Lissu ni kibaraka, anatumiwa na mabeberu wanaotaka kuiba rasilimali za Tanzania

Bora kuwa dalali wa Magharibi kuliko kuwa kibaraka wa Wachina..Tumewahi kuona balozi wa China anahutubia mkutano wa ccm,mbona hatuwaoni wazungu kwenye mikutano ya TL? ccm mtaweweseka sana mwaka huu
 
Mwaka huu mtaanzisha nyuzi nyingi sana za uongo na kweli, uzushi na uchochezi, lakini mpaka mtaongea ukweli tu! Lissu ndiye mkombozi wa hapa tulipokwama!
 
Meko ni dalali wa israeli mtoa roho na shetani mleta mateso kwa binadamu.

Bora Lissu dalali wa mabeberu wanaotuwesesha kupata scholarship na misaada kedekede kwa individuals na our country at large.
Mbona sijawai muona Meko huko Israel Kama nilivyomuona Mbeligiji huko Ubelgiji!?
 
Tajiri Tanzanite,

Kuliko kutuletea utawala wa kikabila na kidini na kikatili ni bora tu waje hao Mabeberu waweke hiyo mikataba ya siri.
Kwani ni mkataba upi uliowahi kuganywa kwa wazi na hao CCM?
Hivi Huseni anatafuta nini kule Zanzibar?
Hivi mnatafuta nini kama watanzania wanamtaka Lisu?
Ina maana Mabeberu watakuja kumpigia Kura Lisu?
Ina maana wale watanzania wanampokea kwa maelfu ndio Mabeberu?

Hii nchi kama kweli kuna mtawala mzalendo basi ajae na sheria ya kuweka wazi mali za Makada wa Chama cha Mapinduzi na jinsi walivyozipata kuanzaia awamu ya kwanza waliofilisi Mashirika ya umma na vyama vya ushirika na baadae kujiuzia nyumba zote za umma na kila kitu cha umma kwa bei chee na wengine kujimilikisha mali za umma kwa mikopo ambayo haikulipika ipasavyo . Kila kitu maCCM walishakichukua na kukimiliki na familia zao. Usione mavyombo ya dola yakiongozwa na Makada wa CCM kinyume na katiba lakini ni kuwa ni watu walioshiriki kwenye kujimilikisha utajiri wa nchi hii.

Hawana lolote Makada wa CCM walioko kwenye mahakama ,Vyombo vya dola n.k, wote ni wanufaika wa rasilimali na kodi za nchi hii bila huruma.

Wapo tayari kutumia Dola kuua kila mtu wabaki peke yao kwa kisingizio kuwa wao ndio wanaolinda amani ya nchi huku wakijua wazi rohoni mwao kuwa wanalinda wizi wao.

Ogopa watu wanapata madaraka kwa dhulma , uchawi,rushwa ,uzinzi, ahadi za kupeana madaraka na vyeo vyenye maslahi. Watu wanaopeana madaraka wakiwa kwenye mabaa wakiwa wamelewa pombe kichwani. Hakuna Mtawala mwenye huruma na mtu zaidi ya nafsi yake na familia yake. Ndio maana wakishapata wanawapa vyeo watoto wa Dada,shangazi , wajomba ,mashemeji, n.k.

Ndio maana tunataka Lisu naye apate tu aweke sheria Kali na asimamie Katiba.

CCM wanakosa umakini ndio maana tunaibiwa na wazungu.

Kinge kinawapiga chenga matokeo yake hata mikataba inakua ni holela na hawaisomi mana imeandikwa kingereza.
Lisu ndiye jawaba ya hao wazungu mana anaijua sheria na sio mtu wa kudanganywa au kuandika mikataba ya kijinga.

Mungu ndiye nayejua kuwa nani atashinda uchaguzi wa mwaka huu.

Mungu amechoka kuwa chini ya binadamu na kuona mtu anatukuza kuliko yeye.

Lisu angekua anatamaa ya Fedha kama hao wazalendo waliokuwapo miaka yote na wakashiriki kutuibia na kujilimbikizia mali zote za nchi hii na hata Mungu anaona wanavyodanganya midomoni mwao huku mioyoni mwao wakiwa wameficha mali walizochuma kupitia SERIKALI ya CCM iliyotawala tangu Uhuru basi angejipendekeza kwao na kupata nafasi za kujilimbikizia mali kama walivyofanya wengine.

Ogopa mtu anayepigwa risasi 16 halafu bado anasema Yale Yale bila kubadilika.

Hao wengine hawapendi hata kujibiwa tofauti na wanavyotaka sembuse kupigwa risasa hata iwakose wangejenga Chuki isiyoisha.

Lisu ni mvumilivu sana na Mungu anamwona na anpango naye. Hakuna namna kama Mungu amepanga hakuna wa kumzuia na atakayezuia mpango wa Mungu ataaibika milele.

