Lissu: Mtu/Watu wenye nguvu walipanga kuniua kwa namna ambayo ingekuwa fundisho kwa wengine


Mtini

Mtini

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2011
Messages
1,050
Likes
1,146
Points
280
Mtini

Mtini

JF-Expert Member
Joined Apr 28, 2011
1,050 1,146 280
Hakuna njia nzuri ya kufahamu una marafiki kiasi gani au una maadui kiasi gani kama ukiwa na shida na hasa ukiwa na shida ambayo si ya bahati mbaya.

Kuna shida ambazo ni za bahati mbaya na kuna nyingine ni za kutengenezwa kabisa. Watu wanakaa wanapanga wakutengenezee shida fulani. Kwangu mimi somo kubwa la hii miezi 16 ni hilo.

Nimeweza kufahamu nimegusa maisha ya watu kiasi gani. Nimeendelea kujifunza kuna watu kiasi gani ambao wangefurahi sana kama nisingekuwa kwenye dunia hii. Na hii story bado ina unflod.

Nimegundua kuna mahali nimefanya vitu sawa sawa na pengine kuna mahali nimefanya vitu sio sawa sawa. Nimepigwa risasi ambazo nisingemaliza nusu saa katika hali ya kawaida.

Ukiniangalia hivi unaniona kama Lissu yule wa Bungeni na hakuna namna ya kuwaonesha nyuma ya nguo hizi nikoje lakini ni makovu matupu ya risasi na visu vya hospitalini. Huu mwili umechanwa chanwa sana.

Kushambuliwa kwangu haikuwa ajali, haikuwa bahati mbaya. Kuna watu walikaa mahali wakaamua huyu Tundu Lissu stahili yake afe na afe kwa namna ambayo itatoa fundisho kwa akina Lissu wengine na wanaofikiria kuwa yeye.

Walipanga nife saa 7 mchana katikati ya vipindi vya Bunge. Wakatuma watu wa kuja kutekeleza hivyo ndio maana nasema haya si mazingira ya kawaida.

Baada ya kutengeneza huo mpango wao kelele ilikuwa kubwa sana juu ya matibabu yangu na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu alisema Dada Alice(mke wangu) tunaomba uandike barua ya maombi na Spika naye akasema tunawasiliana na familia tunahitaji tu waandike maombi ili utaratibu wa sisi kulipa gharama ufanyike.

Tuna barua 5 toka Bungeni kuhusu matibabu. Ya mwisho inasema Bunge haliwezi kulipa gharama sababu kwanza hakuna barua ya kibali cha madaktari watatu toka Muhimbili, hakuna kibali cha K/Mkuu Afya na tatu hakuna kibali cha Rais cha kuidhinisha malipo.

Bunge lililipia gharama za matibabu ya Samwel Sitta ambaye hakuwa Mbunge kwa wakati ule lakini alituma email ya maombi ya kutibiwa na akalipiwa. Mimi niliyepigwa risasi nikiwa natoka kuchangia Bungeni nimepewa majibu kama hayo.

Eneo nililopigiwa risasi ile siku hakukuwa na ulinzi. Ni mtu mwenye nguvu kiasi gani anaweza kutoa amri ya ulinzi kutolewa mahali wanapoishi viongozi wa juu ikiwemo Mawaziri? Someone very powerful wanted me dead.

Rais Magufuli anavyopenda Televisheni lakini tangu 07.09.2019 hajawahi kutaja hata jina Tundu Lissu. Kuna katweet kamoja kanatembea sana ila siamini kama ni ya Magufuli. Ile ni ya Gerson Msigwa.

Someone ambaye sitilii shaka maneno yake aliniambia the order was akifa, hakuna shughuli Bungeni na msimlete Dar mkimbizeni kijijini mkamzike as soon as possible. Nahofia kutaja majina ila kuna siku nitayataja. Itakapokuwa salama kwao, si kwangu maana mimi ni survivor wa 16 bullets.
 
GUSSIE

GUSSIE

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2014
Messages
2,240
Likes
4,444
Points
280
GUSSIE

GUSSIE

JF-Expert Member
Joined Dec 2, 2014
2,240 4,444 280
Hivi watu kwa wastani kwa sasa kuna mtu anafikisha miaka hata 100

Maana hawa wanaofikisha miaka 90 sasa mfano Mzee Mwinyi utotoni na ujanani kwao hakukuwa na Baga au kuku wa mwezi mmoja halafu unatafuna

Walikula mavitu ya porini sana hata chumvi au sukari hawakuijua iliishia kwa mkoloni

Sasa mtu ukimuua mwezako halafu una miaka zaidi ya umri uliobakiza kuishi utapata nini?

