Lissu: Mtu/Watu wenye nguvu walipanga kuniua kwa namna ambayo ingekuwa fundisho kwa wengine


Mtini

Mtini

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2011
Messages
1,051
Likes
1,146
Points
280
Mtini

Mtini

JF-Expert Member
Joined Apr 28, 2011
1,051 1,146 280
Hakuna njia nzuri ya kufahamu una marafiki kiasi gani au una maadui kiasi gani kama ukiwa na shida na hasa ukiwa na shida ambayo si ya bahati mbaya.

Kuna shida ambazo ni za bahati mbaya na kuna nyingine ni za kutengenezwa kabisa. Watu wanakaa wanapanga wakutengenezee shida fulani. Kwangu mimi somo kubwa la hii miezi 16 ni hilo.

Nimeweza kufahamu nimegusa maisha ya watu kiasi gani. Nimeendelea kujifunza kuna watu kiasi gani ambao wangefurahi sana kama nisingekuwa kwenye dunia hii. Na hii story bado ina unflod.

Nimegundua kuna mahali nimefanya vitu sawa sawa na pengine kuna mahali nimefanya vitu sio sawa sawa. Nimepigwa risasi ambazo nisingemaliza nusu saa katika hali ya kawaida.

Ukiniangalia hivi unaniona kama Lissu yule wa Bungeni na hakuna namna ya kuwaonesha nyuma ya nguo hizi nikoje lakini ni makovu matupu ya risasi na visu vya hospitalini. Huu mwili umechanwa chanwa sana.

Kushambuliwa kwangu haikuwa ajali, haikuwa bahati mbaya. Kuna watu walikaa mahali wakaamua huyu Tundu Lissu stahili yake afe na afe kwa namna ambayo itatoa fundisho kwa akina Lissu wengine na wanaofikiria kuwa yeye.

Walipanga nife saa 7 mchana katikati ya vipindi vya Bunge. Wakatuma watu wa kuja kutekeleza hivyo ndio maana nasema haya si mazingira ya kawaida.

Baada ya kutengeneza huo mpango wao kelele ilikuwa kubwa sana juu ya matibabu yangu na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu alisema Dada Alice(mke wangu) tunaomba uandike barua ya maombi na Spika naye akasema tunawasiliana na familia tunahitaji tu waandike maombi ili utaratibu wa sisi kulipa gharama ufanyike.

Tuna barua 5 toka Bungeni kuhusu matibabu. Ya mwisho inasema Bunge haliwezi kulipa gharama sababu kwanza hakuna barua ya kibali cha madaktari watatu toka Muhimbili, hakuna kibali cha K/Mkuu Afya na tatu hakuna kibali cha Rais cha kuidhinisha malipo.

Bunge lililipia gharama za matibabu ya Samwel Sitta ambaye hakuwa Mbunge kwa wakati ule lakini alituma email ya maombi ya kutibiwa na akalipiwa. Mimi niliyepigwa risasi nikiwa natoka kuchangia Bungeni nimepewa majibu kama hayo.

Eneo nililopigiwa risasi ile siku hakukuwa na ulinzi. Ni mtu mwenye nguvu kiasi gani anaweza kutoa amri ya ulinzi kutolewa mahali wanapoishi viongozi wa juu ikiwemo Mawaziri? Someone very powerful wanted me dead.

Rais Magufuli anavyopenda Televisheni lakini tangu 07.09.2019 hajawahi kutaja hata jina Tundu Lissu. Kuna katweet kamoja kanatembea sana ila siamini kama ni ya Magufuli. Ile ni ya Gerson Msigwa.

Someone ambaye sitilii shaka maneno yake aliniambia the order was akifa, hakuna shughuli Bungeni na msimlete Dar mkimbizeni kijijini mkamzike as soon as possible. Nahofia kutaja majina ila kuna siku nitayataja. Itakapokuwa salama kwao, si kwangu maana mimi ni survivor wa 16 bullets.
 
