Lissu kumshtaki rais Kikwete bungeni

Lissu kumshtaki rais Kikwete bungeni

MBUNGE wa Singida Mashariki Tundu Lissu (CHADEMA), ambaye pia ni mnadhimu mkuu wa kambi ya upinzani bungeni, amesema anakusudia kuleta hoja binafsi bungeni kumshitaki Rais Jakaya Kikwete kwa madai kuwa amevunja katiba kwa kuteua majaji wasio na sifa. Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini hapa, Lissu alisema anakusudia kufanya hivyo katika Bunge la Februari mwakani baada ya rais kuendelea kuteua majaji wasio na sifa.

Alisema anakusudia kuwasilisha hoja ya kumsitaki rais bungeni kwa kutumia kanuni za kudumu za Bunge sehemu ya 11 na Ibara ya 46A na 46B ya katiba ya sasa kifungu cha 121,122,123,124,125 na 126 ya azimio la kumwondoa rais madarakani. Lissu alisema pamoja na mambo mengine, rais amekuwa kiongozi wa kuvunja katiba ya nchi kwa kiasi kikubwa kwa kitendo chake cha kuendelea kuteua majaji ‘vihiyo’. Aidha, alisema hata kama Bunge litashindwa kufanya maamuzi ya kumwondoa rais madarakani kutokana na uvunjifu wa katiba kwa uteuzi mbovu wa majaji, ataangalia utaratibu wa kumshitaki katika vyombo vya sheria.

Katika hatua nyingine, Lissu alimtaka Spika wa Bunge, Anne Makinda, kusoma ripoti ya Tume ya Ngwilizi iliyokuwa ikimchunguza na kumhoji kwa madai kuwa alitoa kauli ya kuwadhalilisha majaji na kudhalilisha muhimili wa mahakama kwa kile alichosema kuwa, majaji wengi hawafai kwani hawana sifa. Alisema kutokana na kauli yake ya Julai 13, mwaka huu ambayo aliitoa bungeni wakati akiwasilisha hotuba ya Waziri kivuli wa Katiba na Sheria, Lissu aliwataja majaji walioteuliwa na rais kwamba hawana uwezo na sifa za kuwa majaji jambo ambalo lilimfanya Spika Makinda kuunda kamati ya kumshitaki katika Kamati ya Bunge ya Maadili na kinga bungeni ili atoe maelezo na ushahidi.

Source:tanzania daima jumatano 7/11

Lissu, kama huna hoja ya kuongea bungeni bora ukakae kimya. Kama vp tuandamane!!!!!!!!!!
 
Rais wa hii nchi ana madaraka sana..yaani karibia kila mtu anamchagua yeye...warioba inabidi abadilishe vitu vingi sana kwenye hii katiba mpya...Sijawahi ona rais mwenye madaraka mengi kama huyu wa kwetu

Jiandae nawe siku si nyingi utachaguliwa na Mhe. Rais, vp utakubali?????????
 
Lissu, kama huna hoja ya kuongea bungeni bora ukakae kimya. Kama vp tuandamane!!!!!!!!!!

'Join Date : 6th November 2012'
Posts : 9

Uandamane kwenda wapi ilhal hujui uendako.
 
Zomba Zomba Zomba,Comment yako inatia mashaka uelewa wako wa mambo,Siasa mpaka Degree ya Siasa? Nyererer alikuwa na degree ya Siasa? Yet he was Role model of all Politician in TZ and Africa!

Role model wa kutuingiza kwenye umaskini wa mwisho duniani?
 
Amefikia ukingoni. Na nna uhakika hana jipya. Kuna kigezo cha kuwa jaji Tanzania? alikianzisha yeye hicho kigezo? Hata Marehem Mzee Kasiim alikuwa Jaji Tanzania, ana kigezo kipi? Huyo Tundu Lussu ana kigezo kipi cha kuwa mwana-siasa? Ana shahada ya siasa? aliitowa wapi? Iramba?
Lissu ametaja vifungu vya katiba ambavyo vimevunjwa, sasa wewe unapouliza kuhusu vitego una maana gani? afadhali ungekaa kimya ungeweza kuficha upuuzi wako. Siyo lazima uchangie humu kama hujajiandaa kuchangia.
 
Kwa upuuzi wa wabunge wa CCM sijui kama itawezekana. Ila ni kwamba atakapoteua tena atakuwa makini kutoteua 'washikaji' kuwa majaji.

