Lissu aitimulia vumbi CCM Babati, 1500 wajiunga Chadema, we acha tu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lissu aitimulia vumbi CCM Babati, 1500 wajiunga Chadema, we acha tu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Apr 27, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Apr 27, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  WanaCCM 1500 Wajivua magamba na kuvaa magwanda
  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimezidi kupoteza nguvu zake sehemu mbalimbali nchini, baada ya waliokuwa viongozi na makada wake ngazi za vijiji na wilaya kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Habari kutoka mikoa ya Manyara, Iringa na Kagera zimesema kuwa wimbi la kukimbia kwa wanachama wa CCM na kujiunga na upinzani limeshika kasi kuliko mwaka wowote tangu kuingia kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa.
  Huko Babati zaidi ya wanachama 1,500 wa CCM wakiwamo wenyeviti wa vijiji wilayani Babati wamekihama chama hicho na kujiunga na CHADEMA, wakati wa mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki, Tundu Lissu. Kati ya waliojiunga na CHADEMA ni pamoja na Bi. Zamda ambaye ni kada maarufu wa CCM mjini hapa, Wakili Lumambo na wenyeviti wawili wa vijiji vya Mruki na Hala, ambao walijiunga na wanachama wao zaidi ya 100.

  Akihutubia mkutano huo, Lissu amewataka wananchi wa Jimbo la Babati Mjini na wengineo kuiga mifano ya waliokataa kuonewa na kunyanyaswa na serikali ya CCM badala yake wachukue hatua ili kuondoa uvundo, wizi na uozo unaoendelea kufanywa na watawala.
  "Hatujaweka mkataba wa kuibiwa na serikali ya CCM kwa kipindi cha miaka mitano mitano, kwa hiyo hatuhitaji kusubiri hii miaka mitatu ya uchaguzi iliyobaki. Wakati umefika sasa wa kuchukua hatua, tukianzia na hili suala la mawaziri wanane, na pamoja na umaskini wetu tukiamua kusema kwa pamoja hakuna mtu atakayeweza kutuzuia," alisema Lissu.


  Iringa nako Chadema yapangua gear kuongeza kasi
  Huko Iringa, Mwenyekiti wa Kijiji cha Kihesa Mgagao, Kata ya Ng├║ruwe, wilayani Kilolo, Isdori Kindole na wazee wawili, Tula Dumba (75) na Japhet Ngoda (88) wamejiunga na CHADEMA kutokana na kile walichodai kuwa wameshindwa kupata haki ya kweli kutoka katika chama hicho kupitia uongozi wao wa kijiji hususan diwani wao kutuhumiwa kuhujumu mali za umma. Wazee hao wamedai kuwa wao waliingia kwenye TANU wakati Rais akiwa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, walipata fursa ya kukaa pamoja na kuzungunza juu ya mambo mbalimbali yakiwamo ya chama pamoja na maendeleo ya Watanzania kwa ujumla.

  Akindole alisema sababu kubwa iliyomfanya kuhamia CHADEMA ni kuona uongozi wa CCM wa sasa ukiwanyanyasa wananchi kupita kiasi na kunyamazishwa pindi wanapokuwa na maneno ya kushauriana juu ya maendeleo ya kijiji chao. "Kwa sababu hiyo mimi nimeamua kutoka kwenye Chama cha CCM na kuhamia CHADEMA ili nijaribu kuona msimamo unakwendaje, maana tunanyanyaswa kupita kiasi na tukitaka kulalamika serikali haitusikilizi, na mbunge akija hapa tukilalamika hata yeye hatusikilizi. Mimi nilikuwa na mambo yangu mengi tu nimelalamika mpaka wilayani lakini sikusikilizwa. Tufanyeje wananchi?'' alisema Japhet.


  Kwa upande wake mzee Tula amesema kuwa, wakati wa uongozi wa Mwalimu Nyerere kulikuwa na viongozi waliokuwa wamepata mafunzo ya uongozi kwa lengo la kuwasaidia wananchi lakini kwa sasa wananchi wakilalamika viongozi hawatoi msaada wowote zaidi ya kukandamizwa kutokana na viongozi wengi kukosa maadili ya uongozi. "Hapa nilipo nina miaka 75, mzee kama mimi sikuwa na haja ya kuhama hama chama, lakini ninatafuta msaada, kama CCM kungekuwa na msaada viongozi wasio bora wangekuwa wanaonywa na kufuata maadili ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, kwa kweli nisingehama," alisema Tula.


  Aidha, wazee hao wamesema kuwa, licha ya wao kuhamia CHADEMA, lakini bado wanaiomba serikali kumchukulia hatua mwenyekiti huyo wa Kijiji cha Kihesa Mgagao ambaye pia ni diwani wa kata na mwenyekiti wa CCM, kwani hawatendei haki wazee wa kijiji hicho na wananchi kwa ujumla na uongozi wake ni wa kidikteta.  CHADEMA yaiburuza CCM Uchaguzi Geita

  Huko Chato, katika Mkoa mpya wa Geita, CHADEMA kimepata ushindi wa kishindo katika uchaguzi mdogo wa wenyeviti wa serikali za vijiji baada ya kuibwaga CCM kwa kupata vijiji vinane kati ya 11 vilivyokuwa vikishindaniwa. Uchaguzi huo mdogo wa kuziba nafasi zilizoachwa wazi na baadhi ya viongozi waliokuwepo awali jimboni humo kutokana na sababu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na vifo ambao ulifanyika hivi karibuni uliwafanya baadhi ya Wana CCM kujiunga na CHADEMA mara baada ya matokoeo kutangazwa akiwamo aliyekuwa mgombea wa CCM wa Kijiji cha Minkoto.

