Lissu kumshtaki rais Kikwete bungeni

Lissu kumshtaki rais Kikwete bungeni

Huo ndo mwendo, ningependa kila mara kusikia wanasiasa wanamsakama rais mpaka aione ikulu chungu. Rais wetu amejisahau sana
 
is this the best you can do ???????
It's sad. Watu wanatembea barabarani unadhani wazima, kumbe wagonjwa wa akili, same applies to zomba (see cooment no.5 above)

namaanisha kila neno nililoliandika hapa
by the way i am not zomba
 
Watanzania wanapenda maigizo sana. Hii tabia hupelekea watu kuacha hoja nzito na kufuata upepo!!

Swali la kujiuliza ni kwa nini viongozi wa kisiasa wapinzani n.k hawajitokezi katika kutoa elimu juu ya mchakato wa katiba mpya? wananchi wengi wanatoa maoni just kama kutimiza wajibu tu. Kama kweli Lissu and hic co. wana nia ya dhati katika kuleta mabadiliko kwenye katiba kwanini wasingefanya kampeni kubwa kuelelimisha jamii juu ya ubovu na mapengo katika katiba ya sasa?

Tunashanganzwa na M4C, V4C, operation mchaka mchaka, sangara nk, kwanini hizi operation zisihamasishe wananchi kuielewa katiba ya sasa na kutoa maoni mazuri yatakayotupatia katiba mpya itakayokidhi mahitaji ya sasa na baadae?

Badala yake kila kukicha kuanzisha maigizo mapya na kudivert important issues.

SHAME
 
Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu​

SUALA la kuwapo kwa majaji wasiokuwa na sifa nchini limeingia katika sura mpya baada ya Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu kusema atawasilisha hoja ya kumshtaki Rais Jakaya Kikwete kama atashindwa kuwaondoa kazini ifikapo Kikao cha Bunge lijalo. Akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za Bunge jana, Lissu alisema amechukua uamuzi huo baada ya kuona Bunge limeikalia ripoti ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge iliyomhoji kuhusu kauli yake ya kuwatuhumu majaji kuwa baadhi yao hawana sifa.
Alisema ameamua kuchukua hatua hiyo baada ya kuona Rais Kikwete ambaye ana mamlaka ya kuteua majaji, ameshindwa kuwaondoa kazini majaji hao wasiokuwa na sifa.

Lissu alisema atawasilisha hoja yake hiyo kwa kutumia Kanuni ya Bunge sehemu ya 11, Ibara ya 121, 122, 123, 124, 125 na 126 na pia kwa kutumia Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ibara ya 146 A. Sehemu ya 11 ya Kanuni ya Bunge, Ibara ya 121 inaeleza kuwa mbunge yeyote anaweza kuwasilisha kwa Spika taarifa ya hoja ya kumshtaki Rais kwa madhumuni ya kumwondoa Rais madarakani kupitia azimio la Bunge kwa mujibu wa Ibara ya 46 A ya Katiba ikiwa inadaiwa kwamba Rais; ametenda vitendo ambavyo kwa jumla vinavunja katiba au sheria ya maadili ya viongozi wa umma.
Lissu alisema atakusanya saini za wabunge kuunga mkono hoja yake ambayo ni asilimia 20 kwa mujibu wa Kanuni za Bunge. Wabunge wote kikatiba ni 357. Julai 13, mwaka huu wakati akitoa maoni ya Kambi ya Upinzani katika Wizara ya Katiba na Sheria bungeni, Lissu alisema uteuzi wa majaji umegubikwa na ukiukwaji wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano. Alisema baadhi ya majaji walioteuliwa hawana sifa, uwezo na kwamba hawakufaa kufanya kazi hiyo.
Kauli hiyo ilisababisha Bunge kuiagiza Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge inayoongozwa na Mbunge wa Mlalo (CCM), Hassan Ngwilizi kumhoji ili athibitishe kauli yake. Alisema wakati akihojiwa na kamati hiyo, pamoja na nyaraka nyingine, aliwasilisha nakala ya ripoti ya kikosi kazi kilichoundwa mwaka 2008 na aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika na aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo kuchunguza uteuzi wa majaji nchini.
Alisema ripoti ya kikosi kazi hicho kilibaini kuwapo majaji ambao hawana sifa ya kufanya kazi hiyo, lakini Rais Kikwete ameshindwa kuwaondoa kazini. Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki kwa tiketi ya Chadema alisema hali ya mahakama ni mbaya, kwani kuna majaji wawili ambao waliwahi kukamatwa kwa rushwa wakiwa mawakili, lakini wakateuliwa kufanya kazi hiyo.
Alisema baadhi ya majaji hawana uwezo hata wa kuandika hukumu kutokana na kutojua vyema lugha ya Kiingereza ambayo ndiyo inayotumika katika Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani. Mbunge huyo alimtaja Jaji mmoja wa Mahakama ya Rufani ambaye ameteuliwa akisema hana hata shahada ya kwanza ya sheria kinyume cha taratibu.
“Kwa mfano, yupo Jaji wa Mahakama ya Rufani (jina tunalo), ambaye hana hata shahada ya sheria anaweza vipi kuwa jaji?,” alihoji Lissu.

