Lissu amlima barua Shibuda

Lissu amlima barua Shibuda

Atawaomba radhi watu wangapi? wabunge 48 wa chadema? au viongozi wote wa CHADEMA? au wana-CHADEMA wote? Hivi Shibuda anajua nani ni CHADEMA? Kwa akili yake na hao waliomtuma wanafikiri CHADEMA ni wabunge na viongozi wengine ndani ya chama. Lakini kwa kumsaidia CHADEMA na mamilioni ya watanzania wake wa kwa waume, wazee kwa kwa vijana, waliopigika kimaisha na kupoteza imani na ccm pamoja na serikali yake? Na alichokifanya Shibuda bungeni dhidi ya posho ni kuweka waziwazi dhamira yake kuwa hayuko bungeni kusaidia watanzania maskini, yuko pale kutunga BETI za kiswahili ili kumfurahisa bosi wake ccm.

Mh Lissu na viongozi wengine CHADEMA, mtoseni huyu, na huo ujira wa mwera akawadai mabosi wake ccm au aje huku mtaani aone maisha yanakuwaje. Kiongozi wa hovyo kabisa huyu.
 
Kuna watu humu JF walionya kuhusu Shibuda na nia yake ya kujiunga Chadema. Sasa wanajionea wenyewe......
 
Afukuzwe tu huyo, anataka abaki na Ubunge akikaribia kumalizia awamu yake atakiharibu sana Chama. Atoswe tu na uitishwe uchaguzi mdogo, potelea mbali hata kama jimbo litapotea
 
Lakn kuna haja ya viongozi wajuu wa Chama kumtizama mh.kwa asije VUJISHA "SIRI" za chama wakati tukielekea uchaguzi mkuu kwa sababu anaonekana ni mtu mwepesi wa kumbadilisha mawazo na ana Interest binafsi so atizamwe mara mbili hata kama aki apologise.
 
Mtu anayeomba radhi ni yule anayejutia kitendo alichokifanya. Kila alipopata nafac ya kuchangia, Shibuda aliongea kwa mbwembwe, kejeli na dharau ya hali ya juu. Kama anataka kuomba radhi, basi ni kwasababu ameona kwamba kitumbua chake kinaelekea kuingia mchanga (kuhyang'anywa kadi ya CDM) na si kwa sababu amegundua amewadhalilisha viongozi na chama kwa ujumla.

Ili kutenganisha mwanga na giza, lazima achukuliwe hatua za kinidhamu kama zilivyoainishwa na katiba na taratibu za chama na kambi ya upinzani.
 
Aende public atumie runinga kuomba msamaha watanzania wapendao Tanzania kusema alipotoka na kudhani anatumikia chama chao za Ma CCM
 
Aondolewe huyu jamaa hafai kwa ukombozi na hii iwe fundisho kwetu juu ya watu wa ccm wanaohamia chadema baada ya kuondolewa kwene kura za maoni.sheria ifuate mkondo wake
 
Hatuwezi kupiga midomo kama CCM. Lazima kuwe na nidhamu ya kusema. Kila mtu akiacha mdomo wazi, nidhamu ndani ya chama itatoka wapi? Ni kosa kubwa sana kuzipinga sera za chama nje ya vikao stahiki. Na kama mwanachama anapinga sera zilizokubaliwa kwa kauli moja kupitia kwa wawakilishi wa wanachama basi anazipinga nje ya hapo hafai hata kidogo. Na hakuna kuonywa hapo kwani amekosa nidhamu.

Huku ni kutetea maslahi binafsi. Ni Watz wangapi ambao wamemsikiliza kupitia vyombo vya habari? Na alikuwa hajui kama umma wa Watz unamsikiliza? Chama kichukue maamuzi mazito na ya haraka kwa utovu wa nidhamu wa aina hii. Siyo kuwa fundisho kwa wengine bali kuleta hali ya kuwa na nidhamu ktk jamii ya wanachama kwa wale wasio na nidhamu.

