Lissu: Mtu/Watu wenye nguvu walipanga kuniua kwa namna ambayo ingekuwa fundisho kwa wengine

Mtini

Mtini

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2011
Messages
1,051
Likes
1,146
Points
280
Mtini

Mtini

JF-Expert Member
Joined Apr 28, 2011
1,051 1,146 280
Hakuna njia nzuri ya kufahamu una marafiki kiasi gani au una maadui kiasi gani kama ukiwa na shida na hasa ukiwa na shida ambayo si ya bahati mbaya.

Kuna shida ambazo ni za bahati mbaya na kuna nyingine ni za kutengenezwa kabisa. Watu wanakaa wanapanga wakutengenezee shida fulani. Kwangu mimi somo kubwa la hii miezi 16 ni hilo.

Nimeweza kufahamu nimegusa maisha ya watu kiasi gani. Nimeendelea kujifunza kuna watu kiasi gani ambao wangefurahi sana kama nisingekuwa kwenye dunia hii. Na hii story bado ina unflod.

Nimegundua kuna mahali nimefanya vitu sawa sawa na pengine kuna mahali nimefanya vitu sio sawa sawa. Nimepigwa risasi ambazo nisingemaliza nusu saa katika hali ya kawaida.

Ukiniangalia hivi unaniona kama Lissu yule wa Bungeni na hakuna namna ya kuwaonesha nyuma ya nguo hizi nikoje lakini ni makovu matupu ya risasi na visu vya hospitalini. Huu mwili umechanwa chanwa sana.

Kushambuliwa kwangu haikuwa ajali, haikuwa bahati mbaya. Kuna watu walikaa mahali wakaamua huyu Tundu Lissu stahili yake afe na afe kwa namna ambayo itatoa fundisho kwa akina Lissu wengine na wanaofikiria kuwa yeye.

Walipanga nife saa 7 mchana katikati ya vipindi vya Bunge. Wakatuma watu wa kuja kutekeleza hivyo ndio maana nasema haya si mazingira ya kawaida.

Baada ya kutengeneza huo mpango wao kelele ilikuwa kubwa sana juu ya matibabu yangu na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu alisema Dada Alice(mke wangu) tunaomba uandike barua ya maombi na Spika naye akasema tunawasiliana na familia tunahitaji tu waandike maombi ili utaratibu wa sisi kulipa gharama ufanyike.

Tuna barua 5 toka Bungeni kuhusu matibabu. Ya mwisho inasema Bunge haliwezi kulipa gharama sababu kwanza hakuna barua ya kibali cha madaktari watatu toka Muhimbili, hakuna kibali cha K/Mkuu Afya na tatu hakuna kibali cha Rais cha kuidhinisha malipo.

Bunge lililipia gharama za matibabu ya Samwel Sitta ambaye hakuwa Mbunge kwa wakati ule lakini alituma email ya maombi ya kutibiwa na akalipiwa. Mimi niliyepigwa risasi nikiwa natoka kuchangia Bungeni nimepewa majibu kama hayo.

Eneo nililopigiwa risasi ile siku hakukuwa na ulinzi. Ni mtu mwenye nguvu kiasi gani anaweza kutoa amri ya ulinzi kutolewa mahali wanapoishi viongozi wa juu ikiwemo Mawaziri? Someone very powerful wanted me dead.

Rais Magufuli anavyopenda Televisheni lakini tangu 07.09.2019 hajawahi kutaja hata jina Tundu Lissu. Kuna katweet kamoja kanatembea sana ila siamini kama ni ya Magufuli. Ile ni ya Gerson Msigwa.

Someone ambaye sitilii shaka maneno yake aliniambia the order was akifa, hakuna shughuli Bungeni na msimlete Dar mkimbizeni kijijini mkamzike as soon as possible. Nahofia kutaja majina ila kuna siku nitayataja. Itakapokuwa salama kwao, si kwangu maana mimi ni survivor wa 16 bullets.
 
M

masluphill

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2012
Messages
332
Likes
89
Points
45
M

masluphill

JF-Expert Member
Joined Jul 4, 2012
332 89 45
Ifike Muda Lissu ukubali kwamba unajichanganya katika maelezo, pili ujue kuna mamlaka za dunia ambazo Mungu alisema tuziheshimu pia, hivo kelele hazisaidii kitu unatapatapa tu kama mtu aliyekosa la kushikilia, hapa tulia najua BAVICHA hawautaki ukweli huu,