Nyange

Nyange

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2010
Messages
3,121
Likes
1,068
Points
280
Nyange

Nyange

JF-Expert Member
Joined Mar 25, 2010
3,121 1,068 280
Naona makamanda wanachungulia tu halafu wanasepa. Yericko Nyerere alisema Lissu leo amepata mwaliko kuhutubia chuo kikuu cha Maryland. Kumbe chuo kipo magogoni? Ha ha ha, nilikua sijui.
Hiyo Avatar uibadili , make haiendani na ujasiri wa mwenye nayo.
 
P

Papa1

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2012
Messages
1,493
Likes
932
Points
280
Age
58
P

Papa1

JF-Expert Member
Joined Apr 21, 2012
1,493 932 280
Mi bado naamini waliotaka kumuua ni Chadema. Lakini, ngoja nitafakari
 
P

Papa1

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2012
Messages
1,493
Likes
932
Points
280
Age
58
P

Papa1

JF-Expert Member
Joined Apr 21, 2012
1,493 932 280
Hivi Chadema waliwezaje kuondoa ulinzi maeneo yote Yale? Hivi Chadema si ndio walimsindikiza hadi Nairobi? Kwanini hawakuchomoa madrip kwenye ndege akajifia, ile si ilikuwa nafasi ya pekee kukamilisha Mission? Hivi Chadema wanaweza kumshawishi mkuu asitoe kibali cha pesa za matibabu? Hivi hasa Chadema wamepeleka wapi CAMERA ya Kalemani halafu Kalemani akawaacha tu utadhani ni CCM kachukua? Kwanini Tundu Lisu aparamie serikali wakati wasiojulikana ni CHADEMA, huu si ni upotoshaji wa hali ya kiwango cha flyover? Inawezekana mbunge Mollel amekimbia wauwaji kwenda kwa watetezi wa wanyonge eti? Ngoja niendelee kutafakari!
 
Gullam

Gullam

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2013
Messages
4,242
Likes
2,692
Points
280
Gullam

Gullam

JF-Expert Member
Joined Dec 1, 2013
4,242 2,692 280
Daud Arbaty Bashite ndiye alikwenda Dodoma akiambatana na wasiojulika wanne na Le mutuz, jerry muro muro, cyprian Musiba na Heri kisanduku ambaye ndiye alimimina Risasi kwa maelekezo ya Cyprian musiba aliyekuwa na bunduki ndogo yaani bastora
Duh, hukumu yao ipo kabla hawajaonja mauti.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
minyoo

minyoo

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2013
Messages
10,622
Likes
6,182
Points
280
minyoo

minyoo

JF-Expert Member
Joined May 25, 2013
10,622 6,182 280
Hiyo siku ya kuwataja isichelewe, tunaisubiri kwa hamu!
Le mutuz mpaka sasa kafikisha idadi ya waganga wa kienyeji 70 baada ya kuongeza watano toka Africa ya kati ili waje kusaidia kumyamazisha Tundu Lisu ni matumizi mabaya ya pesa za umma
 
minyoo

minyoo

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2013
Messages
10,622
Likes
6,182
Points
280
minyoo

minyoo

JF-Expert Member
Joined May 25, 2013
10,622 6,182 280
Kama mnakumbukumbu, baada ya jiwe kuongea maneno hayo, ndio Mh TL alipopigwa risasi. Sasa nimeanza kuamini kitu. Ila acha tumruhusu Mungu awafunue!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Mtukufu malaika toka chato na Naibu Rais ndugu Daud Arbaty Bashite ndiyo waliomchakaza Tundu kwa Risasi
 
M

manengelo

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2018
Messages
8,828
Likes
13,844
Points
280
M

manengelo

JF-Expert Member
Joined Aug 13, 2018
8,828 13,844 280
Kuna taarifa kwamba ratiba ya mazishi na hotuba zilikwishaandaliwa na Ndugai
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ zimeshakuwa outdated...maskini...!Ndugai yake sijui ndo Tulia ataiandaaπŸ˜‚πŸ˜‚..
 

Forum statistics

Threads 1,262,487
Members 485,588
Posts 30,123,570