Adamu alipoumbwa na Mungu alipewa amri au Katiba ya kuifuata na sio Madaraja wala mareli na mabwawa.
Adamu Alihesabiwa kuwa amemwasi Mungu pale aliposhindwa kufuata amri au Sheria au Katiba aliyopewa na Mungu .
Tunataka Kiongozi atakayetuongoza kwa haki na mwenye kufuata sheria au katiba ya nchi . Mwenye kutenda haki na asiyembaguzi wala makabila na akijaribu kuwa mkabila basi atakutana na katiba na sheria inayomkataza na kuweza hata kumvua uongozi.

Katiba tuliyo nayo inampa mamlaka Rais kuweza kuweka hata serikali nzima ndugu zake wa familia yake tuu. Na hakuna wa kusema na ukijaribu unapewa kibano cha uhakika. Hii ni zaidi ya Ubeberu. Tumwache Lisu mana hata ujio wake umebadili watu ndani ya CCM walioanza kujawa na kiburi na kumdharau mpaka mungu na ukuu wale kwa kusema kuwa kuna mtu ameikimbiza korona .

Kuhusu rasilimali kuwapa wazungu ni uzushi mana mpaka sasa nchi hii haina kilichobaki .Mpaka Ardhi ya nchi yetu ilyouzwa kwa Mwarabu Kule Loliondo hatujasikia Mzalendo feki yeyote akiizungumzia . Tafakari utagundua kuwa CCM ni kama alivyosema Prof. Lipumba. liyeamua kutumia viongozi wa Dini matapeli na wabinafsi wanaotumia shida za watu kujitajirisha na kujilimbikizia mabilioni ya pesa na Mali za kila aina bila kuwa na uchungu na maisha ya watu maskini na wengine waliwatukana mpaka makadinali enzi za JK kwa sababu tu ya kuuchukia uislama wa JK, leo wanagombea Ubunge kupitia Chama kile kile walichotumia kumtukana JK na kadinali Pengo.
Tanzania hii ndiyo Mwalimu Nyerere aliitaka, lakini Watanzania ndiyo tumeshabadilika hata hao CDM ndiyo walewale maana Ubinafsi umesha tutawala kwenye nafsi,kila mtu anataka kula na familia yake tu!!
 
Na kama kuna mtu anayepaswa kulipizwa kisasa basi hawezi kukwepa kisasi mana kisasi ni juu ya Mungu. Na Mungu amemponya Lisu na kisaha kuondoa Korona ili Uchaguzi mwaka huu ufanyike kama ulivyopangwa na Lisu arudi siku salama ambayo hata yule Mla raha zote z duniani kwenye nchi maskini alikua ameshacha ukuu wa mkoa na ikawa ni siku ya msiba mkubwa .
Yote hayo ni wazi kuwa Kuna jambo Mungu amelipanga kupitia Lisu . Mabeberu mnawasingizia tuu. Lisu kama sio mwaka huu lakini kuna dalili ya kuja kuingia madarakani na kuweka sheria na katiba mpya yenye misingi ya haki na usawa. Itakua ni uamuzi wake kulipa kisasi au kusamehe japo hawezi kulipa kisasi mana kitendo alichofanyiwa sio cha kibinadam na ni kitendo kilicho kinyume cha sheria na haki za binadam. Lisu ni muumini wa haki
Lissu Kama kweli yeye ni Mzalendo kweli,aingie CCM na ataona baada ya mitano ya Magufuli 2025 CCM watamsimamisha,Kama kweli ana nia ya dhati kuikombowa Tanzania!!
 
Nasikia mgombea wenu ashaanza kuchanganyikiwa. Sasa ilani kaitupa pembeni, anaanza kuahidi vitu anavyoahidi Lissu. Jana kuna sehemu alisikika akisema Mungu oyeee.
 
Lissu Kama kweli yeye ni Mzalendo kweli,aingie CCM na ataona baada ya mitano ya Magufuli 2025 CCM watamsimamisha,Kama kweli ana nia ya dhati kuikombowa Tanzania!!
Maskini hata kuandika Kiswahili hajui.
Ada aliyolipa mzazi wako ni kumtia hasara tu. Kuikombowa maana yake nini?
 
Lissu Kama kweli yeye ni Mzalendo kweli,aingie CCM na ataona baada ya mitano ya Magufuli 2025 CCM watamsimamisha,Kama kweli ana nia ya dhati kuikombowa Tanzania!!
Hatashetani huja kwa sura ya malaika akiwaaminisha watu ni mwema...Lissu ni Sio hata kidogo.

