Lissu: Tungekuwa wengi, ingekuwa nzuri, na bunge lijalo, ninatamani liwe na uwiano sawa wa wabunge wa CCM na upinzani ili kuleta usawa kuliko hali ya sasa.
Lissu: ‘Best moment' ya upinzani ni pale tulipowasha moto bungeni,Spika ajaye pia ajipange na moto wa upinzani ambao mwakani utakuwa mkubwa zaidi.
Lissu: Natamani kuona Bunge la uwiano sawa wapinzani na CCM, hili ni la msingi na wabunge wa upinzani natamani kuona wenye mitazamo migumu kama ya Lissu, (John) Mnyika, (Mch Peter) Msigwa, (Halima) Mdee, Mkosamali, (David) Kafulila wabunge wa namna hii watachangamsha sana Bunge.