Alisema jaji huyo hivi sasa anasoma shahada ya sheria katika chuo kikuu kimoja hapa nchini. Lissu alisema ili mtu aweze kuchaguliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu lazima awe na elimu ya shahada ya kwanza ya sheria, awe ametumikia miaka 10 mahakamani na anayechaguliwa kuwa jaji wa Mahakama ya Rufani lazima awe ametumikia miaka 15 mahakamani.
Mbali ya kueleza hayo, Lissu alisema kwamba alitoa pia katika kamati hiyo, ushahidi unaoonyesha kuwa kuna jaji mmoja wa Mahakama Kuu ambaye hawezi hata kuandika sentensi moja ya Kiingereza iliyonyooka… “Kama jaji hawezi kuandika hata sentensi moja ya Kiingereza iliyonyooka, tunaweza vipi kuwa na mahakama inayotenda haki?”
Alisema kuna jaji mwingine ambaye ameongezewa mkataba wa kufanya kazi mara ya tatu kitu ambacho ni kinyume cha sheria. Alisema kwa mujibu wa Tume ya Mahakama, hakuna jaji ambaye anaweza kufanya kazi kwa mkataba kwa vipindi vitatu. Mbunge huyo alisema mbali ya madudu hayo katika sekta ya mahakama, hivi sasa kuna jaji maarufu ambaye ameghushi umri wa kuzaliwa ili aweze kuendelea kufanya kazi hiyo.

Alisema jaji huyo amezaliwa Septemba 4, 1949 lakini amebadilisha umri wake kuwa amezaliwa Septemba 4, 1952 ili aweze kufanya kazi hiyo hadi mwaka 2017. Mbunge huyo alisema kazi hiyo ya kughushi umri wa jaji huyo imefanywa kwa kunyofoa nyaraka za kumbukumbu zake Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Alimtaka jaji huyo kuzirejesha mara moja nyaraka hizo vinginevyo katika Bunge lijalo atamtaja kwa jina hadharani.
Alipotakiwa kueleza kwa nini asimtaje sasa alisema akifanya hivyo anaweza kutingisha nchi. Kama Lissu atachukua hatua hiyo, itakuwa ni mara ya pili kwa mbunge kuwasilisha bungeni hoja ya kutaka kumwajibisha kiongozi wa juu serikalini. Mara ya kwanza alikuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe katika Bunge lililopita alipokusanya saini za wabunge kutaka kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitaka awajibishe baadhi ya mawaziri waliokuwa wametajwa kuhusika katika matumizi mabaya ya madaraka katika Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
Hata hivyo, Rais Kikwete alifanya mabadiliko makubwa katika Baraza lake la Mawaziri hivyo kuzima hoja hiyo ya Zitto.
Chanzo: Mwananchi: mwanzo - Gazeti la habari za kiswahili la kila siku Tanzania, linaongoza
 
Makinda hakuchaguliwa kwa merit bali ilikuwa ni kumkomoa six tu.kazi yake kubwa ya kwanza ni kuitetea serikali kwa nguvu zake zote,kwa akili yake yote angalia alivyokurupuka kumwambia Lema alete Ushahidi kwenye tuhuma zake kuwa serikali inauwa wananchi na ni lini aliileta bungeni?
alikuwa pia anataka kuipotezea ripoti ya Ngwilizi<iko wapi ripoti ya Jairo?Lissu anayosema na aliyosema ni kweli tupu kama siyo kwa nini hataki kuleta ripoti zijadiliwe ili wananchi waujue ukweli?SHAME ON CCM
 
Huyu dhaifu dawa yake ni the HAGUE 2!

.....
kWELI KABISA NA KWA MSAADA MKUBWA WA igp MWEMA na timu yake ya makamanda wa mkoa kesi iyakuwa nyepesi watu kama kamuhanda ,Shilogile nk
 
Tunashanganzwa na M4C, V4C, operation mchaka mchaka, sangara nk, kwanini hizi operation zisihamasishe wananchi kuielewa katiba ya sasa na kutoa maoni mazuri yatakayotupatia katiba mpya itakayokidhi mahitaji ya sasa na baadae?

Ni kweli unavyosema. Ila pia kumbuka kuwa na majaji feki ni suala la hatari sana.

Tundu Lissu kwa hili la majaji haleti maigizo. Amelivalia njuga hasa. Na huo ndo upinzani wa kweli. Tuangalie atafikia wapi
 
Ni kweli unavyosema. Ila pia kumbuka kuwa na majaji feki ni suala la hatari sana.