Hapa hakuna kusema wanachama wanazibwa midomo bali kuna kukiuka maadili ya uanachama. Hatuwezi kukosa utaratibu wa kuongea kama vile tupo CCM, kila mtu anaongea anachojua. Ndani ya CHADEMA huu utaratibu wa kuongea bila utaratibu usipewe nafasi kabisa. Wakaongee kwenye vikao husika.

Ni aibu kwa chama mbunge kupinga sera za chama ktk kusanyiko kubwa kama bunge. Cha ajabu zaidi alikuwa anashangiliwa sana na wabunge wa CCM. Chama kwanza kimechukua muda mrefu kumwajibisha. Alipaswa kuwa ameshawajibishwa mara baada ya pale kwa kuandikiwa barua ya kujieleza kwa nini asifukuzwe ndani ya chama.

Kama CHADEMA ikitaka kulinda hadhi yake mbele ya umma wa Watz basi vitendo kama hivi vikomeshwe mara moja. Mbunge ni mtetezi wa sera za chama; sasa huyu mbunge anatetea sera zipi?
 
Fukuzeni Shibuda haraka, alishawaponda na kuwaharibia hapo mwanzo, anaendelea kuharibu hivi sasa, hebu mfukuzeni haraka asije akatuharibia, tena mahali ambapo sentitive huko mbele jamani!!!!! SHIBUDA HATUFAI. Bora jimbo lichukuliwe na chama cha kujivua magamba, kuliko kukaa na SHIBUDA ndani ya chama chetu, ili tuepuke msemo usemao 'KIKULACHO KINGUONI MWAKO'!
 
yaan nasikia hadi kichefchef kumsikia mtu tena kijana mwenye akili timam anasema cdm ni ndoto kushika nchi ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,hivi kijana amerogwa au?lakin kweli c unajua wanamajimarefu?
 
Cdm nawashauri msihadaike na vitu vidogo huyo hata akiomba radhi ni unafiki na tamaa zake tu. Jiulizeni tangu ameingia dcm ni lipi jema alilolifanya zaidi ya kukipaka matope chama? Ni heri kuwa na wabunge wachache wenye nia ya dhati kuliko kuwa na utitiri wa wanafiki. Siungi mkono msamaha kwa huyu mnafiki kabisa. Cdm jiaminini kwani watz wanawakubali, huyo shibuda si lolote asiwatishe. Mtimueni tuone ataenda wapi, nina uhakika maswa hawatampa kura na sijui chama gani kitampokea. Anaboa sana
 
"'""Shibuda asema atawaeleza wananchi kuhusu maovu ya Mbowe na Zitto na ubinafsi CHADEMA 03/07/2011

http://www.wavuti.com/4/post/2011/0...we-na-zitto-na-ubinafsi-chadema.html#comments



Mbunge wa Maswa Magharibi, John Shibuda, amesema hatishiki na vitisho vinavyofanywa na viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na yuko tayari kufukuzwa katika chama kwa kosa la kusema ukweli siku zote.

Katika maelezo yake, Shibuda, ambaye alihamia CHADEMA mwaka jana akitokea CCM, baada ya kushindwa katika kura za maoni, alisema pamoja na kwamba Mbowe na Zitto wanaamini wako sahihi, ukweli utabaki pale pale kwamba wanasiasa hao wanahatarisha demokrasia katika chama hicho.

Hivi karibuni, Shibuda amedaiwa kwenda kinyume cha msimamo wa chama chake, kuhusiana na suala la posho za wabunge, kitendo ambacho kimemfanya aonekane muasi ndani ya chama na hivyo kuundiwa tume ya kumchunguza.


KUOMBWA RADHI

Akizungumza na MTANZANIA Jumapili mjini Dodoma jana, Shibuda alibeza shutuma hizo zilizoelekezwa kwake na kuwataka viongozi wa juu wa chama hicho, Mwenyekiti, Freeman Mbowe na Naibu Katibu Mkuu, Kabwe Zitto, kumwomba radhi kutokana na kumchafua.

