MasterP.
JF-Expert Member
- Jun 5, 2013
- 7,985
- 6,248
KwendraaaaaaaaaaNi aibu kwa mwanasheria nguri anayetaka kuwa kiongozi mkuu wa nchi kutumia jukwaa la kisiasa kwa matatizo yake mwenyewe.
Nimemsikia Lissu akiwasomea wananchi, kwenye kampeni yake ya Urais wa JMT, vifungu kutoka kwenye kitabu cha MAADILI YA UCHAGUZI WA RAIS, WABUNGE NA MADIWANI YA MWAKA 2020 (Chini ya Kifungu cha 124.A cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343) kuhusu kuitwa kwake na Tume. Yeye mwenyewe, kwa mdomo wake, ameituhumu Tume na anatakiwa aende kutoa ushahidi. Je, wananchi ndio mashahidi wake au baraza la wazee wa mahakama?
Lissu asiweweseke kutaka kufanya kosa lake liwe la kiasa. Je, akifanikiwa kuwa Rais ataacha watu wafanye wanavyotaka?
Kwa jinsi alivyojipambanua ya kuwa ni jasiri wa dharau, ni dharau hiyo hiyo atawashushia walio chini yake.
Hakika atapata kura za wanachama wa CHADEMA wasiojitambua.