Lissu bado anahitaji msaada wenu Watanzania

elmagnifico

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2011
Posts
8,260
Reaction score
9,760
Nimesikia kwenye taarifa ya habari ya asubuhi toka UFM akihojiwa kaka yake Lissu na kudai kuwa, familia iliandika barua kwenda ofisi za Bunge kuomba Bunge kuchukua jukumu la matibabu ya Tundu Lissu.

Lakini toka watume hiyo barua hakuna jibu walilopewa mpaka sasa.
Pia akadai ya kwamba Lissu kwasasa anaongea na ndiye shahidi namba 1 hivyo kama wameshindwa muhoji dereva basi wakamuhoji Tundu Lissu.
Anadai mpaka sasa wao kama familia hawajapewa taarifa yoyote juu ya upepelezi wa kesi ya kushambuliwa Lissu.

Watanzania, mmeacha kuchangia matibabu yake? Maana Watanzania wengi walidai hata serikali isipotoa ela wao watachanga sasa kwanini mmeacha Lissu badi hajapona anahitaji pesa ya kwenda kwenye matibabu hasa ya mazoezi ya viungo.

Dr Shika asiwafanye msahau kuwa kuna Lissu jamani
 
Watanzania!!!!
ina maana yeye alikua hana akiba hata kidogo?? mkewe?? ndugu zake?? marafiki??
Guys tuweni serious kidogo.

Na Bunge nalo kwann halimsaidii sasa labda tumuulize Mange atasemaje.
 
Watanzania!!!!
ina maana yeye alikua hana akiba hata kidogo?? mkewe?? ndugu zake?? marafiki??
Guys tuweni serious kidogo.

Na Bunge nalo kwann halimsaidii sasa labda tumuulize Mange atasemaje.
Matibabu yake siyo madogo mkuu hata kama ana akiba inaweza isitoshe.
Bunge ndiyo hivyo liko kimya.
Nimeuliza watanzania maana walidai wako tayari kugharamia matibabu ila naona kama kawaida uwa inakuwa nguvu ya soda
 
Aiseee kwa kweli ilikua nguvu ya soda maisha magumu sana asikwambie mtu labda hao walioahidi ni wale ambao kwamba.

Msaada wangu mimi upo kwenye maombi ila pesa hehehe.
 
Aiseee kwa kweli ilikua nguvu ya soda maisha magumu sana asikwambie mtu labda hao walioahidi ni wale ambao kwamba.

Msaada wangu mimi upo kwenye maombi ila pesa hehehe.
Wewe ni kati ya wale wa utaambulia ushauri ukihitaji msaada wa kifedha...
 
Huku JF watu waliongoza kupinga ile kauli ya wizara kwamba family iandike barua ili serikali imtibu.
Familia ikaingia mkenge,walipoona michango imekata wakaandika!;
Mwanasiasa hajawahi kuwa na nia njema kwa yeyote.
Any way Lema alisema atauza figo ili apate helahela kwa ajili ya Lisu.
Labda hajapata mteja
 
Figooo!!!
Lol, kuna Mapenzi na Mahaba hayo sijui tuiteje....
 
Hiii kitu ilikosewa sana mwanzo pale.[emoji41]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…