Hakuna cha ICC

Hakuna cha BBC kukusaidia

Hakuna cha Mshahara wako

Hakuna cha huruma ya watanzania wanaojielewa, maana walipoanza kukuhurumia ukahisi una right ya kuhurumiwa na ukaitumia vibaya
MUNGU kasema tuziheshimu mamlaka za Duniani katika HAKI na sio katika UFIRAHUNI,
Nitakupa mifano ya watu wa MUNGU waliopingana na mamlaka za kidunia katika ufirahuni na MUNGU akawa upande wao,
1/ Daniel mtumishi wa MUNGU aligoma kusujudia sanamu la mfalme,hii ilikuwa amri ya utawala lakini DANIEL aligoma kuifuata na alipotupwa kwenye TUNDU la simba wenye Njaa ili wamtafune na kumuangamiza Kwa namna ya kustaajabisha ( kama tukio la T.A.L) MUNGU almlinda na simba wenye njaa hawakumdhuru.
2/ Musa mtumishi wa MUNGU alipodai kuwachukua Watu wake Misri ili waende Kaanani Mamlaka za FIRAHUNI ilitoa aamri ya kutoruhusu waondoke na Katika moambano huo MUNGU alikuwa upanxe wa Musa na akashinda.
3/ Mamajusi walipo pewa Amri ya kuleta Taarifa za mtoto YESU kwa HERODE akiwa na DHAMIRA OVU. MUNGU alituma ujumbe kwao waepuke kupeleka taarifa za YESU kwa kuwa HERODE alikuwa na nia ovu na MUNGU alikuwa upande Mama jusi.
Sasa wewe kupendezeshwa na uovu na kuushabikia ni UJINGA WAKO TU.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MKANDAHARI

MKANDAHARI

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2011
Messages
2,397
Likes
2,111
Points
280
MKANDAHARI

MKANDAHARI

JF-Expert Member
Joined Apr 7, 2011
2,397 2,111 280
Sijui hizi likes 18 umezipata wapi!
Ifike Muda Lissu ukubali kwamba unajichanganya katika maelezo, pili ujue kuna mamlaka za dunia ambazo Mungu alisema tuziheshimu pia, hivo kelele hazisaidii kitu unatapatapa tu kama mtu aliyekosa la kushikilia, hapa tulia najua BAVICHA hawautaki ukweli huu,

Hakuna cha ICC

Hakuna cha BBC kukusaidia

Hakuna cha Mshahara wako

Hakuna cha huruma ya watanzania wanaojielewa, maana walipoanza kukuhurumia ukahisi una right ya kuhurumiwa na ukaitumia vibaya
 
Omusolopogasi

Omusolopogasi

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2017
Messages
972
Likes
1,698
Points
180
Omusolopogasi

Omusolopogasi

JF-Expert Member
Joined Aug 31, 2017
972 1,698 180
Maandiko yanasema, amtegemeae mwanadamu ni mpumbavu. Mimi namtegemea Mungu.
Utajuaje kama mbinguni itatolewa nani kafa kaja na ushaidi huo?

Wakati huu siyo wa kumtegemea mungu ukiona wenzio wananyolewa tia maji za kwako!

wakati ukuta.
 
N

Ninaweza

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2010
Messages
8,441
Likes
2,069
Points
280
N

Ninaweza

JF-Expert Member
Joined Dec 14, 2010
8,441 2,069 280
mtwa mkulu

mtwa mkulu

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2013
Messages
2,644
Likes
674
Points
280
mtwa mkulu

mtwa mkulu

JF-Expert Member
Joined Sep 11, 2013
2,644 674 280
M
Akiupata watu tutashukuru
Mabedui wataingilia chaguzi zetu na kumpitisha kibabe...

.mtashangilia sana kwakuwa kwa fikra zenu finyu mnadhani adui yenu ni CCM.......
Haita pita miaka miwili mtalua kilio cha kusaga Mawe...... Mambo kama Escrow yatatajwa kwenu...... Nanyi mtaanza kupandana madume kwa madume...... Hata kule shuleni masomo yatasimama kwanza kupisha zoezi la kuzalishana hata ukomo wa uraisi utaondolewa asemavyo mfalme wenu!
Hapo afrika itakuwa sare sare nchi zote zitafanana iwe furaha kwa Mabedui
 
K

kabombe

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2011
Messages
19,755
Likes
11,969
Points
280
K

kabombe

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2011
19,755 11,969 280
Samweli Sitta aliugua akiwa ameshamaliza kipindi chake cha ubunge. Akajipeleka mwenyewe Ujerumani kujitibia, akiwa kule akapungukiwa fedha. Akaandika barua serikalini kuomba msaada. Serikali ikakubali na kumlipia matibabu yote. Hakuhitaji barua ya rufaa ya Muhimbili, hakuhitaji ruhusa ya Katibu Mkuu, hakuhitaji kibali cha Rais.
Lissu yupo tayari kukosa utu ili tu afikie malengo yake
Kosa kumtaja marehemu ambaye hawezi kujitetea ili ujinufaishe kisiasa
Lissu sasa anaelekea kuishiwa maneno,kukosa kulipiwa matibabu imekua ajenda yake,chadema mwambie kua mlikataa asiguswe kabisa na serikali watammalizia kumuua
 