Lakini habari zitakuwa zimefika (message sent)
 
Zomba,
Hoja zako zingekuwa supported na ibara ndani ya ya Katiba ningekuelewa.Kwani makosa mawili yakifanyika yanafanya jambo kuwa sahihi? Heshima yako inapungua unapotoa hoja zisizo na mashiko.

Sema Mh. Lissu kakosea wapi? Kwa hiyo kwako wewe Rais akimteua Mzee Jangala kuwa Jaji wa Mahakam ya Rufaa sawa tu.

Mkuu vifungu hivyo hapo
Kwa kutumia Kanuni ya Bunge sehemu ya 11, Ibara ya 121, 122, 123, 124, 125 na 126 na pia kwa kutumia Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ibara ya 146 A.
Sehemu ya 11 ya Kanuni ya Bunge, Ibara ya 121 inaeleza kuwa mbunge yeyote anaweza kuwasilisha kwa Spika taarifa ya hoja ya kumshtaki Rais kwa madhumuni ya kumwondoa Rais madarakani kupitia azimio la Bunge kwa mujibu wa Ibara ya 146 A ya Katiba ikiwa kwamba Rais; ametenda vitendo ambavyo kwa jumla vinavunja katiba au sheria ya maadili ya viongozi wa umma.
anatakiwa kukusanya saini za wabunge kuunga mkono hoja yake ambayo ni asilimia 20 kwa mujibu wa Kanuni za Bunge. Wabunge wote kikatiba ni 357.
 
Lissu ametaja vifungu vya katiba ambavyo vimevunjwa, sasa wewe unapouliza kuhusu vitego una maana gani? afadhali ungekaa kimya ungeweza kuficha upuuzi wako. Siyo lazima uchangie humu kama hujajiandaa kuchangia.

Katiba hiyo hiyo isiyofaa inayobadilishwa?
 
MBUNGE wa Singida Mashariki Tundu Lissu (CHADEMA), ambaye pia ni mnadhimu mkuu wa kambi ya upinzani bungeni, amesema anakusudia kuleta hoja binafsi bungeni kumshitaki Rais Jakaya Kikwete kwa madai kuwa amevunja katiba kwa kuteua majaji wasio na sifa. Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini hapa, Lissu alisema anakusudia kufanya hivyo katika Bunge la Februari mwakani baada ya rais kuendelea kuteua majaji wasio na sifa.

Alisema anakusudia kuwasilisha hoja ya kumsitaki rais bungeni kwa kutumia kanuni za kudumu za Bunge sehemu ya 11 na Ibara ya 46A na 46B ya katiba ya sasa kifungu cha 121,122,123,124,125 na 126 ya azimio la kumwondoa rais madarakani. Lissu alisema pamoja na mambo mengine, rais amekuwa kiongozi wa kuvunja katiba ya nchi kwa kiasi kikubwa kwa kitendo chake cha kuendelea kuteua majaji ‘vihiyo’. Aidha, alisema hata kama Bunge litashindwa kufanya maamuzi ya kumwondoa rais madarakani kutokana na uvunjifu wa katiba kwa uteuzi mbovu wa majaji, ataangalia utaratibu wa kumshitaki katika vyombo vya sheria.

Katika hatua nyingine, Lissu alimtaka Spika wa Bunge, Anne Makinda, kusoma ripoti ya Tume ya Ngwilizi iliyokuwa ikimchunguza na kumhoji kwa madai kuwa alitoa kauli ya kuwadhalilisha majaji na kudhalilisha muhimili wa mahakama kwa kile alichosema kuwa, majaji wengi hawafai kwani hawana sifa. Alisema kutokana na kauli yake ya Julai 13, mwaka huu ambayo aliitoa bungeni wakati akiwasilisha hotuba ya Waziri kivuli wa Katiba na Sheria, Lissu aliwataja majaji walioteuliwa na rais kwamba hawana uwezo na sifa za kuwa majaji jambo ambalo lilimfanya Spika Makinda kuunda kamati ya kumshitaki katika Kamati ya Bunge ya Maadili na kinga bungeni ili atoe maelezo na ushahidi.

Source:tanzania daima jumatano 7/11
Mhe. Tundu Lisu nadhani hata Ubunge CDM si mahali pake labda akagombee uongozi kijijini kwake alikozaliwa ndo aanze kupanda vyeo
 
MBUNGE wa Singida Mashariki Tundu Lissu (CHADEMA), ambaye pia ni mnadhimu mkuu wa kambi ya upinzani bungeni, amesema anakusudia kuleta hoja binafsi bungeni kumshitaki Rais Jakaya Kikwete kwa madai kuwa amevunja katiba kwa kuteua majaji wasio na sifa. Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini hapa, Lissu alisema anakusudia kufanya hivyo katika Bunge la Februari mwakani baada ya rais kuendelea kuteua majaji wasio na sifa.

