Lissu Kuhamia ACT Wazalendo? Muda utaamua

Lissu Kuhamia ACT Wazalendo? Muda utaamua

Waswahili wanasema usilolijua ni sawa na usiku wa giza. Baada ya mvutano sa muda mrefu na wenye chama hatimaye kuna kila dalili Lissu akahamia ACT.

Leo hapa najua kuna wale washabiki watatoa povu, lakini muda utaamua. Muda haujawahi kuongopa kwenye chochote.

Yapo ambayo ningeweza kuyaweka wazi Ila sababu ya kuheshimu muda basi wacha ibaki hivyo. Ila ndio ninawasanua kuwa baada ya muda mtapigwa mshangao.
hii mbona kama inakuja na kutoka, tusubiri huo muda
 
Sijui kama amerudi rasmi, sijaona taarifa yoyote toka Chadema mpaka sasa, au kama ndio amerudi kimya kimya kama alivyoondoka .. ok.
Kasema Hana chama bado wakati huo huo akaipigia kampeni Chadema 2025 iingie ikulu!! So nahisi anatengeneza connection arudishwe kwenye chama apewe kitengo.
 
Kasema Hana chama bado wakati huo huo akaipigia kampeni Chadema 2025 iingie ikulu!! So nahisi anatengeneza connection arudishwe kwenye chama apewe kitengo.
Sijui kwanini viongozi wapo kimya kwenye hili, naona wameacha muda uamue, sijui hii ni dalili ya kutokuwa na msimamo wa pamoja kule juu au ni kitu gani kingine?

Anyway, kama mleta mada asemavyo, time will tell.
 
Wala usishangae viongozi wengi wa chadema ni majuha
 
Lissu inabidi awepo kwenye Serikali ya mama atamsaidia sana aende tu CCM.
 
Lissu ahaimie Act? Unaota ndoto mbaya sana chizi wewe!
 
Vyama vya siasa ni majukwaa tu, popote pale sawa ili mtu mwenye maono ya uongozi atumize maono yake. Hata hivyo msiamini chama, aminini mtu bila kujali anagombea uongozi kupitia chama gani. Mpimeni mtu na sio chama chake. Lissu akihamia ACT hakuna kitachombadilisha yeye na maono yake
 
Ny
Waswahili wanasema usilolijua ni sawa na usiku wa giza. Baada ya mvutano wa muda mrefu na wenye chama hatimaye kuna kila dalili Lissu akahamia ACT.

Leo hapa najua kuna wale washabiki watatoa povu, lakini muda utaamua. Muda haujawahi kuongopa kwenye chochote.

Yapo ambayo ningeweza kuyaweka wazi Ila sababu ya kuheshimu muda basi wacha ibaki hivyo. Ila ndio ninawasanua kuwa baada ya muda mtapigwa mshangao.
ie chawa mama yenu alisema mjibu hoja sio kugeuka vituko kiasi hiki
 
Katiba ya Warioba - ilikuwa inapendekeza uwepo wa mgombea binafsi, Chadema wanapendekeza rasimu ya Warioba irudi. Hivyo ni wazi wanaunga mkono uwepo wa mgombea binafsi, ukisikia wanasema hakuna mtu aliye mkubwa kuliko chama basi wanakua wanamaanisha kwa katiba hii ya sasa mtu hawezi kuwa mkubwa kuliko chama, ila kwa katiba mpya, mtu anaweza kuwa mkubwa kuliko chama.

Achaneni na kuviamini vyama vya siasa, aminini wagombea na sera zao, mkitaka vyama tutabaki hapa tulipo.
 
Ndoto za zitto kabwe ni kuona Lissu akihamia Ujiji kitu ambacho mhe Lissu hawezi kukifanya hata kwa kulogwa
 
Moja ya kazi kubwa ya BIG CHAWAS, ni kuandika chochote ili mradi tu kinasiliba upande wa pili. Shida inakuja miaka inawapita MIKEKA INAMWAGWA, but nothing kwa kweli. Pato lote la uchawa inaishia kwa karumanzila tuuuu.
 
Mkiandika sana kwenye uzi wa huyu mvuta bangi mtamfanya avimbe kichwa wakati kichwa chenyewe kimejaa bangi tu.
 
Zinachosha kuwaamini watu kwamba wapo kwa ajili ya wananchi kumbe kila mtu na tumbo lake....
Wanasiasa ni kama bongo movie tu hamna ukweli kwenye siasa
Baby wewe ndo unaliona hilo leo? Mimi nililiona waziwazi 2015 kwenye ujio wa Lowasaa. Wale tuliokuwa tunawaamini kuwa ni wenzetu kwenye kundi la 'against' walitusaliti baada ya kukatiwa cha juu. Wale tuliogomea cha juu na kubaki na misimamo yetu tukabaki na maumivu tu. Kuanzia hapo nikaachana na kushabikia vyama vya siasa. U-independent unanifaa zaidi.
 
Mimi nishabaki shabiki maandazi tu, najaribu jaribu na kuvaa mashati ya kijani labda lolote linaweza kutokea kwenye panga pangua za mama 😁😁😁 nami nijaze tumbo langu.....

2015 nilisafiri mikoa kadhaa kwenda kuvote nikiwa na kitoto changu bado kichanga yaani jaji Lubuva anatangaza matokeo nilikua nahisi homa. Kile kisauti chake hadi leo bado kipo kichwani "Anna Mghwira ACT amepata kura 1365 sawa na asilimia 0.0001"

"Edward Ngoyai Lowasa Chadema amepata kura elf 5 sawa na asilimia....." Nachoka haki ya mama 🤣🤣🤣
Ningumu sana ngamia kupenya kwenye tundu la sindano
 
Back
Top Bottom