K

Kalamu1

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2018
Messages
1,526
Likes
1,917
Points
280
K

Kalamu1

JF-Expert Member
Joined Jul 7, 2018
1,526 1,917 280
Ifike Muda Lissu ukubali kwamba unajichanganya katika maelezo, pili ujue kuna mamlaka za dunia ambazo Mungu alisema tuziheshimu pia, hivo kelele hazisaidii kitu unatapatapa tu kama mtu aliyekosa la kushikilia, hapa tulia najua BAVICHA hawautaki ukweli huu,

Hakuna cha ICC

Hakuna cha BBC kukusaidia

Hakuna cha Mshahara wako

Hakuna cha huruma ya watanzania wanaojielewa, maana walipoanza kukuhurumia ukahisi una right ya kuhurumiwa na ukaitumia vibaya
Britanicca?
Michango ya namna hii nilidhani iko chini ya hadhi yako! CCM ya Mwalimu? Sidhani!
 
britanicca

britanicca

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2015
Messages
9,458
Likes
13,887
Points
280
britanicca

britanicca

JF-Expert Member
Joined May 20, 2015
9,458 13,887 280
Britanicca?
Michango ya namna hii nilidhani iko chini ya hadhi yako! CCM ya Mwalimu? Sidhani!
mkuu usemalo kweli si lazima nichangie kumfurahisha mtu ila nachangia mawazo ninayoona yanaweza kuwapa wtu direcion, Lissu anatengeneza bomu kubwa la kulipukia nyumbani kwake bila kujua, yeye anadhani huko BBC au kwingine atapata msaada hapana, yataisha kama ya KYAGULANI SENTAMU na atarudi kwake tu hapa na si lazima impact aipate atuapo nchini yaweza pita hata miaka miwili au mitatu kabisa ndo ataanza kulialize kwamba he was right but using wrong approach
 
K

Kalamu1

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2018
Messages
1,526
Likes
1,917
Points
280
K

Kalamu1

JF-Expert Member
Joined Jul 7, 2018
1,526 1,917 280
mkuu usemalo kweli si lazima nichangie kumfurahisha mtu ila nachangia mawazo ninayoona yanaweza kuwapa wtu direcion, Lissu anatengeneza bomu kubwa la kulipukia nyumbani kwake bila kujua, yeye anadhani huko BBC au kwingine atapata msaada hapana, yataisha kama ya KYAGULANI SENTAMU na atarudi kwake tu hapa na si lazima impact aipate atuapo nchini yaweza pita hata miaka miwili au mitatu kabisa ndo ataanza kulialize kwamba he was right but using wrong approach
Unajua huwezi kuchangia kunifurahisha mimi kwa lolote kwa sababu nina mawazo huru kabisa, hilo moja.

Unaposema Lissu "anatengeneza bomu kubwa la kulipukia nyumbani bila kujua------". Unajua wazi sio kweli. Wanaotengeneza bomu ni hao unaowapigia vigelegele, kwa sababu unazozijua mwenyewe unaona ni rahisi kuhamishia shutuma kwa mtu ambaye tayari amekwishalipukiwa na bomu, na kwa kudra za Mwenyezi Mungu akabaki salama.

Kama bado kuna watu ambao walikuwa hawajaweka msimamo kuhusu jambo hili kiasi kwamba na wewe ikakulazimu uliwekee msisitizo ili wakubali hayo mnayoyasema juu ya ziara za Tundu Lissu, sidhani kuna watu wengi wa aina hiyo. Sana sana ni kuendeleza vigelegele kwa hao ambao akili zao zilishachotwa toka mwanzo.
 
Polite

Polite

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2011
Messages
2,654
Likes
736
Points
280
Polite

Polite

JF-Expert Member
Joined Apr 12, 2011
2,654 736 280
mtamkumbuka dhaifu.

watu msio kua na shukrani
 
J

Jozi 1

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2015
Messages
5,779
Likes
2,913
Points
280
J

Jozi 1

JF-Expert Member
Joined Aug 16, 2015
5,779 2,913 280
Hakuna njia nzuri ya kufahamu una marafiki kiasi gani au una maadui kiasi gani kama ukiwa na shida na hasa ukiwa na shida ambayo si ya bahati mbaya.

Kuna shida ambazo ni za bahati mbaya na kuna nyingine ni za kutengenezwa kabisa. Watu wanakaa wanapanga wakutengenezee shida fulani. Kwangu mimi somo kubwa la hii miezi 16 ni hilo.

