Lissu kumshtaki rais Kikwete bungeni

Lissu kumshtaki rais Kikwete bungeni

Medical Dictionary

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2012
Posts
1,060
Reaction score
309
MBUNGE wa Singida Mashariki Tundu Lissu (CHADEMA), ambaye pia ni mnadhimu mkuu wa kambi ya upinzani bungeni, amesema anakusudia kuleta hoja binafsi bungeni kumshitaki Rais Jakaya Kikwete kwa madai kuwa amevunja katiba kwa kuteua majaji wasio na sifa. Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini hapa, Lissu alisema anakusudia kufanya hivyo katika Bunge la Februari mwakani baada ya rais kuendelea kuteua majaji wasio na sifa.

Alisema anakusudia kuwasilisha hoja ya kumsitaki rais bungeni kwa kutumia kanuni za kudumu za Bunge sehemu ya 11 na Ibara ya 46A na 46B ya katiba ya sasa kifungu cha 121,122,123,124,125 na 126 ya azimio la kumwondoa rais madarakani. Lissu alisema pamoja na mambo mengine, rais amekuwa kiongozi wa kuvunja katiba ya nchi kwa kiasi kikubwa kwa kitendo chake cha kuendelea kuteua majaji ‘vihiyo'. Aidha, alisema hata kama Bunge litashindwa kufanya maamuzi ya kumwondoa rais madarakani kutokana na uvunjifu wa katiba kwa uteuzi mbovu wa majaji, ataangalia utaratibu wa kumshitaki katika vyombo vya sheria.

Katika hatua nyingine, Lissu alimtaka Spika wa Bunge, Anne Makinda, kusoma ripoti ya Tume ya Ngwilizi iliyokuwa ikimchunguza na kumhoji kwa madai kuwa alitoa kauli ya kuwadhalilisha majaji na kudhalilisha muhimili wa mahakama kwa kile alichosema kuwa, majaji wengi hawafai kwani hawana sifa. Alisema kutokana na kauli yake ya Julai 13, mwaka huu ambayo aliitoa bungeni wakati akiwasilisha hotuba ya Waziri kivuli wa Katiba na Sheria, Lissu aliwataja majaji walioteuliwa na rais kwamba hawana uwezo na sifa za kuwa majaji jambo ambalo lilimfanya Spika Makinda kuunda kamati ya kumshitaki katika Kamati ya Bunge ya Maadili na kinga bungeni ili atoe maelezo na ushahidi.



Source:tanzania daima jumatano 7/11
 
Ni kupoteza tu muda kumshitaki Rais kwenye bunge lenye asilimia 80 ya wabunge kutoka CCM. Yeye apeleke hoja binafsi bungeni kupinga uteuzi wa rais na kutaka utenguliwe lakini si kumshitaki rais mwenyewe. Wabunge wa CCM na njaa zao watakubali anayewalisha aondolewe?
 
Rais wa hii nchi ana madaraka sana..yaani karibia kila mtu anamchagua yeye...warioba inabidi abadilishe vitu vingi sana kwenye hii katiba mpya...Sijawahi ona rais mwenye madaraka mengi kama huyu wa kwetu
 
Huyu dhaifu dawa yake ni the HAGUE 2!
 
Amefikia ukingoni. Na nna uhakika hana jipya.

Kuna kigezo cha kuwa jaji Tanzania? alikianzisha yeye hicho kigezo?

Hata Marehem Mzee Kasiim alikuwa Jaji Tanzania, ana kigezo kipi?

Huyo Tundu Lussu ana kigezo kipi cha kuwa mwana-siasa? Ana shahada ya siasa? aliitowa wapi? Iramba?
 
Hili linaweza kuwa jaribio zuri sana la constitutional process yetu na hapa ndio inaweza kuwa ni vizuri kuona wale waliotaka PM Pinda aondolewe watakuwa tayari kusimama kumshtaki Rais. It'll be very interesting.
 
Kwa upuuzi wa wabunge wa CCM sijui kama itawezekana. Ila ni kwamba atakapoteua tena atakuwa makini kutoteua 'washikaji' kuwa majaji.
 
Kwa mara ya kwanza taifa litashuhudia katiba na sheria ikisimamiwa kumwajibisha mkuu wa nchi!

Njia anayoamua kuifuata Mh Lisu ni nzuri na ina mihemuko mikubwa kwa Rais, japo kuwa ni vigumu kupata matokeo chanya lakini kile kitendo tu cha "rais kushitakiwa" kinatupatia sura ya udhaifu wa rais na serikali yake!

