Lissu na Kichwa cha Yohana Mbatizaji kwenye Sinia

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,891
LISU Na KICHWA CHA YOHANA MBATIZAJI KWENYE SINIA

Na, Robert Heriel


Moja ya hadithi mashuhuri duniani hasa kwa Wafuasi wa Dini za Ukristo ni Pamoja na Kisa cha Nabii Yohana Mbatizaji ambaye kwa Waislamu hufahamika kama YAHAYA. Yohana Mbatizaji(John the Baptist) aliitwa Sauti iliayo Nyikani. Alikuwa ni mtayarishaji au mtu aliyemsafishia njia Yesu wa Nazareth.

Yohana Mbatizaji alikuwa Mashuhuri kwa kipindi kile kuliko hata Yesu, licha ya kuwa alikuwa akitangaza ujio wa Masihi(Yesu Kristo) Yohana Mbatizaji alikuwa na Wafuasi wengi kuliko Yesu kwa kipindi kile bila shaka ni kutokana na uwepo wake wa muda mrefu kwenye field ya unabii. Hii ni kusema hata watawala serikalini walimfahamu akiwemo Mfalme Herode.

Yohana aliingia matatani kwa sababu ya Kusema ukweli; Mdomo wake ndio uliomponza, hata hivyo alikuwa kwenye majukumu yake ya kinabii na kiutumishi kwani moja ya kazi ya nabii ni kusema ukweli na kukemea maovu. Nabii, kuhani, Askofu au mchungaji, Sheikhe, Imamu, Mufti na wengineo wasimamao kwenye madhabahu ya Bwana moja ya kazi zao ni pamoja na Kukemea uovu na kusema ukweli bila kujali nani kaufanya na nini matokeo yake.

Ukiona unaabudu kwenye dini, kanisa, msikiti ambao viongozi wake wanashindwa kukemea uovu au kusema ukweli kwa kuwaambia watu. Au wanaubaguzi wa kukemea watu maovu yao, yaani wanauwezo wa kuwakemea waumini wa kawaida wafanyapo makosa lakini muda huo huo wanashindwa kuwakemea viongozi wakubwa wa nchi, au kukemea matajiri, basi jua unaabudu mahali pasipo sahihi. Jua kiongozi huyo wa dini hana mamlaka ya kukusalisha, hana kibali cha Mungu bali anajali maslahi yake.

Ni bora ukaabudu Msikiti au kanisa la Mashetani linalokemea maovu kuliko kuabudu katika msikiti au kanisa linalojiita la Mungu wakati linashindwa kukemea maovu.

Yohana Mbatizaji kama walivyo manabii wengine na makuhani waliowaaminifu akamchana makavu Mfalme Herode kwa kumwambia aache dhambi ta Uzinzi kwa kutoka na Mke wa Kaka yake, kwani hiyo sio halali.

Ukisoma kisa kile utagundua kuwa Mfalme Herode alikasirika mno na alitaka kumuua lakini alihofia watu kwani walishamuona Yohana Mbatizaji kuwa ni Nabii. Hivyo alichokifanya akaunda njama/ zengwe, na Hila akamsweka Yohana Mbatizaji Mahabusu. Nafikiri lengo lake ni kuondoa kero za Yohana Mbatizaji ili yeye azidi kula Uroda na Mke wa Kaka yake, yaani shemeji yake. (Na Hapa ni Mke wa Kaka yake Mfalme Herode yaani shemeji yake)

Kumbuka kusema ukweli ndio kilichomponza Yohana Mbatizaji lakini hatuwezi kusema kilimponza kwani alikuwa kwenye majukumu yake. Ni sawa na Dokta kujichoma sindano kwa bahati mbaya wakati akimchoma mgonjwa.

Kumbe yule mwanamke(Herodia mke wa Filipo anayechepuka na Mfalme Herode) naye alipenda mchezo wa kuliwa uroda, hivyo hakupendezwa na harakati za Yohana Mbatizaji. Hivyo naye alimuweka kiporo huku akimtafutia nafasi ya kumuangamiza.

Siku moja ya ya karamu katika Jumba la Mfalme Herode kulikuwa na muziki ambapo binti mmoja alicheza kupitiliza (binti huyu mamaye ni Herodia) mpaka Mfalme Herode akafurahi na kumpa nafasi ya kutaka lolote naye akiahidi kumpa. Binti Herodia kusikia hivyo akaenda kwa Mamaye(ndiye Herodia) kumuuliza, hii ikawa nafasi ya herodia kummaliza Yohana Mbatizaji. Hivyo akaagiza aletewe kichwa cha Yohana Mbatizaji kwenye Sinia.

Binti akarudi akamuambia Mfalme Herode kuwa anahitaji kichwa cha Yohana Mbatizaji kiletwe pale muda ule ule kikiwa kwenye sinia. Bila shaka Mfalme akajua kuwa hizo ni hila za mchepuko wake(Herodia) Pengine ingekuwa filamu basi angegeuza shingo taratibu na kumuangalia mchepuko wake, kisha mchepuko wake(Herodia angetabasamu kwa kuona ameshinda.

Mfalme Herode aliumia sema hakuwa na jinsi kwani tayari alishaahidi tena mbele za watu. Hatimaye kichwa cha Yohana Mbatizaji kilikatwa huko Gerezani na kuletwa kwenye sinia. Loooh!

Kichwa cha Nabii leo juu ya sinia, mbele za watu mziki wa starehe ukipigwa watu wakishangilia wachache wakisononeka.

Lisu ni kama Yohana Mbatizaji, anasema ukweli lakini ukweli wake hauna maana yeyote kwa watu wapumbavu na waovu. Lisu yupo kwenye majukumu yake, hata ajali aliyoipata ni ajali kazini.

