Lissu: Biashara ya pamba inatawaliwa na Vigogo wa CCM, inaleta mgongano wa kimaslahi

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Jul 24, 2021
576
1,625
Tundu Lissu ameyasema hayo akizungumza muda na huu tar 9/22023 na Waandishi wa Habari Bariadi, akisema wakulima kila mahali wanalalamika hawapati faida kama awali na hili linasababishwa na watu wanaoamua pamba inunuliwe na nani na kwa bei gani ambao wengi ni Wanaccm.

Akisema Bodi ya Pamba ndio inapanga bei ya pamba, lakini;

- Mwenyekiti wa Bodi ya Pamba ni Christopher Mwita Gachuma ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM na ndiye mnunuzi mkubwa wa pamba nchini.

- Bariadi mnunuzi mkubwa wa pamba katika mkoa wa Simiyu ni Bwana Njau (Mbunge wa jimbo la Itilima kwa tiketi ya CCM) na ndugu yake Gungu (Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM).

- Mwandoya Jimbo la Kisesa utaambiwa kuna mtu anaitwa Gaki lakini ukiuliza kila mtu eneo hilo anayefahamu atakwambia hiyo Jineri inaendeshwa na ndugu wa Luhaga Mpina Mbunge wa Jimbo Kisesa CCM.

- Maswa Mashariki - Mbunge Nyongo ndiye mnunuzi mkubwa wa pamba eneo hilo.

- Wilaya ya Kishapu, Jineri inamilikiwa na Cherehani, Mbunge jimbo la Ushetu ambaye ndiye mnunuzi mkubwa wa pamba eneo hilo.

- Ushetu kwenyewe kuna mgogoro mkubwa kwenye zao la Pamba na Tumbaku, ambako wananchi wamesema mnunuzi mkubwa wa pamba katika jimbo la Ushetu ni kampuni ya Mkwawa ambayo nyuma yake viongozi wengi wa CCM akiwepo Hussein Bashe.
 
Halaf Bashe akikunja kimdomo chake kile na vimaneno kibao vya Kiingereza...

Utafikiri mwadilifu kweli kumbe Wizi mtupu
 
Hilo liko wazi CCM inahujumu uchumi wa wakulima na uchumi wa nchi kwa ujumla.
Wakulima wengi wameshaacha kulima pamba, ni hasara tupu kulima pamba bora ufanye vibarua vya kulima, kulima kulima pamba ambapo gharama ya uzalishaji wa ekari 1 ni Tsh 700,000-1,000,000 huku
Tija ya Ekari 1 ni kilograms 400-1200.

Hivyo wastani wa wakulima wengi huzalisha chini ya tija yaani kilo 300-700 kwa ekari 1.
Leo bei ya kilo 1 ya pamba ni Tsh 1060
Kulima pamba ni kushibisha matumbo ya mafisadi wa CCM
 
Hilo liko wazi CCM inahujumu uchumi wa wakulima na uchumi wa nchi kwa ujumla.
Wakulima wengi wameshaacha kulima pamba, ni hasara tupu kulima pamba bora ufanye vibarua vya kulima, kulima kulima pamba ambapo gharama ya uzalishaji wa ekari 1 ni Tsh 700,000-1,000,000 huku
Tija ya Ekari 1 ni kilograms 400-1200.

Hivyo wastani wa wakulima wengi huzalisha chini ya tija yaani kilo 300-700 kwa ekari 1.
Leo bei ya kilo 1 ya pamba ni Tsh 1060
Kulima pamba ni kushibisha matumbo ya mafisadi wa CCM
Hapa meatu tunauza kwa 1100 ni hasara kubwa
 
Hapa meatu tunauza kwa 1100 ni hasara kubwa
Poleni Sana achaneni na kilimo Cha pamba kama serikali itakuwa ikiongozwa na CCM .
Limeni mbaazi, Choroko, Kunde, Dengu, Mahidi, Alizeti, pia fugeni mbuzi breed/mbegu zilizoboreshwa ili muongeze kipato.
Zao la Pamba lilikuwa zamani kabla ya ushirika haujaingiliwa na siasa za CCM
 
Kwa mujibu wa Lisu Viongozi hao ni Wabunge wa ccm wanaotoka Kanda ya Ziwa ndio wanashirikiana na Wafanyabiashara wakubwa kupinga bei ya soko.

Ni vyema hili jambo likabainishwa bila ushabiki ,Je bei ya zao la pamba kwenye soko la Dunia imeporomoka?

View: https://twitter.com/Nipashetz/status/1698946976245518500?t=aTuemlGeuIcA9_1PoXBJdw&s=19

My Take
Bashe wape majibu Wakulima la sivyo usipoangalia utatemeshwa uwaziri.

Huwapendi CHADEMA lakini kutwa kuchat uko busy kupost taarifa zake kuliko Hata za vyama vyako vya CCM na ACT Wazalendo
 
Back
Top Bottom