Tundu Lissu kwa hili la majaji haleti maigizo. Amelivalia njuga hasa. Na huo ndo upinzani wa kweli. Tuangalie atafikia wapi

Kwa hiyo mkuu unaamini kwa mfumo wa bunge letu ambalo ushabiki wa kisiasa ndio zaidi LISSU atafanikiwa azma yake? Lakini kwanini asielekeze nguvu kwenye mchakato wa utoaji maoni ili kuleta katiba iliyo imara?
Tuwe makini na hawa wasasiasa........ Loh!
 
Ni kupoteza tu muda kumshitaki Rais kwenye bunge lenye asilimia 80 ya wabunge kutoka CCM. Yeye apeleke hoja binafsi bungeni kupinga uteuzi wa rais na kutaka utenguliwe lakini si kumshitaki rais mwenyewe. Wabunge wa CCM na njaa zao watakubali anayewalisha aondolewe?

Well said, ni sawa na kesi ya mume ukampa mkewe atoe hukumu!!
 
Amefikia ukingoni. Na nna uhakika hana jipya.

Kuna kigezo cha kuwa jaji Tanzania? alikianzisha yeye hicho kigezo?

Hata Marehem Mzee Kasiim alikuwa Jaji Tanzania, ana kigezo kipi?

Huyo Tundu Lussu ana kigezo kipi cha kuwa mwana-siasa? Ana shahada ya siasa? aliitowa wapi? Iramba?
Nina mashaka na uwezo wako wa akili
 
Amefikia ukingoni. Na nna uhakika hana jipya.

Kuna kigezo cha kuwa jaji Tanzania? alikianzisha yeye hicho kigezo?

Hata Marehem Mzee Kasiim alikuwa Jaji Tanzania, ana kigezo kipi?

Huyo Tundu Lussu ana kigezo kipi cha kuwa mwana-siasa? Ana shahada ya siasa? aliitowa wapi? Iramba?

ah kumbe wewe Zomba, nilikuwa nataka kutoa comments lakini basi sikuona jina
 
Zomba Zomba Zomba,Comment yako inatia mashaka uelewa wako wa mambo,Siasa mpaka Degree ya Siasa? Nyererer alikuwa na degree ya Siasa? Yet he was Role model of all Politician in TZ and Africa!
 
Lisu mshitaki hata kama bungen watamtetea tutawawekea alama wabunge uchwara then 2015 tutawahukumu,hatua ya kumshitak na kumsema bungen itapunguza sana kura za magamba fanya hivyo mkuu
 
Hili linaweza kuwa jaribio zuri sana la constitutional process yetu na hapa ndio inaweza kuwa ni vizuri kuona wale waliotaka PM Pinda aondolewe watakuwa tayari kusimama kumshtaki Rais. It'll be very interesting.

Hili swala madam Spika hatalikubali. Atalipotezea au atasema nitalipitia nione kwa muda wangu mwenyewe either kulikubali au la. Hata hivyo, hiyo ilishashindikana kwa Waziri Mkuu,vipi kwa Raisi? Bunge letu bado halina uwezo wa kuisimamia serikali. Ni formality tu kwamba nchi haipaswi kwenda bila bunge, basi!!
 
Kwa hiyo mkuu unaamini kwa mfumo wa bunge letu ambalo ushabiki wa kisiasa ndio zaidi LISSU atafanikiwa azma yake? Lakini kwanini asielekeze nguvu kwenye mchakato wa utoaji maoni ili kuleta katiba iliyo imara?
Tuwe makini na hawa wasasiasa........ Loh!
First things first, na pia kwakuwa mimi I'm not a slave to a public opinion nachelea kusema at this point in time discussing constitutional changes is a waste of time. You know as well as I do they can't finalise this referendum
in time for the 2015 general elections
 
Udhaifu wa Rais JK, Uzembe wa Bunge na Upuuzi wa CCM. Zengwe na mipasho itatawala hii hoja kama ikifanikiwa kufika Bungeni.
 
Hili swala madam Spika hatalikubali. Atalipotezea au atasema nitalipitia nione kwa muda wangu mwenyewe either kulikubali au la. Hata hivyo, hiyo ilishashindikana kwa Waziri Mkuu,vipi kwa Raisi?

Unajua ni vipi lilishindana kwa waziri mkuu? Je kama ZZK angeendelea nalo kwenye vikao vinavyoondelea sasa hivi angeshindwa?

Mimi nadhani kusema ilishindikana kwa waziri mkuu, is being myopic in your view. Thanks to that petition JK was forced to axe some ministers
 
Hoja ya Lissu inaungwa mkono na majaji na watumishi wengi wa Mahakama ambao wanakatishwa tamaa na teuzi zisizoheshimu vigezo! Kwasababu wao hawawezi jitokeza wazi,wanamsaidia mtu kama Tundu Lissu kwa vielelezo na taarifa za siri za majaji watuhumiwa!
 
Back
Top Bottom