Kuna mambo yanayosababisha watu tuamini kuwa Lisu ni mpango wa Mungu .
JPM aliletwa na Mungu kama alivyokuwa Yohana Mbatizaji aliyetangulia kunyoosha njia ya Masihi.
JPM kazi yake ya inapaswa kukamilishwa na Mpenda haki.

Jiulize ni kwa nini Lisu apigwa risasi 16 kisha apone na kurejea akiwa na akili zake Timamu nila woga.
Hivi yeye halendi kuishi kama hao wengine ambao walishastaafu lakini bado wanapigania maslahi yao?
Kwa nini Mungu aiepushe Tanzania na Korona uchaguzi uendelee bila kuahirishwa. Si ingekua rahisi tu kuendelea na Korona ili Yohana aendelee hata mpaka 2025?
Kwa nini Mungu amrejeshe Lisu wakati Makonda mtumia nguvu za Risasi akiwa amejiuzulu Ukuu wa mkoa kwa hiyari yake ?
Kwa nini Mungu amrejeshe Lisu wakati wa msiba mkubwa wa Mkapa na kuacha nafasi kwa wananchi kumpokea nila kupigwa mabomu na kuumizwa.?
Kwa nini Watanzania wamejawa na Furaha kumuona Lisu bila hata kulazimishwa wala kuahidiwa vyeo kama wengine wanavyofanya ili kuwafurahisha watu?
Kwa nini watu wamejawa na ujasiri walipomuona Lisu na Hofu kuwajaa CCM wenye Mabomu na risasi kwenye maghala yaajeshi wanayotumia kuwatisha watanzania Wenzao?
Kwa nini CCM imepoteza dira ya utu,haki, usawa, umoja shikamano na serikali kutojifungamanisha na dini wakati huu wa uchaguzi?,

Bila shala Mungu ameingilia kati na kuchukua huzuni ya watanzania.

Huwezi kuwaua watu kwa dhulma unayofanya eti unapigania rasilimali zilizoumbwa na Mungu.
Dunia ni ya Mungu na vyote tutaviacha.
Kuua watu,kutesa watu na kunyanyasa watu waliombwa na Mungu kwa sababu ya yale anayotengeneza mwanadamu kwa Kodi zao ni jambo baya sana.
 
Augustino Chiwinga
0756810804.

Kibaraka ni mtu anayetumiwa kuhujumu mtu,jamii, au Taifa kwa manufaa au maslahi ya mtu au kikundi kinachomtuma.

Vibaraka wapo kila nchi na hapa Tanzania tunao pia mmjowapo ni Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu.

Ukweli mchungu ni kwamba vita ya Uhuru wa kiuchumi anayopigana Rais Magufuli imeacha majeruhi wengi kwa wanufaika wa mtandao wa wizi uliokua umekithiri Tanzania.

Majeruhi wa vita hiyo ndani na nje ya nchi hawajaridhika za hatua za kizalendo anazochukua Mh.Rais Magufuli, wamejipanga kumyumbisha na kumrudisha nyuma katika vita yake hiyo.

Wanatumia mbinu na mikakati mbalimbali ikiwemo vyombo vya habari, na kuwapandikiza ama kuwanunua watu katika sehemu mbalimbali na ndio hao wanaoitwa vibaraka.

Tundu Lissu ni miongoni mwa watu hao wanaopokea malipo ya kutumika na Mabeberu yaliyokua yananyonya raslimali ze nchi.Ziara zote na maneno anayoongea ni malipo ya fedha alizolipwa na mabwana zake ili kuichafua taswira ya nchi yetu lakini haswa.

Majizi yaliyokua yanaiba kwenye madini, nishati, na raslimali nyingine yameungana kumpiga vita Rais Magufuli kupitia vinywa vya Watanzania wenzetu vilivyokubali kununulika na kuuza utu wao.

Kibaraka ni mtu mbaya na hatari anayeweza kutamka au kufanya jambo lolote ili kuwafurahisha mabwana zake.Kibaraka ni adui wa Taifa lolote.

Tundu Lissu anatumika na mabeberu majizi,wanataka Rais Magufuli apunguze makali ili yaendelee kunufaika na wizi waliokua wanaufanya.

Tumkate Kibaraka wa Mabeberu Tundu Lissu na matendo yake yote
Huenda uko sahihi lkn naomba nifafanulie kuhusu
- fao la kujitoa kwa watumishi,
- asilimia 3 - 15 elimu ya juu,
- bei ya mazao ya kibiashara kuporomoka (pamba 2,100 - 880; kahawa 2300 - 1100; korosho nk nk). Mazao ya chakula muhogo 600 - 250);
- hivi sukari inauzwa bei gani kweli

Kwa ufupi huenda hoja yako iko sahihi lkn tujiulize hizi hasira za hawa uliowaita watanzania zinatokana na nini?
 
Back
Top Bottom