Nimeweza kufahamu nimegusa maisha ya watu kiasi gani. Nimeendelea kujifunza kuna watu kiasi gani ambao wangefurahi sana kama nisingekuwa kwenye dunia hii. Na hii story bado ina unflod.

Nimegundua kuna mahali nimefanya vitu sawa sawa na pengine kuna mahali nimefanya vitu sio sawa sawa. Nimepigwa risasi ambazo nisingemaliza nusu saa katika hali ya kawaida.

Ukiniangalia hivi unaniona kama Lissu yule wa Bungeni na hakuna namna ya kuwaonesha nyuma ya nguo hizi nikoje lakini ni makovu matupu ya risasi na visu vya hospitalini. Huu mwili umechanwa chanwa sana.

Kushambuliwa kwangu haikuwa ajali, haikuwa bahati mbaya. Kuna watu walikaa mahali wakaamua huyu Tundu Lissu stahili yake afe na afe kwa namna ambayo itatoa fundisho kwa akina Lissu wengine na wanaofikiria kuwa yeye.

Walipanga nife saa 7 mchana katikati ya vipindi vya Bunge. Wakatuma watu wa kuja kutekeleza hivyo ndio maana nasema haya si mazingira ya kawaida.

Baada ya kutengeneza huo mpango wao kelele ilikuwa kubwa sana juu ya matibabu yangu na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu alisema Dada Alice(mke wangu) tunaomba uandike barua ya maombi na Spika naye akasema tunawasiliana na familia tunahitaji tu waandike maombi ili utaratibu wa sisi kulipa gharama ufanyike.

Tuna barua 5 toka Bungeni kuhusu matibabu. Ya mwisho inasema Bunge haliwezi kulipa gharama sababu kwanza hakuna barua ya kibali cha madaktari watatu toka Muhimbili, hakuna kibali cha K/Mkuu Afya na tatu hakuna kibali cha Rais cha kuidhinisha malipo.

Bunge lililipia gharama za matibabu ya Samwel Sitta ambaye hakuwa Mbunge kwa wakati ule lakini alituma email ya maombi ya kutibiwa na akalipiwa. Mimi niliyepigwa risasi nikiwa natoka kuchangia Bungeni nimepewa majibu kama hayo.

Eneo nililopigiwa risasi ile siku hakukuwa na ulinzi. Ni mtu mwenye nguvu kiasi gani anaweza kutoa amri ya ulinzi kutolewa mahali wanapoishi viongozi wa juu ikiwemo Mawaziri? Someone very powerful wanted me dead.

Rais Magufuli anavyopenda Televisheni lakini tangu 07.09.2019 hajawahi kutaja hata jina Tundu Lissu. Kuna katweet kamoja kanatembea sana ila siamini kama ni ya Magufuli. Ile ni ya Gerson Msigwa.

Someone ambaye sitilii shaka maneno yake aliniambia the order was akifa, hakuna shughuli Bungeni na msimlete Dar mkimbizeni kijijini mkamzike as soon as possible. Nahofia kutaja majina ila kuna siku nitayataja. Itakapokuwa salama kwao, si kwangu maana mimi ni survivor wa 16 bullets.
Ninayaangalia malalamiko ya Lissu kuwa serikali imejaribu kumuua kwa risasi anayoyatoa huko Marekani.

Nikiiangalia historia ya Marekani na msimamo wa nchi hiyo kwa mauaji ya wanasiasa na wanahabari wenye misimamo mikali sidhani kama ni jambo la kushangaza au kushtusha sana kwao.

1. Wameua kwa risasi wanasiasa wao wengi na hata Marais wake. Ulinzi mkali wa rais wa Marekani ni dhidi ya vitisho vya ndani kuliko vya nje.

2. Marekani imewaua wanasiasa na marais wengi wa nchi za nje na kupindua serikali zao..au kuunda vita.

3. Hadi leo Trump, rais wa Marekani amegoma kabisa kutoa msimamo dhidi ya kuchinjwa kwa mwanahabari Kashoghi na serikali ya Saudi Arabia.

Haya mambo yananipa mawazo ya jinsi serikali hiyo itakavyochulia shambulizi la risasi dhidi ya Lissu.

Jamaa watanyanyuka kama nyati aliyejeruhiwa pale tu JPM atakapogusa maslahi yao ya kiuchumi na maliasili.
Hapo yatamkuta ya Maduro.
 
kbosho

kbosho

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2012
Messages
12,608
Likes
3,445
Points
280
kbosho

kbosho

JF-Expert Member
Joined Jun 4, 2012
12,608 3,445 280
Aiseee..... Kwenye hii dunia kuna watu wenye roho ngumu.
 
Forum statistics

Threads 1,262,489
Members 485,588
Posts 30,123,691