Lissu na Samia, Maaskofu na Mashekhe

Lissu na Samia, Maaskofu na Mashekhe

TheMaster

Member
Joined
Aug 10, 2023
Posts
61
Reaction score
131
Nimesoma kitabu cha CRASH OF CIVILIZATION AND REMARKING OF NEW ORDER cha mwandishi nguli Samwel P. Huntington juu ya namna gani watu wamekuwa na ustaarabu mpya wa kujuana na kutambuana aidha hata kuhishimiana kutokana na dini zao kuliko hata tamaduni zao.
Mwandishi alianza kwa kunishtua mtima wangu pale alipoandika
Unless we hate what we are not we cannot love what we are”
Bado akaendelea katika ukurasa uleule kuwa
We know who we are only when we know who we are not and often only when we know whom we are against”

Hapa Utakuta muislamu akisha mtambua muislamu mwenzake, hata salamu hubadilika na kuwa Assalaam alaykum
Vivyohivyo kwa wakatoliki Tumsifu yesu kristu.
Kwasasa naiona ile salamu ya kiswahili Shikamoo na marhaba ikipotea kwa kasi kubwa saana. Yote ni kwasababu ya ujio wa ustaarabu mpya wa watu kutambuana kwa dini zao zaidi.

Mwandishi samweli bado akaendelea kuandika “To a very large degree, the major civilizations in human history have been closely identified with the world’s great religions; and people who share ethnicity and language but differ in religion may slaughter each other

Andiko hili likanishtua zaidi kisha nikakumbuka yaliyotokea Centra Africa kati ya SELEKA na ANTI-BALAKA
Bado nikafikiria yaliyotokea Burma mzozo uliowaumiza zaidi kundi la kiislamu la Rohingya dhidi ya kundi la kidini la Budha

Sijaishia hapo nikawazua yaliyoendelea China dhidi ya Wakristu na Waislamu wa Uyghur, Kadhalika kugawanyika kwa Sudan na Sudan Kusini, Mgogoro wa waislamu na wahindu huko India nk.

Dini zimebeba ushawishi mkubwa zaidi kwa binadamu kabla ya kitu chochote na hivyo bhasi, dini zikiingia kwenye Siasa kwenye Taifa ambalo watu wake wametofautiana imani za kidini, kwa namna yeyote lazima itawasha moto kwenye vifua vya watu.

Padri au Askofu akimkosoa hadharani Rais Muislamu, Wakristu watahishimu lakini Waislamu hawawezi kuhishimu wala kusikiliza maoni ya padri au askofu kwasababu, WE KNOW WHO WE ARE ONLY WHEN WE KNOW WHO WE ARE NOT .

Kadhalika Mashekhe wakimkosoa Rais Mkristu, Waislamu watahishimu na kusikiliza lakini Wakristu katu hawawezi kutilia maanani maneno na kauli za mashekhe kwasababu WE KNOW WHO WE ARE ONLY WHEN WE KNOW WHO WE ARE NOT .

Pindi Maoni ya mashekhe na Maaskofu yatapokinzana juu ya mwenendo wa kiongozi wa nchi, nachelea kusema ni rahisi zaidi kuzua tafrani na mgogoro mkubwa kwenye taifa kwasababu ya hisia tofauti na tumeshashuhudia huko nyuma kuwa “people who share ethnicity and language but differ in religion may slaughter each other”

Naona Taifa la Tanzania sasa Maaskofu wameelezea Hisia zao kukerwa na Mkristu mwenzao Tundu Antipas Lissu kuswekwa korokoni na kuagiza aachiwe haraka bila masharti, kauli ambazo hazipaswi kabisa kusemwa kwenye vipaza sauti na vyombo vya habari kwa kuhofia mtafaruku.

Bado hatujakaa sawa, tumeona mashekhe mmoja mmoja wameanza kuelezea hisia zao kukerwa na maoni na hisia za maaskofu kuingilia mamlaka inayoongozwa na Muislamu Mwenzao, kuwa mbona kipindi akiongoza mkristu alifanya kila aina ya ukatili lakini kanisa haliwahi kupiga kelele kama hivi?

Je, mwisho wake ni nini?

KWASASA NIKIMTAZAMA SAMIA NA TUNDU LISSU, NAUTAZAMA UISLAMU NA UKRISTU.

Kwaheri Papa Francis
 
Ujumbe wa Kwaresima 2019 Maaskofu haohao walimshukia vikali muumini wao aliyekuwa mtawala (soma katika sura ya tatu.)

Sasa kwanini Sasa maoni yao yaonekane ni udini? (Kwamba Wanapendelea)

Wao wanelezea maadili yanavyopaswa kuwa bila kujali ni wa dini Yao au sio wadini yao.

Hivyo hoja yako haina mashiko,totally absurd.
 

Attachments

Ujumbe wa Kwaresima 2019 Maaskofu haohao walimshukia vikali muumini wao aliyekuwa mtawala (soma katika sura ya tatu.)

Sasa kwanini Sasa maoni yao yaonekane ni udini? (Kwamba Wanapendelea)

Wao wanelezea maadili yanavyopaswa kuwa bila kujali ni wa dini Yao au sio wadini yao.

Hivyo hoja yako haina mashiko,totally absurd.
Sahihi
 
Back
Top Bottom