Mbali ya kuombwa radhi, amesema pia ataandaa mikutano ya hadhara wenye lengo la kuwaeleza wananchi tabia za viongozi hao, "Natarajia kusafiri kwenda nje ya nchi kwa shughuli za kibunge, nitakaporudi, nitaitisha mikutano ya hadhara katika maeneo mbalimbali nchini kuwaeleza wananchi juu ya Zitto na Mbowe, ambao tayari wameshanishutumu kupitia vyombo vya habari. Mikutano hiyo nitaianzia jimboni kwangu mwishoni mwa mwezi huu, nitaweka wazi kila kitu kwa sababu wananchi ndio wenye chama na wana haki ya kujua nani anasema ukweli na nani anasema uongo. Hata hivyo, kabla mimi sijaenda kwa wananchi nawaruhusu wao waende kwa wananchi wakanishitaki, wakaeleze ubaya wangu ili mimi nitakapowaeleza wananchi basi wao ndio wapime wenyewe. Mimi nayajua mengi sana ya CHADEMA, kwa muda mfupi niliokaa katika chama hicho nimejionea mengi sana na nalazimika kusema kuwa alichokuwa akikisema Chacha Wangwe (marehemu) ni sawa kabisa na hakukosea kitu....

"Nakwambia sura ya CHADEMA ukiwa nje ya chama ni tofauti na sura ya CHADEMA ya ndani, ni tofauti kabisa kwa sababu yanayofanyika humo ni mambo ya ajabu sana. Mbowe anaendesha chama kibabe na anaungwa mkono na Zitto ambaye anaonekana kuwa na tabia ya ukuwadi na unafiki, mimi siwezi kunyamaza, siwezi kufumbia ukweli katika jambo ambalo naamini ni sahihi. Niliyosema nimeyasema na kama hayakuwafurahisha sitawaomba radhi na sina tabia ya kuomba radhi, kwani hata nilipokuwa CCM sikuwahi kuomba radhi.
Lakini kwa kuwa wao ndio wamenikosea kwa kunichafua kupitia vyombo vya habari, basi nawataka waniombe radhi kwa waliyonizushia na pia nawataka wawaombe radhi Watanzania kwa kutowaambia ukweli," alisema Shibuda.


KUHUSU "MSIMAMO WA CHAMA KUHUSU POSHO"

Juni 28 mwaka huu, akichangia bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu ya mwaka wa fedha 2011/2012, Shibuda aliitaka serikali iongeze posho za wabunge kutoka Shilingi 150,000 hadi Shilingi 500,000 kwa siku, kwa kuwa kiwango cha sasa hakitoshi.

"Hili suala la posho ambalo ndilo chanzo cha haya, nakwambia siyo msimamo wa chama kama wanavyowaambia Watanzania, huo ni uamuzi wao wawili tu kwa sababu katika vikao walikuwa wanawatisha wabunge na kuwatishia kwamba watawafukuza kama hawatakubali kukataa posho. Huwezi kuendesha chama kwa nguvu kwa sababu hizo posho ndicho kipozeo cha mbunge, kwani kama ng'ombe anayekamuliwa akikosa malisho ukimkamua ujue atatoa damu. Sasa kama ndivyo hivyo, wabunge wasipolipwa posho kazi zao watafanyaje, katika hili siwezi kunyamaza, nitaendelea kuheshimu uongozi kwa ajili ya kujenga ufanisi wa maslahi ya chama ya kutajirisha masikini dhidi ya vatu, cheo ni dhamana. Sitoona haya kukosoa tabia ya umimi na uyeye kwa mtu yeyote, sitahama CHADEMA kwa sababu sikutofautiana na chama bali nimetofautiana na watu wachache kutokana na kutoridhishwa na uongozi wao," alisema.



SHUTUMA DHIDI YA ZITTO

Akimchambua Zitto, alisema anajifanya mzalendo machoni pa watu wakati tabia na matendo yake ni tofauti na anavyowaambia Watanzania.