Anaweza kutumia njia "hoja binafsi bungeni kupinga uteuzi wa rais na kutaka utenguliwe"

Hii ina chembe za matokeo chanya, lakini kimuhimili haina uzito, haitupi sura halisi ya udhaifu wa mwenye jamuhuri!

Yote kwa yote nakutakia kilala heri kamanda Lusu!
 
Hana haja ya kufanya hivyo. Asubiri 2015 CDM itakapochukua nchi wawatimue
 
Ilishindikana tu Kumng'oa Waziri mkuu, na sahihi 70 za wabunge zilikwishatimia.Je kwa uraisi itawezekana??? msisahau pia kikatiba raisi anamamlaka ya kulivunja bunge hilohilo.!
 
Zomba,
Hoja zako zingekuwa supported na ibara ndani ya ya Katiba ningekuelewa.Kwani makosa mawili yakifanyika yanafanya jambo kuwa sahihi? Heshima yako inapungua unapotoa hoja zisizo na mashiko.

Sema Mh. Lissu kakosea wapi? Kwa hiyo kwako wewe Rais akimteua Mzee Jangala kuwa Jaji wa Mahakam ya Rufaa sawa tu.
 
Lissu anachodai kina ukweli. Facts zote anazo hata tarehe za kuzaliwa na za kuanza shule za Majaji na hizi facts anazipata humo humo miongoni mwa Majaji, ila naona hii njia ya kupeleka hoja binafsi ya kumng'oa rais haiwezi kufanikiwa.
Kwa nini asipeleke hoja ya kuundwa Tume ya kuchunguza ajira na mienendo ya Majaji kama inavyoendelea nchini kenya kwa sasa? Ikigindulika jaji alidanganya elimu , tarehe ya kuzaliwa kwake au kujihusisha na vitendo vya rushwa au kapendelewa katika uteuzi ambao hastahili anang'oka.
 
Amefikia ukingoni. Na nna uhakika hana jipya.

Kuna kigezo cha kuwa jaji Tanzania? alikianzisha yeye hicho kigezo?

Hata Marehem Mzee Kasiim alikuwa Jaji Tanzania, ana kigezo kipi?

Huyo Tundu Lussu ana kigezo kipi cha kuwa mwana-siasa? Ana shahada ya siasa? aliitowa wapi? Iramba?
You need sanity check up!
 
Godwinnko Ulimbukeni sana,,huyu na mwenzake zitto ni machakubimbi sana
sasa kama ana nia hiyo ya kupeleka huo muswada feb next yr anatutangazia sisi ili iweje?
Kama sio kutafuta umaarafu usio na msingi,kama nia hiyo anayo na hilo suala lipo kisheria za bunge na ni haki yake asubiri muda ukifika aiwasilishe,,sasa anapofikia kututangazia ana chelea nin,tumpgie vigere gere au?
Na huyo mwenzake kabwela kila siku nitataja nitataja,,sasa si utaje hayo majina??mbona slaa aliyataja pale mwembe yanga??
Wanakera sana
 
Last edited by a moderator:
For the SAKE of reckords go go goo honorauble Tundu Lissu. Hii itaingia kwenye hansard za Bunge and it can serve as wake up call wakati tunapotengeneza katiba mpya.

I fully support the idea.
 
ulimbukeni sana,,huyu na mwenzake zitto ni machakubimbi sana
sasa kama ana nia hiyo ya kupeleka huo muswada feb next yr anatutangazia sisi ili iweje?
Kama sio kutafuta umaarafu usio na msingi,kama nia hiyo anayo na hilo suala lipo kisheria za bunge na ni haki yake asubiri muda ukifika aiwasilishe,,sasa anapofikia kututangazia ana chelea nin,tumpgie vigere gere au?
Na huyo mwenzake kabwela kila siku nitataja nitataja,,sasa si utaje hayo majina??mbona slaa aliyataja pale mwembe yanga??
Wanakera sana

Is this the best you can do ???????
It's sad. watu wanatembea barabarani unadhani wazima, kumbe wagonjwa wa akili, same applies to zomba (see cooment no.5 above)
 
Hili ndilo tatizo la kuchagua raisi asiyejua katiba ni nini, anadhani mradi yeye ni raisi basi ni sawa na Sultani/mfalme. Na hivyo ni haki yake kugawa madaraka kwa marafiki zake bila hata kuangalia kama wana uwezo na kama katiba inamruhusu.
He doesn't even consult his lawyers, na mara nyingine anachagua hata wezi na watu wenye makosa ya jinai ktk nafasi nyeti bila kutafiti background ya wateuliwa wake. Halafu wadhaifu wa akili wanadiriki kutetea upuuzi anaoufanya!
 
Watanzani tuwe wazalendo.Hongera Tundu Lissu!
 
Back
Top Bottom