Lissu afichua mapya sakata la Lwakatare

Lissu afichua mapya sakata la Lwakatare

Kama alivyosema Lissu, chama kinapaswa kuweka wazi kila njama itakayokua imegundulika kuandaliwa na ccm dhidi ya rwakatare yenye nia mbovu ya kukihujumu chadema.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
rwakatale hachomoki bado slaa

ndoto za namna hii waachie watoto wako wewe zinakudhalilisha mkuu!.
HAMTAFANIKIWA HATA MOJA KWA YOTE MLIYOYAPANGA DHIDI YA CHADEMA.....hifadhi maneno yangu!
 
Wafanye wafanyalo chadema ndio chama cha wnyonge na dr slaa ndio rais wa mioyo ya watanzania wazalendo
 
Wala Lissu asihangaike kujibizana na mafisadi kupitiavyombo vya habari, ni wazi kuwatumekwisha wagundua CCM so hata wangetafuna njia mbovu dunia nzima za kuvichafua vyama vya upinzani, wala hatutakubali kudanganywa!!!!
 
Mi nadhani kazi ya mawakili wa CDM iwe kuonyesha kuwa mteja wao hana hatia, issue ya nani mwingine anahusika ni ya POLISI

Kudhihirisha kuwa mteja hana hatia ni kazi ya mawakili mahakamani na katika mtandao ni kutuonesha nani yuko nyuma ya picha nzima ilioko sokoni hivi sasa!
 
Mwanasheria wa CHADEMA,Tundu Lissu, amesema wamebaini kuwepo kwa mawasiliano zaidi kati ya Mwigulu Nchemba na mtuhumiwa mwenza wa Lwakatare, aitwaye Ludovick Joseph.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Lissu alidai kuwa tarehe Januari 14, mwaka huu, namba ya simu+255756008888- ya Nchemba inayoonekana kwenye kitabu cha mawasiliano ya wabunge ilituma kiasi cha sh 50,000 kwenda kwa Ludovick.

“Mtakumbuka kuwa video hiyo inayodaiwa kuwa ya kupanga ugaidi ilichukuliwa Desemba 28 mwaka jana, siku moja baadaye Nchemba, kupitia kituo cha Star tv alitangaza kuwa anayo CD ya viongozi wa CHADEMA wakipanga mauaji na akarudia tena Jabuari 2 mwaka huu.

“Sasa tunajiuliza Naibu Katibu Mkuu wa CCM alikuwa na biashara gani na mtuhumiwa wa ugaidi Ludovick, ikizingatiwa pia kuwa siku hiyo hiyo ambayo mkanda ulichukuliwa waliongea kwenye simu?!” alisema Lissu.

Aliongeza kuwa kuna njama kubwa alizodai zinapangwa na dola ili Lwakatare athibitike kuwa alifanya matendo ya kigaidi na hatimaye ionekane kuwa chama anachokitumikia kama Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama kinajihusisha na ugaidi.

Aliongeza kuwa Kamati Kuu ya CHADEMA imejadili kwa kina suala la Lwakatare na kuamua kuwa masuala yote yanayohusu njama dhidi yao kupitia sakata la Lwakatare ni muhimu yawekwe wazi hadharani kadiri inavyowezekana ili Watanzania wajue hujuma dhidi ya chama hicho.

“Napenda kurudia hekaheka zinazoonekana sasa kupitia hata vyombo vya habari kama vile magazeti kuwa CHADEMA inahusika na ugaidi na kupanga njama za mauaji, ni mwendelezo wa propaganda,” alisema Lissu.

Katika mlolongo wa madai hayo, Lissu alisema pia kuwa chama hicho kimebaini kuwepo kwa mawasiliano ya mara kwa mara kati ya Ludovick na mtu aitwaye Dennis Msaki ambaye kwa mujibu wa jalada la polisi katika hati ya mashtaka ndiye anadaiwa kupangiwa njama za kutekwa na Lwakatare na Ludovick.

Kwa kuwa siku hizi kuna technology ya ku hack simu, inaonekana akina Lisu wako na matumaini kuwa wamewin.
 
twende mbele turudi nyuma, Ludovik is a sick mofo, kama kuna mtu amewahi kusoma anavyoandika, utajua kabisa kuna kitu ndani yake na ni laana
 
Siasa bwana!!!! we acha tu! ngoja tuone movie itaishiaje.Bila shaka rwakatale atafikishwa The Heague!
 
.... Ile video ni orijino au feki.,.??
Hilo sijalielewa bado.
 