Alisema anakusudia kuwasilisha hoja ya kumsitaki rais bungeni kwa kutumia kanuni za kudumu za Bunge sehemu ya 11 na Ibara ya 46A na 46B ya katiba ya sasa kifungu cha 121,122,123,124,125 na 126 ya azimio la kumwondoa rais madarakani. Lissu alisema pamoja na mambo mengine, rais amekuwa kiongozi wa kuvunja katiba ya nchi kwa kiasi kikubwa kwa kitendo chake cha kuendelea kuteua majaji ‘vihiyo'. Aidha, alisema hata kama Bunge litashindwa kufanya maamuzi ya kumwondoa rais madarakani kutokana na uvunjifu wa katiba kwa uteuzi mbovu wa majaji, ataangalia utaratibu wa kumshitaki katika vyombo vya sheria.

Katika hatua nyingine, Lissu alimtaka Spika wa Bunge, Anne Makinda, kusoma ripoti ya Tume ya Ngwilizi iliyokuwa ikimchunguza na kumhoji kwa madai kuwa alitoa kauli ya kuwadhalilisha majaji na kudhalilisha muhimili wa mahakama kwa kile alichosema kuwa, majaji wengi hawafai kwani hawana sifa. Alisema kutokana na kauli yake ya Julai 13, mwaka huu ambayo aliitoa bungeni wakati akiwasilisha hotuba ya Waziri kivuli wa Katiba na Sheria, Lissu aliwataja majaji walioteuliwa na rais kwamba hawana uwezo na sifa za kuwa majaji jambo ambalo lilimfanya Spika Makinda kuunda kamati ya kumshitaki katika Kamati ya Bunge ya Maadili na kinga bungeni ili atoe maelezo na ushahidi.

Source:tanzania daima jumatano 7/11

Ana malaria Kali Au sugu Huyu. Yaani Rais aliyechaguliwa na Watz wengi yeye anajifanya anaweza kumuamrisha anavyotaka. Nashauri akapimwe Mirembe hosipitali isije ikawa Ana matatizo asiyojijua yeye mwenyewe.
 
Nchi ya kishikaji, Raisi wa kishikaji, uteuzi wa kishikaji, wabunge washikaji, hata akipeleka hoja itaisha kishikaji!!
 
Ana malaria Kali Au sugu Huyu. Yaani Rais aliyechaguliwa na Watz wengi yeye anajifanya anaweza kumuamrisha anavyotaka. Nashauri akapimwe Mirembe hosipitali isije ikawa Ana matatizo asiyojijua yeye mwenyewe.

Ameonyesha vifungu husika vilivyokiukwa, ofcourse rais atalindwa ila ujumbe umefika, majaji vimulugo wamesikia
 
Yup na rais wetu Kikwete anamkiri kama Role Model........

1) Mimi siyo Rais wenu.

2) Msikilize vizuri kwenye hii hotuba, listen between the lines.

President Kikwete addresses Elders in Dar es salaam, TBC ,18/11/2011 - YouTube
 
Chadema imepinga huo msimamo wa lissu,zaidi soma gazeti la nipashe la tarehe 8.11.2012 chama kmesema lissu amekurupuka kwani chama makini hakiwezi kuunga mkono kitu hicho
 
Chadema kimesema mambo yote ya msingi kinachoyaongelea kwenye jamii huwa kinakaa vikao na si kukurupuka
 
Ana malaria Kali Au sugu Huyu. Yaani Rais aliyechaguliwa na Watz wengi yeye anajifanya anaweza kumuamrisha anavyotaka. Nashauri akapimwe Mirembe hosipitali isije ikawa Ana matatizo asiyojijua yeye mwenyewe.

ww acha fikra finyu,sheria zipo ili zingatiwe na hakuna exception kwenye sheria,kama ukikiuka basi sheria zinakubana tu,ww unasema kachaguliwa na watu wengi je ndo iye blanket ya kuficha maovu yake? Kama ndio ulikuwa wapi kulalama wakati lema anaondelewa arusha halihali amechaguliwa na watu wengi wa jimbo lake? Jaribu kuzingatia nafasi ya sheria katika nchi ya kidemokrasia.
 
Back
Top Bottom