"Zitto siyo mzalendo, namtaka aache tabia ya ukuwadi na kuunda uzandiki wa kufunika uwazi na ukweli kwa dhamira ya ubinafsi wa kujikweza kisirisiri ili apendwe na uongozi na kuidanganya jamii kwamba yeye ni mwadilifu. Zitto asigandamize haki za watu, wanaojua stahili zao kwa sababu yeye anajipamba ili asihitilafiane na kiongozi wake kwa masilahi yake binafsi, aache tabia ya kujifanya mzalendo wakati ni mnafiki anayetaka kujenga matarajio yake binafsi huku akificha ajenda ya siri ya umimi na uyeye. Ili kutambua tabia yake na mwenzake huyo ni sawa na mwenye kiatu ambaye ndiye anayejua jinsi kinavyomuumiza badala ya mtazamaji ambaye anafurahishwa na rangi ya kiatu, aache kabisa tabia hiyo awe wazi na asitafute umaarufu," alisema.

Alisema kinachomgombanisha na wenzake ndani ya chama hicho ni tabia yake ya kupenda uwazi, wakati baadhi ya wenzake wanataka ukweli usielezwe kwa wananchi.

"Chuki iliyopo ni kwamba mimi Shibuda napinga chama kuwa kama kampuni ya kuingiza wanachama wa kutekeleza masilahi binafsi ili kudumisha ukabila, uyeye, umimi, uwao, umajimbo ambao umefichwa na msemo usemao siri ya mtungi aijuaye kata. Binafsi sitarudi nyuma, naahidi kulinda maslahi na kutetea shabaha ya CHADEMA kwa maslahi ya wananchi, nitaendelea kupingana na tabia ya kuwaonea watu kwa sababu wabunge maskini kama mimi tunapata fedha za kuwahudumia wananchi kwa kudunduliza fedha za mishahara na posho. Wabunge matajiri wao wana mapokeo ya hisa kutoka katika biashara zao binafsi, kwa hiyo ndondondo za mapato kutoka bungeni hawazihitaji, ndiyo maana wanawalazimisha wenzao wasiokuwa na kitu wafuate nyayo zao hata kama wanawaumiza," alisema.

Kutokana na hali hiyo, Shibuda alisema atahutubia mikutano ya hadhara wakati wowote mwishoni mwa mwezi huu baada ya kurejea nchini, ili kuweka wazi tabia za badhi ya viongozi wa chama hicho.





KAULI YA MBOWE

Akijibu shutuma hizo, Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Freeman Mbowe, alisema hapendi malumbano kupitia biombo vya habari, "Kamanda sipendi malumbano kwenye vyombo vya habari, tusubiri muda ukifika ukweli utajulikana tu," alisema Mbowe.

- MTANZANIA


KAULI YA ZITTO

Zitto amesema msimamo wa kumfukuza Shibuda upo pale pale kwani kambi hiyo wala CHADEMA hawawezi kumwacha mbunge anayekiuka sera na kuwadhalilisha viongozi hadharani.

"Shibuda hatafukuzwa kinyemela, lazima taratibu zifuatwe kwa Mnadhimu Mkuu wa kambi yetu kumwandikia barua ya kumweleza makosa yake na yeye kupata fursa yakujibu shutuma hizo. Pili, ataitwa katika Kamati Kuu ya chama chetu (CHADEMA) nao watatoa uamuzi wao... Chadema si chama cha kihuni kwamba tutakurupuka ni lazima haki itendeke na mimi sipendi mtu aonewe, Shibuda atapata haki zake zote kama mwananchama. Mbunge yeyote wa CHADEMA anapaswa kujua akienda kinyume na sera ya chama atafukuzwa".

Alisema suala la posho lipo kwenye Ilani ya uchaguzi wa 2010 kwa hiyo ni sera, na kwamba anayepinga atafukuzwa tu na kwamba CHADEMA wataanza na Shibuda.

Zitto alisema "Shibuda anajua mie humtetea sana, lakini anapokwenda kinyume na sera ya chama tutamfukuza, aniite majina yoyote tu akienda kinyume na sera nitakuwa wa kwanza kumfukuza...

"Kuna masuala ya nidhamu kwenye bunge na wabunge wa chama fulani inaitwa "three line whip", masuala ya msimamo wa kitendaji mfano tulipokaidi kwenda bungeni kutoka nje ya ukumbi wakati Rais Jakaya Kikwete alipokuwa akihutubia bunge (walk out), haya ni ya kawaida na hayana adhabu kali, lakini likiwa la sera adhabu ni kufukuzwa, Shibuda asipaparike," alisema Zitto.
 
