesho vile.

Sent from my SM-G360H using JamiiForums mobile app
 
For the Record: What Goes Around Comes Around!!!

Leo wapinzani wa Serikali ya Magufuli tumesemwa sana na kutishiwa kushughulikiwa bungeni na nje ya Bunge.

Kwa sababu hiyo, naomba niweke rekodi ya masuala haya sawa sawa.

Mwezi Machi '97 Bunge lilipitisha Sheria 2 kwa siku moja kwa kutumia Hati ya Dharura.

1) Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbali mbali za Fedha ya '97 ilifuta au kupunguza kodi nyingi kwa ajili ya makampuni ya kigeni ya madini.

2) Sheria ya Uwekezaji Tanzania '97 iliwapa wawekezaji wa kigeni ulinzi mkubwa na manufaa mengi kama vile kuondosha nje fedha na faida yote wanayopata kwa uwekezaji wao nchini.

Mwaka '98 Bunge lilipitisha Sheria ya Madini '98 ambayo ilitamka kwamba mwenye milki ya madini na fedha yote itokanayo na mauzo ya madini ni mwenye leseni ya kuchimba madini hayo.

Sheria hizo tatu nimeziita 'Utatu Usio Mtakatifu' (Unholy Trinity) katika maandiko yangu mbali mbali, na nimezichambua sana tangu mwaka '99 nilipoanza harakati dhidi ya sekta ya madini ya aina hii.

Kwa miaka yote hii hadi leo, Sheria hizi za madini zimeungwa mkono na kupigiwa debe na kila kiongozi na mbunge wa CCM, Magufuli included.

Watu hawa, with very few and minor exceptions, ndio wamekuwa washangiliaji wakubwa wa unyonyaji wa makampuni ya kigeni ya madini katika nchi yetu.

Na ukweli ni kwamba watu hawa na Chama chao ndio wamefaidika sana na utaratibu huu katika sekta ya madini.

Wachache tuliopinga utaratibu huu tuliitwa kila aina ya majina mabaya na uzalendo wetu ulihojiwa kama unavyohojiwa leo na Magufuli.

Kwa mfano, Rais Mkapa alidai, wakati anazindua Mgodi wa Bulyanhulu, kwamba upinzani wetu ulikuwa ni 'ujinga uliofichama katika kivuli cha taaluma.'

Baadhi yetu, kama mimi na Dr. Rugemeleza Nshala, tulikamatwa na kushitakiwa mahakamani kwa uchochezi. Tulikabiliwa na kesi hiyo kuanzia Mei '01 hadi '08 ilipofutwa kwa kukosekana ushahidi.

Kama ilivyokuwa wakati wa Mkapa mwaka '01, leo pia Rais Magufuli ametukebehi na kuahidi kutushughulikia 'tukiropoka' nje ya Bunge.

Tunaambiwa ni lazima tumuunge mkono Rais wetu katika hii 'vita ya uchumi.' Ni sheria ipi ya Tanzania inayotulazimu kumuunga mkono Rais wetu hata kama tunaona amekosea???

Hebu naomba tuitafakari hii 'vita ya uchumi' kidogo. Je, nani hasa ni maadui zetu katika 'vita' hii??? Ni makampuni ya madini ya kigeni??? Kama ni hivyo, fikiria yafuatayo:

1) Wakati tuko vitani, Rais Magufuli na serikali yake wameiruhusu Acacia Mining (tunayoambiwa hata haijasajiliwa!!!) kuendelea kuchimba, kusafisha na kusafirisha nje ya nchi dhahabu kutoka Bulyanhulu, Buzwagi na North Mara Tarime.

Amezuia magwangala yasisafirishwe nje kwenye makontena lakini dhahabu yenyewe hamna shida ikisafirishwa na wezi hawa!!!!!

2) Wakati mapambano ya 'vita ya uchumi' yakiendelea, dhahabu yote inayochimbwa Geita Gold Mine (Mgodi mkubwa kuliko yote nchini) inaendelea kuchimbwa, kusafishwa na kusafirishwa nje ya nchi.

3) Wakati tuko vitani, Rais Magufuli na serikali yake ameruhusu kila mgodi wa dhahabu nchini kuwa na kiwanja chake binafsi cha ndege ili wezi hawa waweze kutorosha 'dhahabu yetu' kwa urahisi zaidi.

4) Wakati tungali vitani, 'Utatu Usio Mtakatifu' wa sheria zetu za kodi, uwekezaji na madini uko pale pale ulipokuwa mwaka '97-'98, cosmetic changes excepted.

Aidha, licha ya kuwa vitani, sisi bado ni signatories wa MIGA Convention na bilateral investment treaties (BITs) zinazowalinda hawa tunaoaminishwa kuwa ni wezi na maswahiba wao wa miaka yote.

5) Wakati tuko kwenye hii vita kubwa ya uchumi, jemedari wetu mkuu na serikali yake hawajatengua mkataba hata mmoja wa uendelezaji madini (Mineral Development Agreements - MDAs) walizosaini hawa anaowaita wanyonyaji na serikali za watangulizi wake Jakaya Kikwete na Ben Mkapa.