Hivi ni vichekesho sana, Mtu ukifariki kwanza hakuna anayependa kukaa na wewe unakimbizwa mochwari

Sasa hata magari au elimu au vyeo na majumba vyote unaacha hapa hapa duniani

Ndio maana wengine wakiacha pesa Bank ndugu wanaamua kumuandikia marehemu cheki halafu cash inaendelea kuwepo Bank, Sasa sijui hiyo check ukizikwa nayo utatolea Bank gani pesa
 
Elli

Elli

JF-Expert Member
Joined
Mar 17, 2008
Messages
30,305
Likes
16,071
Points
280
Elli

Elli

JF-Expert Member
Joined Mar 17, 2008
30,305 16,071 280
Prayer for the Man Who Mugged My Father, 72
Charles Harper Webb
May there be an afterlife.

May you meet him there, the same age as you.
May the meeting take place in a small, locked room.

May the bushes where you hid be there again, leaves tipped with razor-
blades and acid.
May the rifle butt you bashed him with be in his hands.
May the glass in his car window, which you smashed as he sat stopped
at a red light, spike the rifle butt, and the concrete on which you’ll
fall.

May the needles the doctors used to close his eye, stab your pupils
every time you hit the wall and then the floor, which will be often.
May my father let you cower for a while, whimpering, “Please don’t
shoot me. Please.”
May he laugh, unload your gun, toss it away;
Then may he take you with bare hands.

May those hands, which taught his son to throw a curve and drive a nail
and hold a frog, feel like cannonballs against your jaw.
May his arms, which powered handstands and made their muscles jump
to please me, wrap your head and grind your face like stone.
May his chest, thick and hairy as a bear’s, feel like a bear’s snapping
your bones.
May his feet, which showed me the flutter kick and carried me miles
through the woods, feel like axes crushing your one claim to man-
hood as he chops you down.

And when you are down, and he’s done with you, which will be soon,
since, even one-eyed, with brain damage, he’s a merciful man,
May the door to the room open and let him stride away to the Valhalla
he deserves.
May you—bleeding, broken—drag yourself upright.

May you think the worst is over;
You’ve survived, and may still win.

Then may the door open once more, and let me in.
 
minyoo

minyoo

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2013
Messages
10,613
Likes
6,181
Points
280
minyoo

minyoo

JF-Expert Member
Joined May 25, 2013
10,613 6,181 280
Nasikia kabla mwili wake haujapoa mwili ulipaswa uwe kijijini..
Jamaa katili sana..
Malipo ni hapahapa.
Bashite na mtukufu malaika toka chato ni sawa na Iddy Amin dada na yule msaidizi wake mnyama aliyeitwa Maliyamungu
 
minyoo

minyoo

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2013
Messages
10,613
Likes
6,181
Points
280
minyoo

minyoo

JF-Expert Member
Joined May 25, 2013
10,613 6,181 280
Unyama wa hali ya juu Sana.
Daud Arbaty Bashite ndiye alikwenda Dodoma akiambatana na wasiojulika wanne na Le mutuz, jerry muro muro, cyprian Musiba na Heri kisanduku ambaye ndiye alimimina Risasi kwa maelekezo ya Cyprian musiba aliyekuwa na bunduki ndogo yaani bastora
 
kwamtoro

kwamtoro

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2010
Messages
4,851
Likes
848
Points
280
kwamtoro

kwamtoro

JF-Expert Member
Joined Nov 15, 2010
4,851 848 280
Daud Arbaty Bashite ndiye alikwenda Dodoma akiambatana na wasiojulika wanne na Le mutuz, jerry muro muro, cyprian Musiba na Heri kisanduku ambaye ndiye alimimina Risasi kwa maelekezo ya Cyprian musiba aliyekuwa na bunduki ndogo yaani bastora
Looohhh!! Hawa jamaa wapo kwenye hali ngumu now.
 

Forum statistics

Threads 1,262,459
Members 485,588
Posts 30,122,935