Nilisoma kichwa hicho cha habari tz daima,ndani habari ilimnukuu Lissu kwmba ataenda kuandika barua,kwa hiyo bado haikuwa imeandikwa
 
"'""Shibuda asema atawaeleza wananchi kuhusu maovu ya Mbowe na Zitto na ubinafsi CHADEMA 03/07/2011

http://www.wavuti.com/4/post/2011/0...we-na-zitto-na-ubinafsi-chadema.html#comments



Mbunge wa Maswa Magharibi, John Shibuda, amesema hatishiki na vitisho vinavyofanywa na viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na yuko tayari kufukuzwa katika chama kwa kosa la kusema ukweli siku zote.

Katika maelezo yake, Shibuda, ambaye alihamia CHADEMA mwaka jana akitokea CCM, baada ya kushindwa katika kura za maoni, alisema pamoja na kwamba Mbowe na Zitto wanaamini wako sahihi, ukweli utabaki pale pale kwamba wanasiasa hao wanahatarisha demokrasia katika chama hicho.

Hivi karibuni, Shibuda amedaiwa kwenda kinyume cha msimamo wa chama chake, kuhusiana na suala la posho za wabunge, kitendo ambacho kimemfanya aonekane muasi ndani ya chama na hivyo kuundiwa tume ya kumchunguza.


KUOMBWA RADHI

Akizungumza na MTANZANIA Jumapili mjini Dodoma jana, Shibuda alibeza shutuma hizo zilizoelekezwa kwake na kuwataka viongozi wa juu wa chama hicho, Mwenyekiti, Freeman Mbowe na Naibu Katibu Mkuu, Kabwe Zitto, kumwomba radhi kutokana na kumchafua.

Mbali ya kuombwa radhi, amesema pia ataandaa mikutano ya hadhara wenye lengo la kuwaeleza wananchi tabia za viongozi hao, “Natarajia kusafiri kwenda nje ya nchi kwa shughuli za kibunge, nitakaporudi, nitaitisha mikutano ya hadhara katika maeneo mbalimbali nchini kuwaeleza wananchi juu ya Zitto na Mbowe, ambao tayari wameshanishutumu kupitia vyombo vya habari. Mikutano hiyo nitaianzia jimboni kwangu mwishoni mwa mwezi huu, nitaweka wazi kila kitu kwa sababu wananchi ndio wenye chama na wana haki ya kujua nani anasema ukweli na nani anasema uongo. Hata hivyo, kabla mimi sijaenda kwa wananchi nawaruhusu wao waende kwa wananchi wakanishitaki, wakaeleze ubaya wangu ili mimi nitakapowaeleza wananchi basi wao ndio wapime wenyewe. Mimi nayajua mengi sana ya CHADEMA, kwa muda mfupi niliokaa katika chama hicho nimejionea mengi sana na nalazimika kusema kuwa alichokuwa akikisema Chacha Wangwe (marehemu) ni sawa kabisa na hakukosea kitu....

“Nakwambia sura ya CHADEMA ukiwa nje ya chama ni tofauti na sura ya CHADEMA ya ndani, ni tofauti kabisa kwa sababu yanayofanyika humo ni mambo ya ajabu sana. Mbowe anaendesha chama kibabe na anaungwa mkono na Zitto ambaye anaonekana kuwa na tabia ya ukuwadi na unafiki, mimi siwezi kunyamaza, siwezi kufumbia ukweli katika jambo ambalo naamini ni sahihi. Niliyosema nimeyasema na kama hayakuwafurahisha sitawaomba radhi na sina tabia ya kuomba radhi, kwani hata nilipokuwa CCM sikuwahi kuomba radhi.
Lakini kwa kuwa wao ndio wamenikosea kwa kunichafua kupitia vyombo vya habari, basi nawataka waniombe radhi kwa waliyonizushia na pia nawataka wawaombe radhi Watanzania kwa kutowaambia ukweli,” alisema Shibuda.