6) Wakati tunahamasishwa kumuunga mkono jemedari huyu shupavu, bado hatujaonyeshwa mkataba hata mmoja waliosaini na wanyonyaji hawa tangu miaka ya mwanzo ya '90.

Leo Jemedari Mkuu ameahidi kwamba mikataba hiyo italetwa bungeni. Safi sana.

Lakini je, hii ni mara ya kwanza tunaahidiwa hayo???

Mwaka '08 Jemedari Mkuu wa kabla yake alituahidi hivyo hivyo. Tuwe na subira kabla ya kuanza kushangilia prematurely.

7) Nimemsikia Magufuli akielekeza wahusika wote wa uchafu huu washughulikiwe. Kweli???

(a) Je, Jakaya Kikwete aliyesaini leseni za Bulyanhulu na Nzega mwaka '94 anaponaje???

(b) Je, Ben Mkapa aliyekuwa Rais na Mwenyekiti wa Cabinet wakati haya yanafanyika anaachwaje???

(c) Je, waliokuwa mawaziri na manaibu wao wote wakati haya yanatokea wanasalimikaje???

(d) Je, wale washangiliaji na wapiga meza wa bungeni, ambao waliunga mkono kila walicholetewa bungeni na kukipitisha kilivyo wanakosaje lawama???

8) Nimesikia Acacia Mining hawana hata leseni/usajili wa kuendeshea shughuli zao hapa nchini. Labda. Hata hivyo, jiulize yafuatayo:

(a) Hivi wamekuwa wanalipa kodi kama PAYE, SDL, income tax, withholding tax, mrahaba, n.k., kwa kutumia jina gani miaka yote hii???

(b) Je, wana akaunti yoyote katika benki za Tanzania??? Kama ndio, wamezifungua kwa jina gani???

Kama hapana, wanalipaje mishahara ya wafanyakazi wao wa Kitanzania au watoa huduma mbali mbali wa Kitanzania???

(c) Je, wanalipa bili za umeme kwa TANESCO au za simu kwa Vodacom, Tigo, Airtel, n.k. kwa kutumia jina gani???

(d) Je, wamesajiliwaje katika Soko la Hisa la Dar kama Acacia kama wanaendesha shughuli zao kihuni hivi???

(e) Kuna kitu kinaitwa 'estoppel' katika Sheria yetu ya Mikataba (the Law of Contract Act, Cap. 345) na katika Sheria yetu ya Ushahidi (the Law of Evidence, Cap. 6).

Je, estoppel haituhusu kwenye suala hili la leseni au usajili ya Acacia???

Kama estoppel inahusika, je, hoja hii ya ukosefu wa usajili ina uzito gani, kama upo, kisheria???

9) Nimesikia Sheria za Madini zinatakiwa kufanyiwa marekebisho makubwa. Sawa kabisa.

Lakini je, kwanini Rais Magufuli hajasema chochote juu ya Sheria za Gesi Asilia na Mafuta ambazo zilipitishwa haraka haraka kwa Hati ya Dharura baada ya sisi 'waropokaji' kutimuliwa bungeni na Spika Anna Makinda mwaka '15???

Au Rais wetu anaamini kwamba Sheria za Gesi Asilia na Mafuta hazina matatizo licha ya kupitishwa kwa utaratibu ule ule uliotumika kwa Sheria za Madini???

10) Wakati tunaingojea kwa hamu mikataba ya madini iletwe bungeni, hebu na tujiulize yafuatayo:

(a) Mikataba ya uchimbaji gesi asilia na mafuta nayo iko wapi???

(b) Mikataba ya manunuzi ya Bombardier na Dreamliner za Magufuli nayo italetwa bungeni au itabidi tusubiri aondoke madarakani kwanza kama ilivyokuwa kwa JK na BM???

(c) Mikataba ya ujenzi wa airport Chato na Reli ya Standard Geji ya Waturuki au Wachina na mabarabara kibao nayo italetwa bungeni au ndio basi tena tusubiri Bwana mkubwa atakapoondoka madarakani???

Wakati tukisubiri kufukuzwa bungeni na Spika Ndugai kwa maelekezo ya bosi wake, na wakati tukisubiri dhahama ya Bwana Mkubwa nje ya Bunge, hebu na tujiulize hivi nani hasa ndiye mzalendo wa kweli wa nchi hii???

Hebu na atutajie majina na namba za simu za wale wote ambao amedai wamekuwa wanawasiliana na Acacia na lini walifanya mawasiliano hayo na yalihusu kitu gani. Kutoa hukumu kwa innuendo peke yake haitoshi, tunahitaji ushahidi thabiti kutoka kwa Rais Magufuli.

Sijazungumzia bado plagiarism ya taarifa mbali mbali za kiserikali na zisizo za kiserikali katika Taarifa ya Kamati ya Prof. Osoro. Hili ni la baadae.
Serikali ya awamu hii inaishi na kuongoza kinafiki wakijifanya wazarendo lakini hamna lolote la maana linalofanyika zaidi ni kutuandalia hali ngumu ya maisha kwa baadae, ki ukweli huwezi kudhibiti mchanga kusafirishwa wakati huo umeacha madini yenyewe kusafiri bila kipingamizi halafu ukajiita mzarendo☹️☹️ huu ni unafiki wa kiwango cha makinikia..
 
Back
Top Bottom