Mwigulu unaipeleka nchi ktk machafuko damu za watanzania zinamwagiga kwa ajili ya siasa zako chafu!WITO WANA CHADEMA TUHAKIKISHE HUYU MTU HAPATI UBUNGE 2015,mimi kila mnyiramba namwambia madhara ya kuwa na huyu mtu
Nilishawahi kusema humu jamvini, CDM waache siasa za majukwaani na kuwafuata wananchi huko vijijini nikaonekana wa ajabu sana. Hivi Kama CDM wanatumia akili na Kama wanaamini hizo mbinu chafu zimefanywa na Mwigulu, hivi alikwenda na kaseti na kuiweka mdomoni mwa Rwakatare ili ionekana maneno hayo kayasema Rwakatare? Akili ni nywele na kila mtu Ana zake, mmezoea siasa za kichafuana na kuwadanganya wananchi. Rwakatare kakiri kuwa baadhi ya maneno kayasema, Kama ni hivyo CDM man akili kweli?! Dunia Nzima siasa za uongo na kichafuana ndo zilivyo, mnavuna mlichopanda. Usitegemee kulima bhangi halafu ukavuna mahindi. R I P CDM
 
twende mbele turudi nyuma, Ludovik is a sick mofo, kama kuna mtu amewahi kusoma anavyoandika, utajua kabisa kuna kitu ndani yake na ni laana

Hizi za sasa ni vita vya propaganda tu zinazoendeshwa na CHADEMA

Kama Rwakatare hakuhusika na chochote, huyo Ludovick angemrikodi vipi?
 
Hizi za sasa ni vita vya propaganda tu zinazoendeshwa na CHADEMA

Kama Rwakatare hakuhusika na chochote, huyo Ludovick angemrikodi vipi?
Hivi we bibi umeona popote nimesema lwakatare hakuhuika?

ule mkanda ni real, and fyi, my reference is trace-passing trust, leo nikiongea na wewe kwa kuaminiana, and then kesho nikiyasikia mazungumzo yetu somewhere, nitakuita kirusi


i think unasoma sana sasa akili imekua kama matarasi tu, you cant think of anything outside what is written by someone else

shughulisha ubongo
 
Hivi we bibi umeona popote nimesema lwakatare hakuhuika?

ule mkanda ni real, and fyi, my reference is trace-passing trust, leo nikiongea na wewe kwa kuaminiana, and then kesho nikiyasikia mazungumzo yetu somewhere, nitakuita kirusi


i think unasoma sana sasa akili imekua kama matarasi tu, you cant think of anything outside what is written by someone else

shughulisha ubongo

You are not making any sense

Oh well, let me go shughulisha ubongo somewhere else
 
You are not making any sense

Oh well, let me go shughulisha ubongo somewhere else
you are right, no sense at all... A bunch of typos and trespassing


ila ujumbe umefika
 
huu ndio upuuzi wa wapuuzi wa cdm kuandika kwa kutumia masabur .just 50.ugaidi umewashika makalio
hivi bado haujakua mpaka sasa, kuna watu tunawafahamu wamelisaliti TAIFA la Tanzania kwa pakiti ya chumvi, kofia, tisheti, kanga. Sasa wewe unashangaa sh. Elfu hamisini, eti just 50, kuna watu wana njaa ya hela wako tayari hata kukuuza wewe hapo ulipo, ua umesahau yaliyotokea Dodoma, kwa wale wananchi ambao wamejenga nyumba zao tokea miaka ya 2000, 7-ten yrs later, nyumba zao zikabomolewa, na mtu aliyenunua ardhi wakati wao wanaishi hapo bila kujua. Leo kweli tunaitana magaidi kwa suala la kitoto kama hili, mbona majambazi wanatufanyizia sana hutuja thubutu kuwaita magaidi, ila kwa wapinzani wa kisiasa we dare to call them terrorists, very likely we heading to a wrong way. Anyway samahani inawezekana mnyama anayeitwa umaskini wa kipato ongeza na ule umaskini wa fikra jawaribu lake hulijui
 
Kama jambo hili halina ukweli na limetungwa tu, inaonyesha jinsi gani hofu ya Mungu ilivyokosekana ndani ya Mwigulu Nchemba na kufikia kufanya jambo la hatari namna hii na siyo tu kwa kina Rwakatare bali kwa watanzania wote tunaotaka mabadiliko. Nawaomba watanzania wenzangu tusiogope vitisho vya FARAO (CCM) kwani tayari Mungu amemtuma mtumishi wake MUSA (CHADEMA) kutupeleka ktk nchi iliyojaa maziwa na asali
 
wauwaji walimuua baba yako? siyo bule utakuwa umelogwa
 
Sio Slaa. Sema Gaidi Dr Kanjanja Slaa. Hukumbuki aliahidi kuwa nchi haitatawalika?

wanachama wa hichi chama changu bwana wao wanaamini viongozi wao wasafi zaidi ya manabii na hawawezi fanya ovu lolote jamani slaa, mbowe, lwakatare na wengine ni binadamu so tungoje mahakama iamue tusiwe majudge, kisa tu chama tawala kinatawala mbona majimbo kam mwanza, mbeya, arusha na kwingine tunayamiliki chama tawala si kina ona so tuwe wapole kama ipo ipo tu hata mtu abane vip.
 
Back
Top Bottom