Lisu anaeleweka zaidi kwa watu wapenda haki, watu wa Mungu, na anaeleweka zaidi na Mungu.

Lisu hawezi na kamwe hataeleweka kwa watu waovu, wenye tabia ya umungu mtu, mashetani, pengine na wale wajinga ambao sio kosa lao kwani wamepotoshwa na waovu.

Hakukuwa na sababu ya Kumkata Kichwa Yohana Mbatizaji, haikuwepo. Pengine ilikuwepo sababu moja tuu! nayo ni uovu, yaani kumuua msema kweli, mkemea maovu kusudi waovu waendelee kutanua.

Ukweli ni huwezi kumuua ateteaye uovu ukaacha kuua. Lazima uendelee kuua na kuua na kuua mpaka nawe utakapokufa. Walipomuua Yohana Mbatizaji, walidhani wamemaliza kazi lakini kumbe mambo hayaendi hivyo. Punde Yesu naye anaingia kwenye Field, naye wakamuua, wakadhani wamemaliza, lakini haikuwa hivyo, wakaanza kuwaua wanafunzi wake, wakadhani wamemaliza, Looh! haikuwa hivyo wakazaliwa wengine mpaka wakina Martin Luther, Kina Wyclif, William Miler, mpaka hivi leo tupo bado watetezi wa haki huuawa.

Wauaji hawajui jambo moja, huwezi ukamaliza watetezi wa haki kwa kuwaua. Kama ilivyo kwa watetezi wa haki, huwezi kumaliza uovu kwa kuwaua waovu. Uovu haumalizwi kwa kuua watu. Au haki au wema haumalizwi kwa kuua watu wema. Bali mambo hayo humalizwa kwa elimu ya kiroho, na kuchanganya damu.

Lisu ni kama kichwa cha Yohana Mbatizaji kwenye Sinia. Kumkata kichwa haimaanishi ndio kumaliza harakati zake.

Nafikiri waliompiga Lisu Risasi wataungana na Mimi kuwa Risasi au kumuua mtu sio njia sahihi ya kuondoa utetezi wa haki, au kuondoa uovu kama waliona uovu kwa Lisu.

Nimalize kwa kusema; Mungu ni Upendo, nao wenye upendo hao ndio watoto wake.
Hatuwezi nyamazishwa na wanadamu ikiwa tunajua tunatetea haki. Lakini pia hatuwezi kukaa kimya kisa watendao uovu ni watu wetu wakaribu tuwapendao.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa Unguja.
 
Umeandika makala Nzuri sana Sina la Nyongeza zaidi ya kukubali kipawa chako mkuu.

HII MAKALA IMENIGUSA SANA
1.Ukigusia kuielewa vizuri sana misaafu ya neno La mungu.
2. Kusisitiza upendo miongoni mwa watu.
3.Hata makala imekuwa ni mahubiri tosha kwa siku ya leo.
Jumapili.

Kwa kweli sikua na haja ya kwenda kuhubiriwa zaidi ya haya mahubiri mazuri yaliyo nyooka.

Nakubali sana Fasihi na makala zako Taikon Robert lakini selikali zote Duniani huwa hazipendi ukweli.HOFU NI USALAMA WAKO.
 
Mleta mada acha kutumia maneno ya Mungu isivyostahili utapata laana
 
Nabii wa uongo wewe mleta mada tarehe 28 October haitakuacha salaam kama una wafuasi utakimbiwa mchana kweupe na kama Luna waliokuwa wakikuhitaji kuwa. Njoo utuhubirie hutawaona tena

Wewe ni nabii wa uongo mia kwa mia .October 28 ndio itakupa cheti rasmi kama nabii wa uongo Robert Heriel
 
Nabii wa uongo wewe mleta mada tarehe 28 October haitakuacha salaam kama una wafuasi utakimbiwa mchana kweupe na kama Luna waliokuwa wakikuhitaji kuwa. Njoo utuhubirie hutawaona tena

Wewe ni nabii wa uongo mia kwa mia .October 28 ndio itakupa cheti rasmi kama nabii wa uongo Robert Heriel

Hhahahaha! Mimi sijawahi kuwa nabii, mchungaji au askofu.

Mimi ni Taikon wa Fasihi
 
Huyu muongo anaesingizia watu wa tume kukutana na Raisi hawezi hata kidogo kuwa na roho ya kuwa yohana mbatizaji,
Tafadhali iondie hiyo hadhi kwake, mtu snitch leo awe kama yohana?


Alisema tuache makinikia yaende bila kujiridhisha kuna nini na badae akawa anawaibia data Accacia halafu useme ana umungu ndani yake?


Anaweza kuwa na uvumilivu kama wa nabii ruthi aliyekuwa anawaombea msamaha watu wa sodoma mara kibao huyu?
Labda ungesema alikuwa upande wa waharifu wa sodoma na gomora.


Hapo ndo sifa zake zilipo.
 
Huyu muongo anaesingizia watu wa tume kukutana na Raisi hawezi hata kidogo kuwa na roho ya kuwa yohana mbatizaji,
Tafadhali iondie hiyo hadhi kwake, mtu snitch leo awe kama yohana?


Alisema tuache makinikia yaende bila kujiridhisha kuna nini na badae akawa anawaibia data Accacia halafu useme ana umungu ndani yake?


Anaweza kuwa na uvumilivu kama wa nabii ruthi aliyekuwa anawaombea msamaha watu wa sodoma mara kibao huyu?
Labda ungesema alikuwa upande wa waharifu wa sodoma na gomora.


Hapo ndo sifa zake zilipo.


Huwezi elewa mambo makubwa na magumu. Itachukua vizazi vyako vinne kuelewa mambo hayo
 
Back
Top Bottom