Lissu: Serikali ya Magufuli imejaa wapigaji

Lissu: Serikali ya Magufuli imejaa wapigaji

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
26,691
Reaction score
59,193
Heshim kwenu wakuu,

Mbunge Tundu Lissu, amehoji Maswali Mawili;

1. Kama Rais Magufuli hawezi kusafiri nje kwa kuogopa wapigaji, maana yake ni kwamba serikali yake yote, kuanzia Makamu wa Rais, ni wapiga dili.

2. Hivi Juliana Shonza na MaCCM wenzake wataweza kuja kutoa ushahidi mahakamani kwa mashtaka ambayo wamewafungulia wabunge wa CHADEMA leo?

WAKATI utawala wa Rais Dk. John Magufuli ukikaribia mwaka wa pili, huku akiwa amesafiri nje ya nchi mara chache ikilinganishwa na watangulizi wake, amevunja ukimya akisema kwamba anataka kwanza kumaliza wapiga dili ambao akiondoka wataweza kufanya mambo ya ajabu.

Amesema tangu aingie madarakani amepata mialiko zaidi ya 60 kwenda nje ya nchi, lakini ameikataa kwa sababu anataka kuishughulikia Tanzania kwanza.

Rais Magufuli alitoa kauli hiyo jana wakati akizindua mradi wa uboreshaji maji wa Sengerema akiwa katika ziara yake mkoani Mwanza.

“Ndiyo maana mimi sitembei sana, nikienda huko watafanya ya ajabu, ngoja nidili nao kwanza, lazima nihakikishe nasafisha kwanza.

“Leo (jana) nilitakiwa niwe Ethiopia kwenye mkutano wa AU, nimeona nimtume makamu wangu (Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan), ameniwakilisha na anafanya kazi vizuri, mimi ngoja nidili na ya watu kwa sababu nilichaguliwa kwa ajili ya Watanzania, safari nitaenda nikishastaafu.

“Ngoja nizifanyizie safari humu humu ndani kwani ningejuaje kama kuna Sh bilioni mbili za maji zimeibwa na kama wapo walioziiba waanze kuzirudisha.

“Kabla sijaondoka vyombo vyangu vitaanza kufuatilia kwa sababu nina Serikali iko hapa. Lazima mali za watu masikini ziende kuwanufaisha watu, ndio wajibu wangu na ndio haki yao,” alisema.

Wakati huo huo leo Viongozi wa Juu na Wabunge wa Chadema wamefurika nje ya jengo la Makakama Kuu Mjini Dodoma kusubiri kesi ya shambulio la mwili inayomkabili Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea.

Kubenea anashitakiwa kwa kosa la kumshambulia Mbunge wa Viti Maalum, Juliana Shonza.
 
Magufuli hawezi kusafiri nje kisa anaogopa wapigaji?

What the flip is that?

Ndo Magu alivyowahi kusema au ni ubunifu wa fikra za Lissu tu?

Kuhusu Bi. Shonza....dada mshari sana huyo.

Halafu sijui anajiamini nini tu maana mmoja wa wale wabunge wa CHADEMA [simjui jijna] ni bonge la jimama.

Likimlalia Bi. Shonza linam-suffocate kabisa😀
 
Alisema jana kuwa ananyoosha nchi kwanza, kwa mfumo wa nchi yetu, Rais ndiye kila kitu, hivo Mh. Rais anajua kabisa akiondoka tu hali inaweza kubadilika huku nyumbani.

Kikwete aliwaachia uhuru wa kutosha mawaziri na watendaji wake serikalini yeye akawa anazurura tu nje ya nchi, yaliyotokea kila mtu anayajua
 
Mtukufu Rais aliwahi kusema hivyo mkuu!
 
Alisema jana kuwa ananyoosha nchi kwanza, kwa mfumo wa nchi yetu, Rais ndiye kila kitu, hivo Mh. Rais anajua kabisa akiondoka tu hali inaweza kubadilika huku nyumbani.

Kikwete aliwaachia uhuru wa kutosha mawaziri na watendaji wake serikalini yeye akawa anazurura tu nje ya nchi, yaliyotokea kila mtu anayajua
Mbona aliye agiza vichwa vya treni anamfahamu lakini anapiga kelele pembeni bila kumnyookea???
 
Magufuli hawezi kusafiri nje kisa anaogopa wapigaji?

What the flip is that?

Ndo Magu alivyowahi kusema au ni ubunifu wa fikra za Lissu tu?

Kuhusu Bi. Shonza....dada mshari sana huyo.

Halafu sijui anajiamini nini tu maana mmoja wa wale wabunge wa CHADEMA [simjui jijna] ni bonge la jimama.

Likimlalia Bi. Shonza linam-suffocate kabisa😀

Msikilize mwenyewe, hasa kuanzia 2:45
 
Point ijibiwe Kwa point
Kama anaogopa kusafiri kwasababu ya wapigaji, basi lazima atabaki madarakani indefinetly kwasababu hiyo hiyo hiyo ya wapigaji.Cha kubadilisha hapa ni mfumo. Mbona mwalimu walifanikiwa kumdanganya na alikuwa akifuatilia pengine kuliko Huyu wa sasa.
 
tanzania ameikuta ataiacha..
awashukuru akina kikwete na mkapa kwa bao la tumbo walilompigia hadi leo anaweza kubadilisha kuku ikulu.
hata yeye hatumuamini..hakuonesha uaminifu hata kwenye rambirambi..
zile bilioni 900 za malimbikizo ya watumishi nazo kazipeleka wapi..
kwanza atangaze mali alizonazo kwa mujibu wa sheria ya maadili ya viongozi..
 
Back
Top Bottom