KUHUSU "MSIMAMO WA CHAMA KUHUSU POSHO"

Juni 28 mwaka huu, akichangia bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu ya mwaka wa fedha 2011/2012, Shibuda aliitaka serikali iongeze posho za wabunge kutoka Shilingi 150,000 hadi Shilingi 500,000 kwa siku, kwa kuwa kiwango cha sasa hakitoshi.

“Hili suala la posho ambalo ndilo chanzo cha haya, nakwambia siyo msimamo wa chama kama wanavyowaambia Watanzania, huo ni uamuzi wao wawili tu kwa sababu katika vikao walikuwa wanawatisha wabunge na kuwatishia kwamba watawafukuza kama hawatakubali kukataa posho. Huwezi kuendesha chama kwa nguvu kwa sababu hizo posho ndicho kipozeo cha mbunge, kwani kama ng’ombe anayekamuliwa akikosa malisho ukimkamua ujue atatoa damu. Sasa kama ndivyo hivyo, wabunge wasipolipwa posho kazi zao watafanyaje, katika hili siwezi kunyamaza, nitaendelea kuheshimu uongozi kwa ajili ya kujenga ufanisi wa maslahi ya chama ya kutajirisha masikini dhidi ya vatu, cheo ni dhamana. Sitoona haya kukosoa tabia ya umimi na uyeye kwa mtu yeyote, sitahama CHADEMA kwa sababu sikutofautiana na chama bali nimetofautiana na watu wachache kutokana na kutoridhishwa na uongozi wao,” alisema.



SHUTUMA DHIDI YA ZITTO

Akimchambua Zitto, alisema anajifanya mzalendo machoni pa watu wakati tabia na matendo yake ni tofauti na anavyowaambia Watanzania.

“Zitto siyo mzalendo, namtaka aache tabia ya ukuwadi na kuunda uzandiki wa kufunika uwazi na ukweli kwa dhamira ya ubinafsi wa kujikweza kisirisiri ili apendwe na uongozi na kuidanganya jamii kwamba yeye ni mwadilifu. Zitto asigandamize haki za watu, wanaojua stahili zao kwa sababu yeye anajipamba ili asihitilafiane na kiongozi wake kwa masilahi yake binafsi, aache tabia ya kujifanya mzalendo wakati ni mnafiki anayetaka kujenga matarajio yake binafsi huku akificha ajenda ya siri ya umimi na uyeye. Ili kutambua tabia yake na mwenzake huyo ni sawa na mwenye kiatu ambaye ndiye anayejua jinsi kinavyomuumiza badala ya mtazamaji ambaye anafurahishwa na rangi ya kiatu, aache kabisa tabia hiyo awe wazi na asitafute umaarufu,” alisema.

Alisema kinachomgombanisha na wenzake ndani ya chama hicho ni tabia yake ya kupenda uwazi, wakati baadhi ya wenzake wanataka ukweli usielezwe kwa wananchi.

“Chuki iliyopo ni kwamba mimi Shibuda napinga chama kuwa kama kampuni ya kuingiza wanachama wa kutekeleza masilahi binafsi ili kudumisha ukabila, uyeye, umimi, uwao, umajimbo ambao umefichwa na msemo usemao siri ya mtungi aijuaye kata. Binafsi sitarudi nyuma, naahidi kulinda maslahi na kutetea shabaha ya CHADEMA kwa maslahi ya wananchi, nitaendelea kupingana na tabia ya kuwaonea watu kwa sababu wabunge maskini kama mimi tunapata fedha za kuwahudumia wananchi kwa kudunduliza fedha za mishahara na posho. Wabunge matajiri wao wana mapokeo ya hisa kutoka katika biashara zao binafsi, kwa hiyo ndondondo za mapato kutoka bungeni hawazihitaji, ndiyo maana wanawalazimisha wenzao wasiokuwa na kitu wafuate nyayo zao hata kama wanawaumiza,” alisema.

Kutokana na hali hiyo, Shibuda alisema atahutubia mikutano ya hadhara wakati wowote mwishoni mwa mwezi huu baada ya kurejea nchini, ili kuweka wazi tabia za badhi ya viongozi wa chama hicho.





