JE, MAMLAKA IMEPANGA KUMUACHIA LISSU KWA SIRI KUPITIA MAHAKAMA LEO?
Kuna taarifa zinaenea mtandaoni kuwa Mhe. Tundu Lissu amepelekwa mahakamani kimya kimya asubuhi hii. Kama taarifa hizi ni za kweli tutasubiri kupata ufafanuzi kutoka kwa Wakuu wa Magereza ni kwa nini wamefanya hivyo!
Lakini kwa nini Lissu apelekwe ghafla na kimya kimya mahakamani muda mfupi baada ya ntiiti ya Seneti ya Marekani kusambaa mitandaoni. Je, mamlaka imeamua kumuachia Lissu kimya kimya baada ya kumkamata kwa mbwembwe nyingi sana.
Pengine ni busasa kwa wafuasi wa CHADEMA walioko Kigamboni, Magomeni, Ubungo, Ilala, Kariakoo, Buguruni, nk wawahi haraka wafike mahakamani kwani ni haki yao kujua hatima ya kiongozi wao.
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?
Cc: Boniface Anyisile Mwabukusi Paul Kisabo Azaveli Lwaitama John Heche
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Itunge, Dar es Salaam; 30 Aprili 2026; Saa 4:50 asubuhi