Lissu afichua mapya sakata la Lwakatare

Lissu afichua mapya sakata la Lwakatare

SIMON CONDRAD

Member
Joined
Oct 16, 2012
Posts
9
Reaction score
10
Mwanasheria wa CHADEMA,Tundu Lissu, amesema wamebaini kuwepo kwa mawasiliano zaidi kati ya Mwigulu Nchemba na mtuhumiwa mwenza wa Lwakatare, aitwaye Ludovick Joseph.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Lissu alidai kuwa tarehe Januari 14, mwaka huu, namba ya simu+255756008888- ya Nchemba inayoonekana kwenye kitabu cha mawasiliano ya wabunge ilituma kiasi cha sh 50,000 kwenda kwa Ludovick.

“Mtakumbuka kuwa video hiyo inayodaiwa kuwa ya kupanga ugaidi ilichukuliwa Desemba 28 mwaka jana, siku moja baadaye Nchemba, kupitia kituo cha Star tv alitangaza kuwa anayo CD ya viongozi wa CHADEMA wakipanga mauaji na akarudia tena Jabuari 2 mwaka huu.

“Sasa tunajiuliza Naibu Katibu Mkuu wa CCM alikuwa na biashara gani na mtuhumiwa wa ugaidi Ludovick, ikizingatiwa pia kuwa siku hiyo hiyo ambayo mkanda ulichukuliwa waliongea kwenye simu?!” alisema Lissu.

Aliongeza kuwa kuna njama kubwa alizodai zinapangwa na dola ili Lwakatare athibitike kuwa alifanya matendo ya kigaidi na hatimaye ionekane kuwa chama anachokitumikia kama Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama kinajihusisha na ugaidi.

Aliongeza kuwa Kamati Kuu ya CHADEMA imejadili kwa kina suala la Lwakatare na kuamua kuwa masuala yote yanayohusu njama dhidi yao kupitia sakata la Lwakatare ni muhimu yawekwe wazi hadharani kadiri inavyowezekana ili Watanzania wajue hujuma dhidi ya chama hicho.

“Napenda kurudia hekaheka zinazoonekana sasa kupitia hata vyombo vya habari kama vile magazeti kuwa CHADEMA inahusika na ugaidi na kupanga njama za mauaji, ni mwendelezo wa propaganda,” alisema Lissu.

Katika mlolongo wa madai hayo, Lissu alisema pia kuwa chama hicho kimebaini kuwepo kwa mawasiliano ya mara kwa mara kati ya Ludovick na mtu aitwaye Dennis Msaki ambaye kwa mujibu wa jalada la polisi katika hati ya mashtaka ndiye anadaiwa kupangiwa njama za kutekwa na Lwakatare na Ludovick.
 
Sisi tunafuatilia kwa makini. Hatulishwi kasa kirahisi na wapinga mabadiliko. CHADEMA itavuka salama na hapa. Tunataka siasa za sera...si siasa za hela na porojo
 
Siasa za kuhongana 50,0000 kudadeki umaskini huu!! Mtatumika kama napkins na mwisho wa siku watanzania hawaelewi somo lenu la kizandiki na kubambikizia kesi CDM na wanachama wake. Hii ilitumika miaka ya kweusi ikaweza kufanya kazi lakini kwa wakati huu wa science na teknolojia hata kule vijijini hawadanganyiki tena. Kila la heri Gambaz.
 
Siamini kama unaweza kupewa elfu 50 halafu ukakisaliti chama.ngoja nisubiri uamuzi wa mahakama.
 
CCM hata mfanyeje yaani kuliko kuwabakisha madarakani ni bora nikalipigie jiwe kura yangu 2015 lakini si nyinyi wauaji
 
Uzuri wa mawakili au viongozi wa cdm wanafanya utafiti kwa mambo yanayo wakabili. Kama kweli nchemba ana mawasiliano na ludovick basi inatakiwa akamatwe awe mtuhumiwa namba tatu. Mungu ameamua cdm iwepo na hakuna atakaye zuia.
 
Nchi yetu inahitaji kuwa na wapelelezi wa kujitegemea (wapelelezi huru), kesi kama hizi za mkwe na mkamwana kugombea mwiko na upanio wa sufuria ya ugali hazitakuwepo.
 
Mi nadhani kazi ya mawakili wa CDM iwe kuonyesha kuwa mteja wao hana hatia, issue ya nani mwingine anahusika ni ya POLISI
 
Huo ni ushahidi wa kupeleka mahakamani kuliko kutoa katika vyombo vya habari, hii inatoza nafasi kwa upande wa pili kujiandaa
 
Uzuri watanzania wanajua yote kuhusu njama za Chama tawala kutaka kuizoofisha chama chwa wananchi wa kawaida na wazalendo wapenda nchi yao ya Tanzania Chadema. Kura zitaamua 2015.
 
Jamaa ana dhiki kuu yaani 50,000tshs tuu sasa angepewa 500mil si angeweza ata vaa bomu ajilipue na viongozi kwa kughadhilika na mkwanja
 
Siamini kama unaweza kupewa elfu 50 halafu ukakisaliti chama.ngoja nisubiri uamuzi wa mahakama.
Kama kuna watu wanahongwa kofia tuu siku ya uchaguzi na wanasaliti nchi sembuse huyo aliyepewa elf50 kukisaliti chama!!
 
Mwigulu unaipeleka nchi ktk machafuko damu za watanzania zinamwagiga kwa ajili ya siasa zako chafu!WITO WANA CHADEMA TUHAKIKISHE HUYU MTU HAPATI UBUNGE 2015,mimi kila mnyiramba namwambia madhara ya kuwa na huyu mtu
 
Hawa ndo inabidi wawe watuhumiwa wa kwanza kwanza kupelekwa the Hague by Dec 2015
 
Siamini kama unaweza kupewa elfu 50 halafu ukakisaliti chama.ngoja nisubiri uamuzi wa mahakama.

huu ndio upuuzi wa wapuuzi wa cdm kuandika kwa kutumia masabur .just 50.ugaidi umewashika makalio
 
CCM hata mfanyeje yaani kuliko kuwabakisha madarakani ni bora nikalipigie jiwe kura yangu 2015 lakini si nyinyi wauaji

pigia kura jiwe liwe rais wako mm nasubiri atakayepitishwa na chama changu ccm
 
Back
Top Bottom