KAULI YA MBOWE

Akijibu shutuma hizo, Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Freeman Mbowe, alisema hapendi malumbano kupitia biombo vya habari, “Kamanda sipendi malumbano kwenye vyombo vya habari, tusubiri muda ukifika ukweli utajulikana tu,” alisema Mbowe.

- MTANZANIA


KAULI YA ZITTO

Zitto amesema msimamo wa kumfukuza Shibuda upo pale pale kwani kambi hiyo wala CHADEMA hawawezi kumwacha mbunge anayekiuka sera na kuwadhalilisha viongozi hadharani.

"Shibuda hatafukuzwa kinyemela, lazima taratibu zifuatwe kwa Mnadhimu Mkuu wa kambi yetu kumwandikia barua ya kumweleza makosa yake na yeye kupata fursa yakujibu shutuma hizo. Pili, ataitwa katika Kamati Kuu ya chama chetu (CHADEMA) nao watatoa uamuzi wao... Chadema si chama cha kihuni kwamba tutakurupuka ni lazima haki itendeke na mimi sipendi mtu aonewe, Shibuda atapata haki zake zote kama mwananchama. Mbunge yeyote wa CHADEMA anapaswa kujua akienda kinyume na sera ya chama atafukuzwa”.

Alisema suala la posho lipo kwenye Ilani ya uchaguzi wa 2010 kwa hiyo ni sera, na kwamba anayepinga atafukuzwa tu na kwamba CHADEMA wataanza na Shibuda.

Zitto alisema "Shibuda anajua mie humtetea sana, lakini anapokwenda kinyume na sera ya chama tutamfukuza, aniite majina yoyote tu akienda kinyume na sera nitakuwa wa kwanza kumfukuza...

"Kuna masuala ya nidhamu kwenye bunge na wabunge wa chama fulani inaitwa "three line whip", masuala ya msimamo wa kitendaji mfano tulipokaidi kwenda bungeni kutoka nje ya ukumbi wakati Rais Jakaya Kikwete alipokuwa akihutubia bunge (walk out), haya ni ya kawaida na hayana adhabu kali, lakini likiwa la sera adhabu ni kufukuzwa, Shibuda asipaparike," alisema Zitto.
 
Huyu shibuda ni ovyoooo ni mnafiki Kama Mrema fukuzeeni ni afadhali kukaa bila mbunge kuliko fedhaa za huyu nyangumi
 

KATIBA YA CHADEMA

UANACHAMA:
5.1 Sifa za kuwa MwanaChama


5.1.1 Awe raia wa Tanzania.
5.1.2 Awe na umri wa miaka 18 au zaidi
5.1.3 Awe na akili timamu
5.1.4 Awe anakubaliana na katiba, sera, kanuni na maadili ya Chama.
5.1.5 Awe anakubaliana na Itikadi na falsafa ya Chama
.
5.1.6 Asiwe mwanaChama wa Chama kingine cha siasa baada ya kujiunga na CHADEMA.

Kupinga posho lilikuwa ni wazo la Zitto au ni Katiba, Sera, Kanuni, Maadili ya Chama, Itikadi au Falsafa ya CHADEMA?

Na kama imeandikwa sehemu kwamba kupinga posho ni
Katiba, Sera, Kanuni, Maadili ya Chama, Itikadi au Falsafa ya CHADEMA ni kwa nini Lissu asifukuzwe uanachama: Hivi tunavyoongea hapa Lissu anakula posho ya Wabunge, kwa sababu hakuna mtu hata mmoja aliyerudisha posho, uongozi wa Bunge na Serikali walikataa ku entertain kukataa posho, kupokea back posho ya mtu. Kwa hiyo Lissu anakula posho, afukuzwe CHADEMA kwa kukiuka Katiba, Sera, Kanuni, Maadili ya Chama, Itikadi au Falsafa ya CHADEMA?

upuuzi mtupu umetumwa au?
 
shibuda ni mnafiki ametumwa kuvuruga chama,amekaa muda mfupi ameleta matatizo mengi kwa ushauri wangu aturudishie kadi yetu,
 
Back
Top Bottom