  Nafasi zilizogombewa zilikuwa zikishikiliwa na viongozi wa CCM kabla ya baadhi yao kujiuzulu, kuhamia vyama pinzani na wengine kuhama makazi yao na kwenda maeneo mengine. Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari, msimamizi msaidizi wa uchaguzi huo, Sodio Nyuga alisema CHADEMA kimefanikiwa kutwaa nafasi 8 za vijiji dhidi ya tatu zilizonyakuliwa na CCM . Hata hivyo, CCM ilijifariji kwa kutwaa uenyekiti katika vitongoji 28 na CHADEMA kikipata nafasi 10, wakati wajumbe wa serikali za mitaa CCM kilijipatia wajumbe 92 na CHADEMA 46.


  Katibu wa CHADEMA wa Wilaya ya Chato, Mange Sai, alisema ushindi uliopatikana ni ukombozi mkubwa kwa wananchi wa wilaya hiyo kwa kuwa baadhi ya vitongoji CHADEMA ilipitisha wagombe pasipo kuwa na upinzani wa chama tawala jambo ambalo linaonyesha wazi kukubalika kwa chama hicho kwa wananchi. Alisema kuwa CHADEMA kilitegemea kuibuka kidedea katika uchaguzi huo mdogo kutokana na wapiga kura kuchoshwa na ahadi mbalimbali za serikali ya CCM ambazo zimekuwa hazina utekelezaji na badala yake baadhi ya viongozi wamekuwa wakijinufaisha kwa maslahi yao binafsi huku wakiwaacha wananchi wakitaabika.

   
 2. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #2
  Apr 27, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Lisu ubunge leo mwisho
   
 3. M

  Molemo JF-Expert Member

  #3
  Apr 27, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Mungu wangu hii ni kufuru sasa
   
 4. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #4
  Apr 27, 2012
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Inawezekana ni kweli kwa vile mahakama zetu zinafanya kibarua cha ziada kuiokoa CCM
   
 5. K

  Kwayu JF-Expert Member

  #5
  Apr 27, 2012
  Joined: Nov 8, 2007
  Messages: 487
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hakuna tatizo ataungana na Lema kueneza m4c
   
 6. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #6
  Apr 27, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Ukombozi wa Tz toka kwa mkoloni mweusi ccm utafanywa na watz wenyewe
   
 7. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #7
  Apr 27, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  mi naona huku ni kupoteza tu hela za walipa kodi, hata akivuliwa ubunge...uchaguzi ukifanyika tena chadema itashinda ni sawa sawa na kule arusha wamemvua lema lakini kila mtu anajua kua uchaguzi ukifanyika tena cdm wanashinda sa ya nini kupoteza tu hela...kila siku tunaambiwa nchi haina hela alafu karibia kila mwezi kuna chaguzi za ubunge...aah:eek:hwell:
   
 8. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #8
  Apr 27, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Long live kamanda Lissu, long live Chadema.
   
 9. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #9
  Apr 27, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,108
  Likes Received: 6,583
  Trophy Points: 280
  Mpambe

   
 10. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #10
  Apr 27, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,108
  Likes Received: 6,583
  Trophy Points: 280
  Lissu be strong man.
  songa mbele mkuu.
   
 11. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #11
  Apr 27, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  watampa likizo tu kama lema aeneze ujumbe wa CDM hadi kwenye mizizi waliko wapiga kura wengi!
   
 12. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #12
  Apr 27, 2012
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,499
  Likes Received: 1,078
  Trophy Points: 280
  Viva Chadema, VIVA!!!!!!!!!!!!
  Magamba zii!! yaani sasa hivi inafikia chadema mgombea wake anapita bila kupingwa kutokana na CCM kutokuwa na mgombea!!!
   
 13. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #13
  Apr 27, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Acha Mkwara Mkuu! Unamaanisha Mahakama itamkomoa kwa kuivuruga ccm?
   
 14. R

  Radi Member

  #14
  Apr 27, 2012
  Joined: May 22, 2010
  Messages: 94
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Hata kama itakuwa hivyo hapajaharibika kitu.Si unajua pale kwenye jimbo la Lisu wanamwita ,,Ighamba". yaani ni lile dume la ng'ombe. Kwa hiyo sasa hivi hata wakirudia uchaguzi CDM watashinda kama vile kumsukuma mlevi.
   
 15. p

  peter tumaini JF-Expert Member

  #15
  Apr 27, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 575
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  safi sana makamanda tunaelekea pazuri tunahitaji kukaza buti.
   
 16. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #16
  Apr 27, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Unatia kinyaa kwa kufuka moshi wazi wazi. Huoni tulipo, tunapokwenda mpaka umuombee mabaya mpiganaji Lisu?
   
Loading...