Tetesi: Lissu anaumwa

Tetesi: Lissu anaumwa

Kwa akili ndogo sana tu, hivi kesi ya Lissu, dunia nzima inajua, iko live kwenye mitandao mbali mbali, narudia nani adhubutu kumpa sumu ili afe? Hivi issue kubwa kama hii, alafu apewe sumu? Huu ni uongo mkubwa na wa wazi kuichafua Serikali ya CCM, na hata wafuasi na wana chama wa Chadema wanajua hilo haliwezekani, sababu kuu Lissu yupo chini ya Magereza na Magereza ipo chini ya Serikali ya CCM, sasa kwa lipi hasa serikali ijichafue kwa kiwango kikubwa hivyo eti kumuwekea sumu Lissu?

Na uzuri, Serikali imekanusha hizo habari, na kukataa, kuwa hakuna kitu kama hicho, nachosema hapa, hii ni mbinu ya CHADEMA kuichafua Serikali kwa nia ovu tu, basi kutafuta attention tu ya public
Lakini si mwenyewe umeeleza hapo juu jinsi Tundu Lissu mwenyewe anavyo fanya maigizo, sasa kumbe imekuwa ni wafuasi wake ndio waigizaji?

Pamoja na hayo yote, hujakanusha uigizaji wa hao wanaopotezwa na kuuliwa kama akina mzee Kibao. Serikali hiyo hiyo unaiona haina wajibu wowote wa kujisafisha, ata kama ni kwa kufanya maigizo tu ya uchunguzi!

Padre Kitima kabamizwa kichwa, mchana kweupe, serikali usiyotaka ionekane kutokuwa makini, ipo kama haipo!

Ni lini ulisikia uchunguzi wa aina yoyote ulifanyika juu ya mkasa wa kunusurika kwa huyo huyo Tundu Lissu. Halafu leo hii unakuja hapa na kuonyesha kuwa bado kuna serikali inayofuata taratibu za kiutawala?
Hii inatofauti gani na GENGE la wauaji wasiowajibika kwa yeyote?
 
Tumia Id yako original basi
Nawe mwendee bila kuwategemea polisi. Hapo tutamwona ni nani mwamba kati yenu.
Hapa mnajipiga kifua kwa kujuwa mnawategemea polisi wawafanyie uchafu wenu; bila ya polisi nyinyi hamtambi chochote.
Na hao polisi karibuni mtanyang'anywa, tuone mtakimbilia wapi.
 
Sasa tuwaomba Polisi wakae pembeni halafu tukutane. Unasemaje hapo?
Hilo litakuwa jambo jema sana.
Uwanja utakuwa tambalale kabisa.

Lakini nimemaliza kukucheka hicho kiinglish ulicho andika hapo juu #176.!
Kweli wewe ni kihiyo hasa!
 
Back
Top Bottom